Welcome to our online store Portal

Template Information

Monday, December 31, 2012

Waasi wa CAR wakataa pendekezo la rais Bozize


Rais wa CAR akiwahutubia wanainchi mjini Bangui

Waasi nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wamekaribia mji mkuu wa nchini Bangui na wamepuuzilia mbali, tangazo la rais wa nchini hiyo Francois Bozize, siku ya Jumapili, kuanzisha mazungumzo ya amani na viongozi wao.
Msemaji wa waasi wa Eric Massi, ameiambia azizicompdoc.blogspot.com kuwa, ni vigumu sana kwao kumuamini rais Bozize, kwa sababu wanajeshi wake wanaendelea na harakati za kuwashambulia wapiganaji wao mjini Bangui.
Amesema, ikiwa jeshi la kutunza amani la Muungano wa Afrika , halitatumwa mjini Bangui, waasi hao wataingia na kutoa ulinzi wa wafuasi wao.
Lakini serikali ya nchi hiyo imekanusha madai hayo, ya kuwafanya mashambulio dhidi ya wafuasi wa waasi hao.
Siku ya Jumapili, rais Bozizi alitangaza kuwa yuko tayari kuunda serikali ya muungano wa kitaifa na waasi hao na kuwa hatawania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2016.
View detail

Kanisa lashambuliwa na watu 2 kuuawa



Viongozi wa Kanisa la Coptic

Raia wawili wa Misri wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa, kwenye shambulio liliotekelezwa dhidi ya kanisa moja la Coptic mjini Misrata.
Afisa mmoja wa baraza la mji huo ameiambia azizicompdoc.blogspot.com kuwa kumetokea mlipuko ndani ya jengo la kanisa hilo wakati wanne hao walipokuwa wakila chakula chao cha mchana.
Haijulikani ni nani aliyefanya shambulio hilo mjin Dafiniyah, viungani wa Misrata.
Hata hivyo kuna habari za kutatanisha kuhusu ni lini shambulio hilo lilitokea.
Afisa huyo asema kanisa hilo lilishambuliwa kwa bomu la kujitengenezea, kwa kuwa baruti zinazotumika kwa uvuvi zilipatikana katika eneo hilo
Shirika la habari la serikali limesema kuwa, serikali ya nchi hiyo imeagiza maafisa zaidi wa polisi kutumwa katika kanisa hilo.

Serikali ya Misri imeagiza uchunguzi

Waziri wa mambo ya nje wa Misri, Mohammed Kamel Amr, amesema, serikali imeagiza uchunguzi kufuatia tukio hilo na kusema waliohusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.


Majengo yaliyoharibiwa wakati wa machafuko ya kisiasa mjini Misrata

Kanisa hilo lililoka katika eneo la Dafiniyah, nje kidogo ya mji wa Misrata, hutumiwa na raia wengi wa Misri.
Kuna idadi ndogo sana ya wakristu nchini Libya, wengi wao wakiwa raia wa kigeni.
Baadhi yao wahamiaji kutoka Misri ambako waumini wa kanisa la Coptic ndilo dhehebu kubwa zaidi la Kikristo.
Serikali ya Libya imekuwa ikikabiliana na matatizo wa kuhakikisha usalama tangu kuondolewa madarakani wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mwaka uliopita.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mashambulio ya kigaidi dhidi ya majengo ya kibalozi na yale ya mashirika ya kutoa misaada na mwezi Septemba mwaka huu, Ubalozi wa Marekani, mjini Benghazi ulishambuliwa na balozi wa Marekani na maafisa wengine waliuawa.
View detail

Watu 8 wafariki Kenya

Familia zilizoathiriwa
Familia zilizoathiriwa kwa mujibu wa Gazeti la Standard Nchini Kenya wakipekuwa mali yao baada ya maporomoko hayo ya Ardhi

Watu wanane wamekufa baada ya nyumba kadha kufukiwa na maporomoko ya ardhi katika eneo la bonde la Kerio, magharibi mwa Kenya, jana usiku.
Maporomoko ya ardhi yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika bonde hilo. Eneo la Kerio pia limekumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayonyesha.
Chama cha Msalaba Mwekundu cha Kenya kinasaidia jitihada za uokoaji na kutoa taarifa kwamba miili miili ya watu wanane imeonekana na watu wengine watano waliokolewa mapema leo.
Watu wengi hawana makaazi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji au kufukiwa na maporomoko ya ardhi.
View detail

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MZEE MOHAMED ABOUD


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib  Bilali, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Iddi, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam  Desemba 29, 2012.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi ya Marehemu Mohamed Aboud Mohamed, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu, katika Makaburi ya Ngazija jijini Dar es salam ,Desemba 29, 2012.

PICHA NA IKULU
View detail

Friday, December 28, 2012

NPP mahakamani kupinga matokeo Ghana


Nana Akufo Addo

Kiongozi wa NPP Nana Akufo
Chama kikuu cha Upinzani nchini Ghana kimewasilisha kesi katika mahakama kuu zaidi nchini humo kupinga ushindi wa rais John Mahama katika uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi huu.
Chama cha National Patriotic Party (NPP) kimepinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika tarehe Saba Desemba, ikidai ulikumba na udanganyifu mkubwa.
Tume ya uchaguzi nchini humo ilisema kuwa Bwana Mahakama alipata asilimia 50.7 ya kura zote zilizopigwa, idadi ambayo ni kubwa na hivyo kuepuka duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya mgombea wa chama cha NPP Nana Akufo-Addo, ambaye alipata asilimia 47.7 ya kura.
Waangalizi wa kimataifa walisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
Chama hicho cha NPP, kimesema imewasilisha kesi hiyo baada ya kuchunguza takwimu kutoka kwa vituo elfu ishirini na sita vya kupigia kura, vilivyokujwa na zaidi ya kura milioni kumi na moja.
Akufo-Addo alishindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais mwaka wa 2008, kwa asilimia moja lakini alikubali matokeo hayo.
Bwna Mahama wa chama cha National Democratic Congress party, alikuwa makamu wa rais wa Ghana hadi kifo cha ghafla cha rais wa hiyo hiyo John Atta Mills, mwezi Julai mwaka huu, ambako aliteuliwa kuhudumu kama kaimu rais wa nchi hiyo.
Taifa la Ghana limekisiwa kuwa nchi iliyo na demokrasia iliyokomaa na thabiti zaidi barani Afrika.
View detail

Marekani yaondoa wafanyakazi wake Bangui

Waasi wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati

Waasi wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati
Serikali ya Marekani, imesema imewaondoa raia wake katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, huku waasi wanaopinga serikali wakikaribia kuingia mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema haijavunja uhusiano wake wa kibalozi na serikali ya nchi hiyo, ila imechukua tahadhari kuhusu usalama wa raia wake.
Marekani pia imeonya raia wake dhidi ya kwenda nchini CAR wakati wa machafuko hayo.
Hali ya wasi wasi imetanda katika mji mkuu wa Jamuhuri ya Afrika ya kati, Bangui, huku waasi wanaopinga serikali wakikaribia kufika mji huo.
Mjumbe mmoja wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC kuwa ameshuhudia raia wa mji huo wakiwa na wasi wasi mkubwa kutokana na na tishio la shambulio.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa umewahamisha wafanyakazi wake wote nchini humo, nayo serikali ya Marekani imetoa wito kwa raia wao kuondoka nchini humo.
Serikali ya Ufaransa kwa upande wake imeagiza usalama kuimarisha katika ubalozi wake mjini Bangui, baada ya kushambuliwa na waandamanaji.
Wanajeshi wa Serikali ya CAR

Wanajeshi wa Serikali ya CAR
Waandamanaji hao walirusha mare ya kuchoma bendera ya Ufaransa.
Raia hao wanataka serikali ya Ufaransa kusiadia kuzima uasi Kaskazini mwa nchi hiyo.
Wanadai serikali ya Ufaransa imewatekeleza.
Ufaransa ina takriban wanajeshi mia mbili mjini Banguia na utawala wa nchi hiyo umetoa wito kwa Ufaransa kuingilia kati na kusaidia kukabiliana na wanajeshi wa waasi ambao wameuteka maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo.
Lakini rais wa Ufaransa Francois Hollande amekataa wito huo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ameliambia shirika la Habari la Reuters kuwa mzozo huo unapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.
View detail

Sakata la mvamizi aliyeungua moto hadi kufa ndani ya nyumba ya mwanamuziki Chameleone wa Uganda lazidi kuchukua sura mpya.


Askari wa upelelezi akifanya vipimo eneo la tukio.(Picha kwa hisani ya newvision.co.ug). 
Baba mzazi wa mtu aliyejulikana kama Robert Karamagi ambaye alifariki kutokana na majeraha ya kuungua kwa moto kwa kile kinachoaminika kuchomwa kwa makusudi ndani ya nyumba ya mwanamuziki Jose Chameleone wa Uganda ameibuka na kusema mtoto wake hakujilipua mwenyewe kama inavyodaiwa.
Karamagi aliyekuwa na umri wa miaka 27 alifariki katika hospitali ya Mulago saa chache baada ya kufikishwa hapo na kulazwa.
Matukio yaliyosababisha Karamagi aliyevamia nyumba ya msanii huyo kukumbwa na mkasa huo bado ni kitendawili huko mke wa Chameleone Bi. Daniella akisisitiza kuwa Karamagi alijitia moto mwenyewe alipotaka kujaribi kumchoma bibie huyo.

Askari wa jeshi la polisi Uganda wakifanya mahojiano na Jose Chameleone (wa pili kushoto) nje ya nyumba yake.(Picha kwa hisani ya newvision.co.ug).
Lakini baba wa mtu huyo Meja Benedict Kyamanywa amepingana na ripoti kuwa mwanawe alijichoma moto mwenyewe. Amesisitiza kuwa mwanaye alifungwa kwa kamba na kuchomwa moto ndani ya makazi ya mwanamuziki huyo.
Ameongoza kuwa kabla mwanaye huyo hajakata roho alimuambia kuwa alifungwa kamba na kuchomwa na mafuta ya ndege.
Hata hivyo katika hatua nyingine Meja Kyamanywa ambaye ni daktari msaidizi wa Kakiri Barracks amesema kuwa mtoto wa alikuwa na matatizo ya akili, na kuwa kijiji kizima kilikuwa kinajua akiwemo Chameleone mwenyewe.
View detail

KKKT waendelea kufukuzana

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Alex Malasusa
HALI imeendelea kwenda halijojo ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, baada ya Mchungaji Philemon Mollel kufukuzwa kazi na kuvuliwa kutoa huduma za kichungaji katika kanisa hilo nchini.
Wiki iliyopita, Bodi ya Dayosisi hiyo chini ya uenyekiti wa Israel Ole Karyongi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa KKKT, ilimtimua kazi Meneja wa Hoteli ya Corridor Springs inayomikiwa na Dayosisi hiyo, John Njoroge kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za hoteli hiyo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao kilichofanyika juzi chini ya Karyongi, zilisema kuwa Mchungaji Mollel ameamuriwa afukuzwe kazi na avuliwe wadhifa za kiroho za kichungaji.
Vyanzo vyetu vya habari ndani ya kikao hicho vilieleza kuwa hatua hiyo ni kutokana na Mchungaji Mollel kushindwa kutekeleza mambo matatu aliyotakiwa na Tume maalumu ya watu watatu walioteuliwa na Menejimenti ya Dayosisi hiyo na alipewa siku tatu kuomba radhi, lakini hakufanya hivyo.
Habari zilieleza kuwa walioteuliwa Desemba 14, mwaka huu na kwenda kumwona Mchungaji Mollel kutekeleza hayo ni pamoja na Msaidizi wa Askofu Mchungaji Solomoni Massangwa, Katibu Mkuu wa Jimbo Arusha Magharibi, Mchungaji Godwini Lekashu na Katibu Mkuu Karyongi.
Taarifa za ndani zilisema Mchungaji Mollel aliandikiwa barua Desemba 17, mwaka huu kufanya mambo matatu kabla ya kufika Desemba 23, mwaka huu.
Habari zilisema katika mambo matatu aliyotakiwa kufanya ni kumwandikia barua ya kuomba radhi kwa Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dk Thomas Lazer kueleza ni kwa nini alimkashifu na kumdharau.
Pili, alitakiwa atoe tamko katika Mtaa wa Azimio ibadani Desemba 23, mwaka huu kuomba radhi kwa yale aliyotamka; na tatu achukue hatua ifikapo Desemba 23, mwaka huu na kumwarifu Katibu Mkuu kwa barua baada ya kuyatekeleza na awe amefanya hivyo kabla ya Desemba 24, mwaka huu.
Vyanzo vya habari vilisema kuwa baada ya Mchungaji Mollel kukaidi hayo, kikao cha watu watatu chini ya Karyongi kiliamua kumfukuza kazi na kumvua uchungaji.
Hata hivyo, habari za uhakika zilisema kuwa Mchungaji Mollel hakufanya hivyo kwa madai kuwa yeye ni mtumishi wa mungu aliyetukuka kufuata maadili na kamwe hawezi kufanya hivyo kwani hakumkashifu mtu wala kiongozi yeyote, bali alieleza ukweli juu ya nani wa kuwajibika katika deni la Sh bilioni 11.
Mbali ya uchungaji, Mollel alikuwa Kiongozi wa Usharika wa Ngateu katika Jimbo la Arusha ni miongoni mwa wachungaji walioamua kuishupalia katika kikao Bodi ya Hoteli hiyo, kuwajibika kwa kufanya ubadhirifu wa mali ya kanisa hilo.
Hata hivyo, Mchungaji Mollel alipopigiwa simu kama amepata nakala ya barua hiyo ya kufukuzwa kazi na kuvuliwa uchungaji, alikiri kuipata, lakini alisema hayuko katika nafasi nzuri ya kulizungumza kwa sasa.
Mchungaji Mollel alisema uamuzi huo umechukuliwa kwa chuki na fitina, lakini haukuangalia madhara ya deni la Sh bilioni 11 iwapo kanisa litashindwa kulipa.
“Nipe muda ndugu yangu, ntakutafuta mimi mwenyewe na nitawaeleza waumini tatizo liko wapi na nani ni tatizo ndani ya Dayosisi hii na kwani nini mimi nimefanywa mbuzi wa kafara,” alisema Mchungaji Mollel.
Awali, Mollel alisema kwa nguvu zote kuwa madai aliyotuhumiwa nayo ni kusema ukweli juu ya madeni ya miradi ya Dayosisi hiyo na ndio chanzo cha barua ya kutaka ajieleze na huo ndio uliokuwa msimamo wake katika kikao hicho cha wachungaji na wakuu wa majimbo.
“Niliweka wazi msimamo wangu katika tulichofanya Desemba 15, mwaka huu kwamba Bodi lazima iwajibike kwa haya yote na kuwataka wenzangu (Wachungaji na wakuu wa majimbo) tusitafune maneno kwa sababu ukweli uko wazi na dhahiri,” alisisitiza Mchungaji Mollel na kuongeza: “Niliwaambia wajumbe wazi kwamba msitufanye wajinga mbele ya washirika, nikasema sipo tayari kuwaambia washirika ndio kwa jambo lisilowezekana na hiyo ndiyo sababu ya kuandikiwa barua hii na nitaweka kila kitu hadharani.”
Kuhusu Njoroge, habari kutoka ndani ya hoteli hiyo zinasema kuwa alitimuliwa kazi wiki mbili zilizopita kutokana na shinikizo la wachungaji wa kanisa hilo kutokana na hali mbaya ya kifedha ya hoteli hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hoteli hiyo, Karyongi alithibitisha kutimuliwa kwa meneja huyo akidai kuwa ni hatua ya kupisha uchunguzi ili kubaini ukweli wa ubadhirifu wa hoteli hiyo na mambo mengine.
“Ni kweli Meneja ametimuliwa ili kupisha uchunguzi wa kina ufanyike kujua ukweli wa hali halisi na sasa timu ya wakaguzi inaendelea na kazi ya kupitia mahesabu ya hoteli hiyo,” alithibitisha Karyongi.
Hata hivyo, habari za ndani za hoteli hiyo na Dayosisi zinasema, hatua ya kufukuzwa kwa meneja huyo ni janja ya viongozi waandamizi wa Dayosisi ambao inasemekana walishirikiana naye kuifilisi kifisadi.
Uchunguzi wa gazeti hili unaonesha kuwa Njoroge ambaye ni raia wa Kenya, amefichwa Dubai na viongozi hao waandamizi wa Dayosisi (majina yanahifadhiwa kwa sasa) ili wasiumbuke kutokana na kadhia hiyo.
Inasemekana hata mali alizokuwa akimiliki Njoroge ikiwamo Klabu ya usiku inayoitwa Brazil iliyokuwa maeneo ya Nanenane Njiro, ameiuza kabla ya kuondoka nchini kinyemela. View detail

Said Salim Bakhresa akamata nafasi ya 30 katika orodha ya watu matajiri 40 barani Afrika


Orodha ya jarida la Forbes la watu 40 matajiri zaidi barani Afrika imetupa jibu la ‘uhakika’ nani ni mtu tajiri zaidi kuliko wote nchini Tanzania. Si mwingine zaidi ya Said Salim Bakhresa ambaye amekamata nafasi ya 30 kati ya matajiri 40 wa barani Afrika kwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 520 hadi kufikia November, 2012.
Bakhresa ana historia ya pekee kwa kuacha shule akiwa na miaka 14 na kujiingiza kwenye biashara ndogo ndogo ikiwa pamoja na mgahawa na biashara ya unga wa kusaga. Leo hii Bakhresa Group imeajiri zaidi ya watu 2,000 na ni kampuni kubwa zaidi Tanzania. Bidhaa zake zina umaarufu mno nchini na nje ya nchi ambazo ni pamoja na unga, vinywaji, ice cream, usafiri wa meli na mafuta miongoni mwa nyingine.
Kampuni ya Bakhresa ni wazalishaji wakubwa zaidi wa unga wa ngano Afrika Mashariki na kati ambayo huzalisha kiasi cha 3,200 za tani za metric. Kampuni yake huendeshwa na wanae wa kiume waliogawana vitengo mbalimbali.

Kwa kuona matajiri wote Africa fuata link hii  Africa-billionaires list View detail

Bakhresa kumwaga mabasi 300, TABOA na wanasiasa wenye vyombo hivyo msilete hujuma!


Itakuwa ni faraja iliyoje sababu tuna imani kwamba kutokana na uwezo wa kifedha na ubunifu mkubwa katika bidhaa na biashara mbali mbali kampuni hii ya mabasi itakuwa na magari ya kisasa na yenye viwango vya juu. 
Nadhani wote tunashuhudia jinsi mabasi mengi ambayo tunapanda yasivyo na viwango na kusababisha ajali za mara kwa mara ukiachilia mbali uzembe wa madereva, viwango vya magari navyo huchangia ajali. Mfano mengi yameundwa kwa chassis za malori ambapo hazi kuundwa mahsusi kwa ajili ya kubeba abiria. Pia watoaji huduma wengi wamekuwa ni wababaishaji.
Zaidi wengi tunajua jinsi biashara hii ya ma bus inavyo milikiwa kwa kiwango kikubwa na wana siasa. Kwa hiyo tunaomba katika hili ushindani uwe wa kweli. Boresheni huduma zenu ili kuweza kumkabili Bakhresa. Sote tuna kumbuka treni la Mwakyembe lilivyoanza kuletewa mizengwe na wakubwa hawa wanaomiliki madaladala kabla ya umma kuingilia kwa nguvu kupinga hujuma zozote.
View detail

Mandela aruhusiwa kwenda nyumbani

Nelson Mandela

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela, ameruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali moja mjini Pretoria.
Ikulu ya rais nchini humo imesema rais huyo wa zamani wa Afrika kusini, anaendelea kupata nafuu nyumbani mwake.
Msemaji wa serikali amesema Mandela bado hajapoa kabisa na ataendelea kupokea matibabu nyumbani mwake mjini Johannesburg.
Mandela alilazwa hospitaini siku kumi na nane zilizopita kufuatia maambukizi ya mapafu
Mkewe Graca Machel, na rais Jacob Zuma walimtembelea Bwana Mandela siku ya Krismasi na walisema kuwa alikuwa katika hali nzuri.
Baada ya ziara hiyo, rais Zuma alisema kuwa madaktari wamefurahishwa na jinsi Bwana Mandela alivyokuwa akiendelea kupona kwa hara licha ya umri wake.
Rais Zuma aliwashukuru raia wa nchi hiyo kwa risala zao za heri njema kwa rais huyo wa zamani.
Hata hivyo aliomba raia na waandishi wa haabri kuwa na subira na wakati huo huo kuwapa bwana mandela na familia yake nafasi wanayohitaji.
Hi ni mara ya kwanza tangu mwaka wa 1990 ambapo rais Mandela amelazwa hospitalini kwa muda mrefu zaidi.
Mjuu wa Bwana Mandela, Mandla, amesema, kutokuwepo kwa babu yao wakati wa Krismasi kumewasikitisha sana kwa sababu hawakudhani kuwa angesalia hospitalini kwa muda huo wote. View detail

Rais Zuma matatani kuhusu madai ya Mbwa


Rais Jacob Zuma
Rais JJacob Zuma akicheza dansi

Serikali ya Afrika Kusini, imeelezea matamshi yaliyotolewa na rais wa nchi hiyo, ambayo yamewakasirisha watu wanaopenda mbwa.
Rais Zuma, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema umiliki wa mbwa ni itikadi za wazungu na sio mila na desturi ya waafrika.
Lakini msemaji wa rais huyo amesema, rais Zuma, alikuwa akionya watu kutowashughulikia zaidi wanyama kuluko binadamu wenzao na hakupendekeza au uashiria mbwa kutupwa.
Amesema ujumbe huo ulikuwa na ni\ ya kuhimiza raia kuimarisha utamdani wa kiafrika na kuondoa imani na fikra za kikoloni.
Gazeti la Mercury nchini humo limeripoti kuwa rais Zuma, aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara katika mkoa wa KwaZulu Natal kuwa watu wanaotumia pesa kununu mbwa, kuwapeleka hospitalini na kutembea nao, ni watu wanaoiga na kufuata maadili ya wazungu.
Gazeti hilo liliendelea kunadi kuwa rais Zuma alisema kuwa vijana wa taifa hilo wanajaribu kuiga mfumo wa maisha wa makabila mengine yasiyo ya Kiafrika.
'' Hata ukipata nywele zako mafuta ya aina gani, huwezi kuwa mzungu'' Gazeti hilo lilimnukuu rais Zuma.
Matamshi yake yamewagadhabisha watu wengi nchini humo ambao wamechapisha hisia zao katika ukarasa mbali mbali za mitandao ya kijamii.
Wanaharakati wanaotetea maslahi ya wanyama wameshutumu kwa kutoa matamshi ambayo hayapaswi kutolewa na kiongozi wa nchi huku wengine wametuhumu na ubaguzi wa rangi.
View detail

MAGAZETI YA LEO

Thursday, December 27, 2012

MAANDAMANO YA KUPINGA GESI KUSAFIRISHWA KUTOKA MTWARA KUPELEKWA DAR BILA MASLAHI YA WANANCHI WA KUSINI KWANZA

Kutokana na maandalizi yanayofanywa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wa kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara kuelekea Dar,  Vikwazo vimeanza kujitokeza baada ya wananchi wa mikoa ya kusini kugoma kuondolewa kwa gesi hiyo mpaka wajue maslahi ya watu wa kusini. Kauli mbiu ya maandamano hayo ni Ges kwanza Vyama baadae. kwa habari zaidi usikose kutembelea blog hii!!!
Picha za matukio mbalimbali ktk maandamano hayo Mtwara
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop