Wednesday, November 27, 2013

WALIMU WAGEUZA SHULE UKUMBI WA MASUMBWI


SAMSUNG CAMERA PICTURES
Afisa Elimu msingi wilaya ya  Sengerema Bw,Juma Mwajombe ilipokuwa akimvua madaraka Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Luhama kwa kosa la kutotimiza majukumu yake.

AFISA Elimu wa Shule za Msingi Sengerema Mkoani Mwanza, Bw Juma Mwajombe amemvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Luhama iliyoko kata ya Katwe kwa kushidwa kutekeleza majukumu yake.

Amesema kuwa amefikia maamuzi hayo kutokana na mwalimu huyo kushindwa kusimamia vema majukumu yake na kutokusimamia maadili ya walimu wake wanapokuwa kazini.
Bw, Mwajombe amemtaja aliy mvua madaraka hayo kuwa ni Mwalimu  Maila Majula baada ya kuchochea ugomvi kati ya mwalimu Emanuel  Joely  na Mwalimu Alfonsia Ndalahwa uliosababisha walimu hao kutwangana makonde ofisini  kwa kile kinachodaiwa kuwa walituhumiana kula fedha za ujenzi wa kisima cha shule hiyo.

Aidha amesema kuwa Mwalimu Mkuu anapaswa kusimamia vema majukumu yake na kushauri walimu kuacha migogoro isiyo ya lazima na kuzingatia maadili ya kazi na siyo kukuza migogoro isiyo ya lazima na kusababisha walimu kutokuheshimiana sehemu za kazi.
Ameongeza kuwa baada  ya  kuona mapungufu hayo ameamua kumvua madaraka hayo na kuwa mwalimu wa kawaida na kumteua Mwalimu Pema Nteba aliyekuwa mwalimu mkuu msaidizi katika shule ya msingi Mwangika ilyoko katani humo kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo,
Wakati huo huo alimuhamisha Mwalimu Alfonsia Ndalahwa katika shule hiyo na kumpeka shule ya msingi mwangika .Pia ametoa onyo kwa walimu kuacha tabia ya kutokuheshimiana kazini badala yake wafuate  maadili  ya kazi yao.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About