Wednesday, May 8, 2013

Kustaafu kwa Alex Ferguson Hadharani


Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Premier League ,Manchester United, wametangaza kwamba, Sir Alex Ferguson atastaafu kama meneja wa klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Sir Alex anatajwa kuwa ndiye meneja mwenye mafanikio makubwa katika historia ya soka la Uingereza.
Tangu alipojiunga na klabu hiyo mnamo mwaka 1986, ameshinda mataji mawili ya Klabu Bingwa Barani Ulaya, mataji kumi na tatu ya Ligi Kuu na Kombe la FA mara tano.
Katika taarifa yake, Sir Alex amesema ni muda muafaka kwake kustaafu wakati klabu ikiwa imejizatiti katika nafasi nzuri. Atabakia Manchester United kama mmoja wa wakurugenzi na balozi.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About