Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akizungumza katika kilele cha Siku ya Viwanda Afrika
katika ukumbi wa PTA sabasaba wakati wa kufunga maonyesho hayo ya siku
ya viwanda katika bara la Afrika.
WAZIRI
wa Viwanda, Biashara na Masoko Dakta Abdallah Kigoda amesema kwamba
changamoto zilizopo nchini katika sekta ya viwanda kimfumo na
zinahitajika kuzipunguza ili kusukuma maendeleo ya kiviwanda nchini.
Akizumgumza
katika kilele cha Siku ya Viwanda Afrika, Waziri Dakta Kigoda amesema
kwa sasa serikali inatatumia rasilimali fedha za ndani katika kuimarisha
ukuaji wa viwanda katika kupambana na tatizo la ajira nchini.
WAZIRI
wa Viwanda, Biashara na Masoko Dakta Abdallah Kigoda akizungumza kwenye
kilele cha maadhimisho ya siku ya viwanda Afrika jijini Dar.
“Ni
dhahiri kuwa, tangu mwaka 1989 pale Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa
ulipoazimia kuwa Novemba 20 ya kila mwaka kuwa siku ya viwanda Afrika,
imekuwa siku mahsusi kwa wadau kujadili changamoto katika sekta hii
muhimu kwa ukuaji wa uchumi,” amesema Kigoda.
Amesema
matatizo ya kimfumo ni pamoja na mazingira ya kufanyia biashara,
utaratibu wa kuanzisha biashara na uwekezaji na utaratibu wa upatikanaji
wa vibali vya ujenzi na utaratibu wa kupata mkopo katika taasisi za
fedha.
Dakta
kigoda amesema kwamba Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zinazoendelea
bado sekta ya viwanda haijaweza kukua kwa kasi ipasavyo ukilinganisha na
baadhi ya nchi zinazoendelea barani Afrika.
Amesema
Mfano mchache wa mchango wa sekta ya viwanda ni asilimia 40 China,
asilimia 16 nchini India, Vietnam asilimia 20 na Tanzania ni asilimia
8.5 tu mpaka sasa.
Kwa
upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya
Viwanda (UNIDO) Emmanuel Kalenzi amesema ujasiriamali, ajira na
maendeleo ya kiviwanda ni jibu pekee katika matatizo ya kijamii na
kiuchumi katika bara la Afrika.
Amesema
kuwa pamoja na kuhamasisha mambo ya ajira na ujasiriamali katika bara
la Afrika lakini bado bara la Afrika lina nafasi ya kusonga mbele na
kukuza uchumi wake kwa kujikita zaidi kwenye teknolojia na uwekezaji
wenye tija.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Emmanuel
Kalenzi akizungumza katika Siku ya Viwanda Afrika.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara , Dr
Abdallah Kigoda wakati alipofunga maadhimisho ya siku ya Viwanda
Afrika kwenye uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya
Kilwa jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Viwanda Afrika jijini Dar.
Meza kuu.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu viatu kutoka kwa
Elizabeth George (kulia)wakati alipotembelea banda la Woiso Original
Products katika maonyesho yaliyoambatana na maadhimisho ya siku ya
Viwanda Afrika yaliyofaungwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa maonyesho
ya biashara ya kimataifa ya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini
Dar es salaam . Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashar, Dr.
Abdallah Kigoda na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Bw. Gerge Buchafu wa
Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) baada ya kufunga
maadhimisho ya siku ya viwanda Afrika kwenye uwanja wa Maonyesho wa
Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Novemba 20,
2013. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dr. Abdallah Kigoda.
0 comments:
Post a Comment