Welcome to our online store Portal

Template Information

Sunday, March 31, 2013

UHURU KENYATTA ATHIBITISHWA NDIO RAIS HALALI WA KENYA



Willy Mutunga rais wa mahakama ya juu zaidi Kenya


Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya, imeamua kuwa rais mteule Uhuru Kenyatta atasalia kuwa rais mpya wa Kenya baada ya kusema kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia huru na ya haki.
Uchaguzi wenyewe ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ambapo hesabu ya kura ilimpa ushindi Kenyatta kwa zaidi ya laki nane.
Rais wa mahakama hiyo jaji mkuu Willy Mutunga alisema kuwa mahakama imekubali kwa kauli moja kuwa uchaguzi ulifanywa kwa njia ya huru na wazi na kuwa Kenyatta na mgombea mwenza wake walichaguliwa kihalali.
Uamuzi huu una maana kuwa Uhuru Kenyatta ndiye ataapishwa kama rais mpya wa Kenya tarehe tisa mwezi ujao
Kesi hiyo iliwasilishwa katika mahakama ya juu zaidi na mpinzani mkuu wa Kenyatta, Raila Odinga baada ya uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.
Matokeo rasmi yalionyesha kuwa Uhuru alishinda uchaguzi kwa kumpiku Raila kwa asilimia 50.07 huku Raila akipata asilimia 43.28. Matokeo haya yalizuia kufanyika kwa duuru ya pili ya uchaguzi kwa kura 8,100.

Bwana Odinga aliishutumu tume huru ya uchaguzi na mipaka kwa kuhujumu matokeo ya uchaguzi ili kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.
Uchaguzi wa urais, wabunge na wajumbe wengine wa serikali, ulifanyika tarehe nne mwezi Machi, ukiwa wa kwanza tangu uchaguzi uliokumbwa na ghasia mwaka 2007 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya elfu moja.
Bwana Kenyatta na mgombea mwenza wake ,William Ruto,wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya jinai kwa kuchochea ghasia za mwaka 2007. Hata hivyo wamekanusha vikali mashtaka.
Mahakama ya juu zaidi inaweza kuthibitisha ushindi wa Kenyatta au kuubatilisha uamuzi wa wakenya na hivyo kuitisha uchaguzi mpya.

Vyovyote matokeo yatakavyokuwa kuna wale watakaoghadhabika mno.
Rais anayeondoka mamlakani, Mwai Kibaki amewataka wakenya kuwa watulivu na kukubali uamuzi wa mahakama lakini wengi wanatagemea sana idara ya mahakama ambayo imekuwa na mageuzi makubwa na ambayo sasa watu watu imani nayo.
Mawakili wa Odinga wanasema kuwa kesi yao ilihusisha madai ya kuhujumu hesabu ya kura pamoja na matatizo ya usajili wa wapiga kura na vile vile matatizo ya mitambo ya usajili wa wapiga kura.
Mnamo Ijumaa mahakama ya juu zaidi ilidurusu matokeo ya kura katika vituo 22 vya kupigia kura. Na pande zote mbili zilisema matokeo yalithibitisha misimamo yao.
Kenyatta ameutaja uchaguzi huo kama ishara ya kukuwa kwa demokrasia Kenya na ulifanywa kwa njia ya amani.

Tume ya uchaguzi, pia imesisitiza kuwa uchaguzi ulikuwa huru licha ya hitilafu za kimitambo
Wachunguzi wa kimataifa nao walisema kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na kuwa tume huru ya uchaguzi uliendesha uchaguzi huo kwa uwazi.
View detail

Thursday, March 28, 2013

Balozi mpya wa UAE Mhe.Abdulla Ibrahim Al Sowaidi awasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Kikwete leo


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Muungano wa Falme za Kiarabu UAE,Mhe.Abdulla Ibrahim Al Sowaidi ikulu jijini Dar es Salaam leo.Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Juma Maharage View detail

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA RIPOTI YA 2011-2012 NA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Bwana Ludovick Utouh akikabidhi Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2011-2012 kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam leo. View detail

Wednesday, March 27, 2013

Makundi yawadhulumu wakimbizi Somalia

Wanwake wengi wamelalamika sana wakisema wanabakwa na watu waliovalia magwanda ya jeshi

Shirika la kutetea haki za kibinadamu, Human Rights Watch, limesema kuwa makundi yaliyojihami nchini Somalia ikiwemo majeshi ya serikali, yamefanya vitendo vya ubakaji, kuwachapa na kuwadhulumu watu walioachwa bila makao au wakimbizi.
Ripoti ya shirika hilo imegusia wale watu waliokimbia vita tangu mwaka 2011 kwa sababu ya njaa, na sasa wanaishi katika kambi mjini Mogadishu.
Katika ripoti hiyo mpya, shirika hilo limesema kuwa wasimamizi wa kambi hizo , wanaojulikana kama walinzi, huiba msaada wa wakimbizi hao na hata kuwadhulumu.
Shirika hilo linasema , kuwa wakimbizi wa ndani, hasa wanawake wameripoti kubakwa na kudhulumiwa na watu waliovalia sare za kijeshi na wengine wanaoaminiwa kuwa wapiganaji wa makundi ya waasi.
Linasema kuwa baadhi ya vitendo vibaya vya dhuluma walivyofanyiwa ni pamoja na dhulma za kingono dhidi ya wanawake na wasichana.
Kadhalika ripoti hiyo imewanukuu wanawake wanaodai kubakwa akiwemo mwanamke mwenye umri wa miaka 23 aitwaye, Quman.
Anasema alikuwa na ujauzito wa miezi, tisa alipobakwa na kundi la watu asiowajua ingawa walikuwa wamevalia magwanda ya kijeshi.
Mwanamke mwingine, Safiyo, alilazimika kukatwa mguu wake baada ya kubakwa na kisha kupigwa risasi.
Aidha ripoti hiyo inasema kuwa visa vya ubakaji haviripotiwi sana kwa sababu ya hofu ya wanawake kuwa watafanyiwa unyanyapaa na kutengwa na jamii.

''Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa watu katika kambi hizo huwekwa kama watumwa. Hawawezi kuondoka, walinzi wa kambi hizo wenyewe wanafanya dhulma. Wao huiba msaada ambao hutolewa kwa wakimbizi. Watu wengi kwa sasa wanahitaji msaada wa haraka,'' ilinukuu ripoti hiyo.
Human Rights Watch pia limefichua visa vya ubaguzi wa kikabila hasaa kwa wale wanaotoka katika jamii fulani. Linasema kuwa watu wengi wamelalamika kuhusu visa vya kukamatwa kiholela na hata kudhulumiwa. Licha ya serikali ya mpya ya Somalia kupiga hatua bado inakabiliwa na changamoto nyingi.
View detail

Tuesday, March 26, 2013

MUONEKANO WA KIWANDA CHA CEMENT CHA LINDI UTAKAVYOKUA

Hivi ndivyo Kiwanda cha Cement cha Lindi kitakavyokua. Wanalindi watarajia mafanikio makubwa baada ya kiwanda hiki kumalizika na kukidhi matarajio ya wana Lindi. Lengo la wanalindi laweza kua limefikiwa au laa kwa wakazi walindi kusomesha watoto wao na kukabiliana na fursa  zilizopo na kuhakikisha wananufaika na kiwanda hiki kwa kila fursa!! View detail

M-PESA SASA YAPANUA HUDUMA ZAKE KWA KUWAWEZESHA WAJEJA WAKE KUTUMIA ATM ZA DTB KUTOLEA FEDHA



Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati,(kushoto)akiwaelezea waandishi wa habari,jinsi ya kutoa fedha kwenye mashine za kutolea fedha za DTB kupitia huduma ya Vodacom M PESA ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote walipo nchini,huduma hiyo imezinduliwa leo jijini Dares Salaam pamoja nae ni Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim.
 
Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim,akitoa fedha kwa mara ya kwanza baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya kutoa fedha kupia mashine za kutoa fedha za DTB kupitia huduma ya M PESA, ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote zilipo nchini anaeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati.
 
Meneja mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim,pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati.wakifurahia mara baada ya kutoa fedha kwa mara ya kwanza kupitia mashine za kutoa fedha za DTB kwa huduma ya M PESA, ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote zilipo nchini.

Ukuaji wa teknolojia ya huduma maarufu ya kutuma, kupokea fedha pamoja na kufanya malipo ya huduma mbalimbali kwa njia ya simu za mkononi ya kampuni ya Vodacom ya M-pesa inazidi kupanuka na hivyo kuongeza kiwango cha matumizi ya huduma hiyo kuzidi kuboresha maisha na kuyafanya kuwa rahisi zaidi.

Katika kufikia mafanikio hayo Benki ya Diamond Trust (DTB) leo imetangaza ubia wa kibiashara na kampuni ya Vodacom Tanzania ubia ambao unawawezesha wateja wa M-pesa kuwa na uwezo wa kutoa fedha kutoka katika akuanti za M-pesa kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM) za benki ya Diamond Trust.

Wakitangaza na kuzindua huduma hiyo jijini Dar es salaam Mkuu wa Kitengo za Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati, amesema hayo ni mafanikio mengine ya kibishara kwa benki hiyo ya DTB katika kupanua wigo wa huduma na namna benki hiyo inavyoweza kuunganisha teknolojia ili kuleta urahisi kwa watanzania.

"DTB inayo Furaha kubwa kuwa sehemu ya mapinduzi ya kiteknolojia hapa nchini. Hii ni huduma ya kwanza na ya aina yake ambayo hakuna shaka kwamba inaashiria uwezo wa DTB katika kuleta ufumbuzi wa namna bora ya kutumia teknolojia kurahisisha maisha."Amesema Bahati

"Tukishirikiana na Vodacom tunawawezesha wateja wa M-pesa walio karibu na benki zetu na hususan mtandao wa ATM kuwa na uhakika wa kutoa fedha kutoka akaunti zao za M-pesa saa ishirini na nne katika siku zote saba za wiki."

Bahati amesema jambo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na uchumi kwa watanzania wote mijini na vijijini.

Hata hivyo hii ni frusa ya kipekee kwa wateja wa benki ya DTB ambao wamejiandikisha kwa ajili ya huduma ya M-Pesa hawana haja tena ya kutembelea matawi ya benki hiyo ili kuweza kuweka amana zao au kuhamisha fedha kwa biashara, marafiki na familia zao. Pia uzinduzi wa huduma hiyo utawezesha kujenga urahisi wa kuruhusu wasiotumia huduma ya benki kupata huduma za kifedha karibu nao.

Azma ya DTB ni kuzidi kuongeza kasi na maboresho ya utoaji wa huduma kwa wateja wake na washirika wake wengine kwa kuhakikisha inaendelea kupanua wigo wa huduma zake ikiwemo kuongeza ATMs, matawi na huduma nyinginezo kwa lengo la kusogeza karibu huduma za kibenki nchi nzima.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa M- Biashara wa Vodacom Jacques Voogt, amesema, "Hii ni hatua nyingine ambayo tunaifikia leo. Kampuni ya Vodacom inaendelea kupanua mtandao wake wa huduma ya M-Pesa." Voogtz ameongeza kuwa ubia huo ni mwendelezo wa azma ya kampuni ya Vodacom kutumia fursa za teknolojia ya M-pesa kuzidi kuleta amsiha ya watu mikononi mwao kutumia simu za kiganjani.

"Wateja wa Vodacom M-pesa wanayo sababu nyingine ya kujivunia kuwa sehemu ya mtandao mpana wa huduma hii salama, rahisi na yenye kuaminika zaidi nchini wakiunganishwa na makampuni na hata tasisi zaidi ya 200 kufanya malipo ya huduma na manunuzi kwa urahisi na wepesi zaidi kupitia simu za viganjani."Aliongeza Voogtz
View detail

Thursday, March 21, 2013

Rais Obama atua nchini Israel

Rais Obama
Rais Obama

Rais Barack Obama amewasili nchini Israel. Hii ni ziara yake ya kwanza kama rais wa Marekani.
Huku akiwasili, waandamanaji walikusanyika na ulinzi kuimarishwa nchini Israel na katika maeneo ya Palestina.
Bwana Obama anategemewa kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na rais wa Palestina Mahmoud Abbas wakati wa ziara yake ya siku tatu.
Vita nchini Syria na wasiwasi kuhusu nia za Iran za kinyuklia ni kati ya maswala muhimu, wanasema waandishi habari.
View detail

Home shopping centre yakabidhi shule mpya ya msingi mabwepande


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua shule mpya ya msingi ya Mabwepande jijini Dar es salaam leo iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Home Shopping Cenrre
 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni kabla ya kuzindua shule mpya ya msingi ya Mabwepande jijini Dar es salaam leo iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Home Shopping Cenrre
 
 Rais Kikwete akimsikiliza Mkurugenzi wa Home Shopping Centre wakati akikabidhi shule hiyo
 
Rais Kikwete akimshukuru Mkurugenzi wa Home Shopping Centre kwa kujenga shule ya msingi Mabwepande yenye majengo na samani za kisasa. View detail

Wednesday, March 20, 2013

UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI WAENDELEA KWA KASI NA KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA KUONA MAENDELEO YAKE

Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhani Dau akifafanua jambo mbele ya wajumbwe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu walipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa daraja la Kingamboni jijini Dar es Salaam leo. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau (wa pili kushoto) akiangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea mradi huo leo. Kushoto ni Mhandisi wa NSSF, John Msemwa.
 Mhandisi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), John Msemwa akitoa mada wakati Kamati ya Bunge ya miundombinu ilipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni..
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa Ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. 
 Kamati ya Bunge ya Miundombinu ikiangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
 Mafundi wakiwa kazini.
 Mafundi kazini.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Peter Selukamba (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa Ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Hapa moja ya za daraja la Kigamboni itawekwa hapa.
 Mhandisi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Karim Mattaka akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa daraja la Kigamboni. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Selukamba.
 Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu akiwa na Ofisa wa Trafic, Peter.
 Mhandisi wa NSSF, John Msemwa akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni kwa Mkufugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau (kulia)
 Zege ikimiminwa katika moja ya nguzo za daraja hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Peter Selukamba (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa UjenziGerson Lwenge wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa Ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.
View detail

DR. BILALI ATOA POLE KWA WAFIWA WA ASKARI WA USALAMA BARABARANI ALIYEGONGWA NA GARI JANA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam jana.
Picha ya Marehemu enzi za uhai wake. 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Prince David, mtoto wa aliyekuwa askari wa Usalama Barabarani, marehemu WP Elikizaeli Lokisa Nnko, aliyefariki dunia kwa kugongwa na gari na dereva ambaye hadi sasa hajajulikana wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi eneo la Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam jana. 
 
Kutoka (kulia) ni Mume wa Marehemu, David Erasto Luharara, watoto wa marehem, Prince David na Abdulhaman David, wakiwa na huzuni.
 
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu kuomboleza msiba huo.
View detail

Monday, March 18, 2013

NTAGANDA AJISALIMISHA KWA UBALOZI WA MAREKANI



Ntaganda ajisalimisha

Hatimae Marekani imethibitisha kuwa Muasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jenerali Bosco Ntaganda, amejisalimisha katika ubalozi wake mjini Kigali, Rwanda.
Taarifa hiyo ya Marekani inasema kuwa Ntaganda ameomba ahamishwe hadi katika Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa ICC huko the Hague.
Ntaganda aliyeanzisha maasi nchini Congo ameshitakiwa katika mahakama hiyo ya ICC na anakabiliwa na mashitaka ya kuwajumuisha watoto katika jeshi, mauaji na ubakaji.
Jenerali Ntaganda mwenyewe anakanusha madai hayo yote.
Marekani imesema kwa wakati huu inashauriana na serikali kadhaa ili kufanikisha ombo hilo la Jenerali Ntaganda ahamishwe hadi mahakama ya ICC.
Awali Serikali ya Rwanda ilikuwa imetangaza kuwa Jenerali huyo muasi anayetuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amejisalimisha katika ubalozi wa Marekani mjini Kigali, Rwanda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema taarifa walizonazo ni kuwa Kiongozi huyo muasi yuko chini ya ulinzi wa Marekani katika ubalozi wake.
"Tumefahamishwa hii leo (Jumatatu) kuwa Bosco Ntaganda ameingia Rwanda na kujisalimisha katika Ubalozi wa marekani hapa Kigali", amesema Louise Mushikiwabo
Jenerali Ntaganda amekanusha mashitaka yanayomkabili katika mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai ICC kwamba anahusika na uhalifu wa kivita na ule dhidi ya binadamu.
View detail

Saturday, March 16, 2013

UN - HAKI ZA WANAWAKE ZAPOTEA


 
haki za wanawake katika UN


Zaidi ya mashirika 12 ya kutetea haki za binadamu na haki za wanawake kutoka mataifa ya kiarabu yameonya kuwa azimio la UN la kukabili unyanyasaji wa wanawake linatishiwa na upinzani kutoka kwa chama cha Muslim Brotherhood kutoka Misri, uongozi wa Vatican na Urusi.
Azimio hilo liko katika hatua za mwisho za mashauriano kabla ya kuidhinishwa na tume ya kutetea maslahi ya wanawake katika Umoja huo.
Muslim Brtoher hood imesema kuwa azimio hilo linatishia kuvuruga mpangilio katika jamii kwa kuwapa wanawake ruhusa ya kusafiri, kufanya kazi au hata kupanga uzazi bila idhini ya waume wao.
Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu kutoka mataifa ya arabuni (hasa Misri, Lebanon Palestine, Jordan na Tunisia) yametoa wito kwa mataifa yaliyo na uakilishi katika tume hiyo ya UN juu ya haki za wanawake, yakome kutumia dini, utamaduni na mila kama kisingizio cha kuruhusu ukiukaji wa haki na unyanyasaji wa wanawake.
View detail

Friday, March 15, 2013

MISS TANZANIA YANZA RASMI


 Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred (katikati) akigonganisha glass na Mkurugeni wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ni Wadhamini wakuu wa Shindano la Miss Tanzania,Kushilla Thomas (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania,Anko Hashim Lundenga ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2013/14 wakati wa tafrija mchaparo a.k.a mkia wa jogoo (cocktail party),iliyofayika usiku huu kwenye Ukumbi wa Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam
 
 Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania,Anko Hashim Lundenga akizungumza machache wakati wa wakati wa tafrija mchaparo a.k.a mkia wa jogoo (cocktail party) ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2013/14,iliyofayika usiku huu kwenye Ukumbi wa Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam
 
 Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred (katikati) akiwa katika picha pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Redd's Original,Victoria Kimaro (kushoto) na Meneja wa vilaji vha Castle Lite na Ndovu,Pamella Kikuli wakati wa tafrija mchaparo a.k.a mkia wa jogoo (cocktail party) ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2013/14,iliyofayika usiku huu kwenye Ukumbi wa Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam
 
 Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigit Alfred (pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mamiss Tanzania waliopita,Toke Kushoto ni Faraja Kotta,Salha Israel pamoja na Nancy Sumary.
View detail

DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE AZINDUA JENGO LA KITIVO CHA SAYASI LA CHUO KIKUU CHA KIISLAM MOROGORO



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu mjini Morogoro leo
 
 Rais Kikwete akipeana mikono na Bw Ahmed Saggaf
 
 Rais Kikwete akitembelea moja ya vyumba vya maabara
 
 Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya ujenzi wa jengo la kitivo cha TEKNOHAMA katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu mjini Morogoro leo
 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu mjini Morogoro leo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika sherehe za uzinduzi wa jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu mjini Morogoro leo
 
 Rais Kikwete akiendelea na hotuba huku akishangiliwa.
 
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro Mama Mwantumu Malale akiongea machache na kumkaribisha Rais Kikwete.
 Makamu Mkuu wa Chuo Profesa Hamza Mustafa Njozi akisoma ripoti  ya chuo kwa Rais Kikwete.
 
Sehemu ya wanafunzi na wageni waalikwa.
 
 Sehemu ya wanafunzi.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo katika sherehe za uzinduzi wa jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Kiislamu mjini Morogoro leo.
 
 Profesa Juma Mikidadi Mtupa akikaribishwa kupata picha na mheshimiwa
 
 Picha na wahadhiri
 
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop