Welcome to our online store Portal

Template Information

Monday, September 30, 2013

WAJUA FUKUTO KUHUSU RASIMU YA KATIBA?

SURA YA KWANZA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
SEHEMU YA KWANZA
MIPAKA, ALAMA, LUGHA, UTAMADUNI NA TUNU ZA TAIFA
Jamhuri ya
Muungano 1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.

(2) Jamhuri ya Muungano ni Shirikisho la kidemokrasia
linalofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa, usawa wa binadamu,
kujitegemea, utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu.
(3) Hati ya Makubaliano ya Muungano iliyorejewa katika Ibara
ndogo ya (1), ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Katiba hii, kwa kadri itakavyorekebishwa, itakuwa ni mwendelezo wa Makubaliano hayo.

Eneo la Jamhuri ya Muungano
2. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara
ikijumuisha sehemu yake ya bahari na eneo lote la Zanzibar ikijumuisha
sehemu yake ya bahari.
Alama na Siku
Kuu za Taifa 3.-(1) Alama za Taifa ni:
(a) Bendera ya Taifa;
(b) Wimbo wa Taifa; na
(c) Nembo ya Taifa,

kama zitakavyoainishwa katika sheria itakayotungwa na Bunge.
(2) Siku Kuu za Kitaifa zitakuwa ni:
(a) Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9
Disemba;
(b) Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe 12
Januari;
(c) Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
itakayoadhimishwa tarehe 26 Aprili; na
(d) Siku Kuu nyingine zitakazoainishwa na sheria za nchi.
(3) Kila Siku Kuu ya Kitaifa itakuwa ni siku ya mapumziko.
Tufuatilie toleo lijalo kujua zaidi View detail

MKUU WA SHIRIKA LA KIJASUSI LA KENYA MICHAEL GICHANGI AHOJIWA LEO

Mawaziri wa serikali walipokea taarifa kuhusu tisho la mashambulizi ya kigaidi kabla ya kundi la Al Shabaab kushambulia jengo la Westgate mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa za kijasusi zilizofichuliwa, zilionyesha maelezo ya mipango ya mashambulizi hayo kufanyika Nairobi au mjini Mombasa.
Mawaziri wanne na mkuu wa majeshi walikuwa wamefahamishwa kuhusu tisho la kufanyika shambulizi la kigaidi.
Watu 67 walifariki na mamia kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi ambalo Al Shabaab walikiri kulifanya Septemba 21 mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la Daily Nation, mawaziri walipopewa taarifa za kati ta yarehe 13 na 20 kuhusu uwezekano wa kufanyika mashambulizi kadhaa ya kigaidi mjini Mombasa na Nairobi.
Onyo hizo zilitolewa kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Januari kwa mujibu wa gazeti hilo na kwa mara nyingine kuanzia Septemba.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, serikali ya Israel pia ilitoa taarifa za kuonya kuwa huenda magaidi wakashambulia majengo yanayomilikiwa na raia wake kati ya tarehe 4 na 28 Septemba.
Daily Nation limeripoti kuwa taarifa za kijasusi zilionyesha kuwa viongozi wa al-Shabab walikuwa wameanza kulenga maeneo ya kushambulia ikiwemo Westgate na kanisa la Holy Family Basilica.
Kuna hofu idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Maafisa wa serikali wanaosemekana kupokea taarifa hizo ni pamoja na waziri wa fedha, Julius Rotich, waziri wa usalama Joseph Ole Lenku, waziri wa maswala ya kigeni, Amina Mohammed, waziri wa ulinzi Raychelle Omamo na mkuu wa majeshi Julius Karangi.
Mkuu wa shirika la ujasusi Michael Gichangi, anatarajiwa kuhojiwa na kamati ya bunge kuhusu usalama siku ya Jumatatu. View detail

Friday, September 27, 2013

WAKUU WA USALAMA WA NCHI YA KENYA KIKAANGONI

Viongozi wakuu wa ujasusi nchini Kenya wametakiwa kufika mbele ya kamati ya ulinzi ya bunge ili kuhojiwa kuhusu mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jumba la Westgate mjini Nairobi.
Taarifa kwenye vyombo vya habari nchini humo zinaonyesha kuwa hali ya kulaumiana imeanza kuibuka huku mashirika ya usalama yakinyosheana kidole.
Watu 67 waliuawa kwenye shambulizi hilo huku zaidi ya miamoja sabini na tano wakipata majeraha mabaya. Shirika la Red Cross nalo linasema kuwa watu 61 wangali hawajulikani waliko.
Wataalamu wa uchunguzi wa mauaji wangali wanafanya uchunguzi wao wakitafuta miili na dalili za kilichosababisha shambulizi hilo.
Kamati ya bunge inataka maafisa wanaohusika na maswala ya usalama waweze kuwajibishwa.
Kundi la kigaidi la nchini Somalia, al-Shabab limedai kufanya mashambulizi hayo yaliyodumu siku nne kama hatua ya kulipiza kisasi kwa Kenya kujihusisha nchini Somalia kijeshi.
Hii leo ni siku ya tatu ya maombolezi kwa wathiriwa wa shambulizi hilo wakiwemo raia na wanajeshi.
Rais Uhuru Kenyatta amehudhuria mazishi ya mpwa wake na mchumba wake mjini Nairobi ambapo aliwahutubia waumini.

Hatua ya kuwataka maafisa hao wa usalama kufika mbele ya tume ya bunge siku ya Jumatatu, inakuja kutokana na wasiwasi miongoni mwa wakenya kuhusu kiwango cha maafisa hao kujiandaa kwa tukio lolote la kigaidi sawa na lililotokea Westgate.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mmoja wa maafisa waliotakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ni mkuu wa shirika la ujasusi Michael Gichangi, anayesema alitoa taarifa za ujasusi kuhusu shambulizi hilo kwa polisi.
Lakini, afisaa mmoja mkuu katika idara ya polisi alikana kuwa taarifa hiyo ilitolewa kwa polisi.
View detail

Thursday, September 26, 2013

KENYA YAPATA PIGO JINGINE

Magaidi Tena Kenya, walipua kituo cha polisi, waua watu watatu, magari 11 yachomwa
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa watu wanaozaniwa kuwa ni magaidi wamevamia kituo cha
Polisi katika Mji wa Mandera nchini Kenya na kuwaua polisi wawili, watatu wamejeruhiwa vibaya na baadaye kuchoma magari zaid ya 11.Tufuatilie tuzidi kukuhabarisha View detail

Wednesday, September 25, 2013

MWANAMKE ABAKWA MALI NA WANAJESHI WA UN

Kikosi cha wanajeshi cha Minusma nchini Mali kiko chini ya UN
Umoja wa Mataifa unasema kuwa wanajeshi wake wanne wa amani nchini Mali walihusika na kitendo cha kumbaka mwanamke mmoja wiki jana.
Wanajeshi hao ni sehemu ya wanajeshi 1500 wa Umoja wa Mataifa kutoka Chad ambao wanafanya kazi chini ya kikosi cha Minusma. Umoja wa Mataifa unataka serikali ya Chad kuchunguza madai hayo ili kuwachukulia hatua za kinidhamu watakaopatikana na hatia.
Inasemekana mwanamke aliyebakwa alikuwa amekuja kutafuta msaada wa kimatibabu kutoka kwa Umoja wa Mataifa punde baada ya kubakwa Alhamisi wiki jana mjini Gao.
Madai ya mwanamke huyo yalisababisha hatua za haraka za kuchunguza washukiwa.
Haijulikani idadi ya wanajeshi wa Chad waliohusika na shambulizi hilo, lakini mwathiriwa aliweza kuwatambua wanajeshi wanne kuwa miongoni mwa wale waliombaka katika chumba kilichokuwa karibu na baa.
Wakati wa tukio hilo, wanajeshi miamoja na sitini na tano, walikuwa wakishika doria mjini Gao.
Walikiuka amri ya wakuu wao ya kutoondoka kambini katika eneo la Tessalit, Kaskazini mwa nchi, kufuatia tofauti zilizoibuka kuhusu mazingira katika kambi hiyo.
Msemaji wa Minusma mjini Bamako alisema kuwa ilikuwa juu ya jeshi la Chad kuamua adhabu watakayopewa wanajeshi hao,
Alisema kuwa mwathiriwa atapokea matibabu na ushauri nasaha pamoja na msaada wa kisheria lakini sio msaada wa kifedha.
View detail

WESTIGATE YAOKOLEWA LAKINI HAKUNA AL SHABAB ALIYEKUTWA NDANI YA JENGO

Hiki ni kitendawili kisicho na jibu, jeshi limepigana na al shabab mpaka dakika ya mwisho, wanaingia ndani ya jengo hakuna mtuhumiwa wa tukio, baadae yaonekana wamekamatwa wakijaribu kuondoka nchini, wametokaje ktk lile jengo? Watu wa jeshi walikua wapi wakati watu hawa wakitoka? Hii ni changamoto kubwa kwa nchi za Afrika kuhusu usalama wetu.

Kenya inaanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kwa waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi.
Rais Uhuru Kenyatta pia ameseama kuwa bendera zitapepershwa nusu mlingoti kwa heshima ya waliopoteza maisha yao katika mashambulizi hayo.
Watu 67 wameuawa ikiwemo wanajeshi kadhaa wa usalama, ingawa kuna hofu kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Maafisa wa uchunguzi wa kimataifa wanaungana na wale wa Kenya kujaribu kuondoa mili ambayo imenaswa kwenye vifusi vya jengo hilo ambalo sehemu yake iliporomoka jana. Nia ni kujaribu pia kutambua uraia wa washambulizi hao.
Baraza la usalama wa kitaifa linatarajiwa kukutana leo kudadisi yaliyotokea na kujiandaa kwa mkakati mpya wa kigaidi.

Magaidi watatu wa kundi la Al Shabab lililokiri kutekeleza mashambulizi hayo,waliuawa katika shambulizi hilo lililodumu siku nne na kuwa washukiwa wengine 11 walikamatwa wakijaribu kuondoka nchini.
Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumatano , Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa alihisi uchungu mkubwa na kuwa Kenya imejeruhiwa vibaya,lakini alielezea matumaini kwa kuwa shambulizi limeisha na kusema kwamba waliohusika watakiona cha mtemakuni.
Wakati huohuo, afisaa mmoja mkuu wa serikali ya Somalia, amesema kuwa hakuna suluhu la kijeshi kwa kundi la wanamgambo wa Al Shabaab nchini humo. Wanamgambo hao wameitikia kuhusika na mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya ambao watu zaidi ya sitini wameuawa.
Akizungumza na mjumbe wa nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa, Yusuf Mohamed Ismail Bari Bari, alisema kuwa serikali yake na jamii ya kimataifa inapaswa, kuangazia zaidi mizizi ya tatizo la magaidi hao, upatikanaji wa rasilimali pamoja na uwakilishi wa kisiasa.
View detail

Tuesday, September 24, 2013

KENYA BADO HALI SI SHWARI


Vikosi vya usalama nchini Kenya vinasema viko katika mkondo wa lala salama katika kuweza kudhibiti jengo zima la Westgate. Hadi sasa serikali inasema kuwa mateka wote wameokolewa huku wanamgambo sita waliosalia wakiuawa usiku wa kuamkia leo.

 
Polisi wakikabiliana na wanamgambo hao waliokuwa wameteka jengo la Westgate
Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa usalama idadi kamili ya magaidi waliouawa ni tisa
Duru kutoka shirika la AFP zinasema kuwa majeshi ya Kenya yangali yanakabiliana na gaidi mmoja au wawili ambao wamesalia ndani ya jengo la Westgate.
Inaarifiwa magaidi hao walijitawanya wakiwa ndani ya jengo hilo kila mmoja akijificha sehemu yake katika ghorofa ya juu zaidi ya jengo hilo.
Milio ya risasi na milipuko ilisikika mapema leo asubuhi kutoka katika jengo hilo.
Ukabilianaji huo ulitokea baada ya serikali ya Kenya kutangaza kudhibiti jengo hilo zima huku hali hiyo ikishuhudiwa kwa siku ya nne.
Serikali ilisema kuwa mateka wote wameokolewa ingawa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu hali ilivyo sasa.





View detail

Monday, September 23, 2013

KENYA HALI YAZIDI KUA TETE (Westgate)

Jeshi la Kenya linasema kuwa limedhibiti jengo hilo ingawa hali bado ni mbaya
Milio mikubwa ya risasi na milipuko imesikika huku juhudi za usalama zikiendelea katika jengo la Westgate ambako wanamgmbo wa Al shabaab wameteka jengo hilo pamoja na wakenya wachache ambao wangali kuokolewa.
Kwa mujibu wa waziri wa usalama Joseph Ole Lenku, vikosi vya usalama vimeweza kudhibiti jengo hilo nje na ndani na kwamba ni mateka wachache waliosalia katika jengo hilo.
Serikali inasema watu 62 wameuawa lakini shirika la Red Cross lilisema kuwa idadi hiyo ni 69.
Westgate ni jumba la kifahari lenye maduka na mikahawa karibia themanini .
Milio hiyo ilidumu kwa dakika tatu na kufuatiwa na moshi mkubwa juu ya jengo hilo. Hakuna taarifa kamili kuhusu kilichosababisha moshi huo.
Sehemu ya jengo la Westgate ikitoa moshi
Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani. Walikuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.
Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.
Aidha wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wangali ndani ya jengo hilo.
Ripoti zinasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa risasi pamoja na milipuko imesikika katika jengo hilo kwa takriban dakika 15.
Harakati za kuendelea kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora.
Rais Kenyatta amesema kuwa jeshi linajitahidi kuhakikisha kuwa linakabiliana vilivyo na wanamgambo hao.
Wakenya waliofanikiwa kuondoka katika jengo la Westgate kwa usaidizi wa polisi
Helikopta za polisi zinazunguka juu ya jengo hilo pamoja na ndege za kijeshi kushika doria. Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni kujaribu kuwanusuru waathiriwa wakati hali ikiwa ni ya ati ati katika eneo la shambulizi.
Awali jeshi la Kenya lilisema limeweza kudhibiti jengo hilo lote ingawa bado limetaja hali kuwa tete mno hasa katika kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya jengo hilo.
Ripoti zinasema kuwa watu 69 wamefariki katika shambulizi hilo la Al Shabaab kufikia sasa huku 175 wakijeruhiwa. Baadhi wametibiwa na kuondoka hospitalini. Baadhi ya majeraha waliyopata ni majereha ya risasi na kutokana na guruneti ambalo Al shabaab waliwarushia wale waliokuwa ndani ya mikahawa siku ya Jumamosi.
Kundi hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo kutokana na hatua ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini Somalia ili kukabiliana na wapiganaji hao.
View detail

YANGA YAZIDI KUDONDOKA KILELENI


Vinara Simba wanaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 11 na mabao yao 13 ya kufunga na kufungwa magoli manne, huku JKT Ruvu ikifuatia ikiwa na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa ikiizidi Azam licha ya kulingana nao pointi 9 sawa na Ruvu Shooting na Coastal Union.
Azam yenyewe imefunga mabao nane na kuruhusu mabao matano, wakati JKT Ruvu imefunga mabao sita na kufungwa mawili na kuwa, ikifuatiwa na ndugu zao Ruvu Shooting waliofunga mabao sita na kufungwa matatu kisha Coastal iliyofunga magoli matano na kuruhusu nyavu zake zitikiswe mara mbili.

Kagera Sugar iliyoanza ligi kwa kusuasua ushindi wake wa jana dhidi ya Ashanti umeiweka katika nafasi ya sita ikiwa na pointi nane na kufuatiwa na Mbeya City wenye pointi saba kisha Yanga yenye pointi zake sita.
Oljoro JKT iliyokuwa nafasi ya pili toka mkiani imechupa hadi nafasi ya 11 mwa msimamo baada ya ushindi wake wa leo dhidi ya JKT Ruvu ikifikisha pointi nne na kuirithisha nafasi hiyo Prisons-Mbeya huku Ashanti wakiendelea kuzibeba timu zote 13 za ligi hiyo ikiwa na poingti moja tu.
MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA HUU HAPA


Mpaka sasa ligi ikijiandaa kuingia raundi ya sita siku ya Jumatano kwa pambano moja tu kati ya Rhino Rangers ya tabora itakayoialika Ashanti United mjini Tabora jumla ya mabao 76 yameshatinga wavuni, huku Tambwe Amissi wa Simnba akiongoza orodha ya wafungaji wenzake akiwa na mabao sita.
Tambwe anafuatiwa kwa mbali na washambuliaji nyota wa Yanga, Jerry Tegete na Didier Kavumbagu na Haruna Chanongo, mchezaji wenzake wa Simba wenye mabao matatu kila mmoja.

View detail

Saturday, September 21, 2013

AGNESS MASOGANGE APIGWA FAINI YA RANDI 30,000


Agness Gerard ‘Masogange’ na Melissa Edward wameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg baada ya kutakiwa kulipa faini ya Sh 4.8 milioni (Randi 30,000) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumiwa kutengeneza dawa za kulevya.
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini (hawk) Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya bali kemikali aina ya ephedrine.
Hata hivyo mahakama ilibaini kuwa Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana amemsindikiza Masogange, aliyemuomba amsaidie kubeba mzigo huo.
Mosagange alilipa faini ya Shilingi 2.5 milioni (R15, 000), huku akiahidi kumaliza nusu yake ambayo juhudi zilikuwa zinafanyika amalize kulipa jana Ijumaa.
“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kusaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini haikuwa mizigo yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Masogange na si Melissa,” alisema Kapteni Ramaloko.
Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimuomba amsaidie mizigo hiyo kwani ilikuwa mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela miezi 30 (miaka miwili na miezi sita) au alipe faini ya R30, 000(Sh 4.8 milioni).
Hata hivyo alilipa faini na nusu ya fedha hizo ilishalipwa na nyingine ilikuwa inakaribia kulipwa.
Ingawa Kamishana Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa juzi Alhamisi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS) Marika Muller, alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5, mwaka huu ni methamphetamine.
View detail

MULLAH AACHIWA HURU PAKISTAN

Afghanistan yafurahi Taliban afunguliwa



Wakuu wa Pakistan wanasema wamemuachilia huru mfungwa mwenye cheo katika kundi la Taliban - Mullah Abdul Ghani Baradar - ili kurahisisha juhudi za mapatano nchini Afghanistan.
Serikali ya Afghanistan imekaribisha habari hizo na inamuona Mullah Baradar kuwa mmoja kati ya maafisa waandamizi walio tayari kuzungumza.
Afisa mmoja wa Afghanistan alimuelezea Mullah Baradar - naibu kiongozi wa zamani wa Taliban - kuwa mjumbe wa amani.
Hata hivyo, waandishi wa habari wanasema haijulikani Mullah Baradar ana kauli gani bado katika kundi hilo la wapiganaji.
Alikamatwa mjini Karachi, Pakistan, mwaka wa 2010.


View detail

CCM YAMTAKA WAZIRI WA ELIMU AJIUZULU


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa kujiuzulu kwa kushindwa kulipa madeni ya walimu nchini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pia ametoa muda wa miezi sita kwa Waziri huyo na Naibu wake Philip Mulogo kutekeleza hilo agizo hilo vinginevyo chama kitawatumia wabunge wake kuwatimua kwa nguvu.

Kwa mujibu wa taarifa za madeni zilizokusanywa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), hadi sasa walimu wanadai malimbikizo yao ya Sh bilioni 49 ambayo hajalipwa na Serikali.
Kinana alikuwa akihutubia mikutano ya hadhara jana katika wilaya za Bariadi na Busega.
Alisema CCM haiko tayari kuona walimu wakinyanyaswa wakati wana madai ya msingi.
Hivi sasa imejengeka tabia kwa baadhi ya mawaziri na watendaji wa wizara ya kuwadharau walimu na hata kuwanyanyasa huku wengine wakishusha utu na heshima ya walimu kwa kuwatukana, alisema.

Kinana ambaye yupo katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa alisema kwa mawaziri kushindwa kutatua kero za walimu, imefika wakati wahusika waondoke wenyewe na wasipofanya hivyo chama kitawaagiza wabunge wake wawafukuze kwa nguvu.

“Ninatoa muda wa miezi sita kwa Waziri wa Elimu na wasaidizi wake wakiwamo watendaji kuhakikisha wanalipa madeni ya walimu haraka. Haiwezeni hii ni nchi ya watu wote wakiwamo walimu wadharauliwe na hata kunyanyaswa kwa maneno ya matusi

“Hili hapana CCM haiko tayari kuona walimu kila siku wakipigwa danadana kutokana na uzembe wa watu waliokabidhiwa dhamana za kuongoza sekta ya elimu katika nchi yetu,” alisema.
Mwandishi wetu alimtafuta Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiah Oluoch ambaye alisema hadi sasa madeni ya walimu yamefikia Sh bilioni 49 ambayo ni malimbikizo ya mishahara na mapunjo.

“Kila mara tunawaambia kuwa ni vema Serikali itafute Sh bilioni 100 katika fungu la dharura ili iweze kulipa madeni ya walimu na iachane nao lakini hawasikii,” alisema Oluoch.
View detail

Friday, September 20, 2013

BOKO HARAM YAENDESHA OPERESHENI ABUJA

Vikosi vya usalama nchini Nigeria, vinasema vimeshambuliwa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la, Boko Haram, mjini Abuja. dakika 37 zilizopita

Vijana wanaotoa ulinzi kwa wenyeji dhidi ya Boko Haram
Vikosi vya usalama nchini Nigeria, visema kuwa vishambuliwa na wapiganaji wa kiisilamu , Boko Haram, mjini Abuja.
Vijana wanaotoa ulinzi kwa wenyeji dhidi ya Boko Haram










Vikosi hivyo vimesema kuwa watu kadhaa walijeruhiwa wakati wapiganaji hao walipowafiatulia risasi maafisa waliokuwa wanatafuta silaha haramu.
Mapigano haya yanakuja siku tatu baada ya shambulio lengine lililofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram katika jimbo la Borno.
Mwandishi wa azizicompdoc.blogspot.com katika eneo hilo anasema kuwa baadhi ya watu hawajulikani waliko na kuwa huenda zaidi ya watu miamoja waliuawa.
Katika siku tatu zilizopita wafanyikazi katika sekta ya afya wamekuwa wakiondoa miili ya watu waliofariki kwenye malori.

Afisa mmoja alisema kuwa alihesabu mili themanini na saba.
Lakini kuna uwezekano mkubwa kuwa miili zaidi inaweza kupatikana katika misitu na taarifa nyingine zinasema kuwa wapiganaji hao wanaodaiwa kuwa wa Boko Haram, waliwaua zaidi ya watu mia moja arobaini baada ya kuweka vizuizi vya barabarani na kuvalia magwanda ya jeshi wakijidai kuwa wanjeshi.
Jumanne shambulio karibu na Benisheik ni kati ya mabaya mno tangu hali ya hatari itangazwe Kaskazini Mashariki mwa Nigeria Mei.
Juhudi za kumaliza wapiganaji wa kiislamu zimefanya maeneo ya mijini kuwa salama lakini jeshi haliwezi kusema kuwa limeshinda vita kwani watu wanaoishi mashambani wamo katika hatari ya kushambuliwa.
Kwa sasa ni vigumu kupata habari kwani laini zote za simu zimekatwa katika juhudi za kuwasaidia wanajeshi kufaulu katika mpango wao.

Manusura wa mashambulio hayo yanayodaiwa kufanywa na Boko Haram wanasema kuwa wapiganaji hao walikuwa wamevalia sare za jeshi.
Waliwasili kwa magari , wakaweka vizuizi kati ya Maiduguri na Damaturu na wakaanza kuwaua watu.
Waliojaribu kukimbilia misituni walifuatwa na kupigwa risasi.
View detail

Tuesday, September 17, 2013

ICC YAPOKEA USHAHIDI KUTOKA KWA SHAHIDI WA KWANZA KTK KESI YA VIONGOZI WA JUU KENYA


Naibu Rais William Ruto alisindikizwa ICC na kikundi cha wabunge wa chama chake
Shahidi wa kwanza kutoka upande wa mashtaka, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ICC kutoa ushahidi dhidi ya naibu Rais wa Kenya William Ruto.
Mahakama inamlinda shahidi huyo kwa kutoonyosha sura yake.
Ruto anakabiliwa na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007-2008
Kesi dhidi ya Ruto na mshtakiwa mwenzake Joshua Arap Sang, ilianza tarehe 10 mwezi Septemba, baada ya wawili hao kutuhumiwa katika kuhusika na ghasia hizo za mwaka 2007.
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu mashahidi kujiondoa kwenye kesi hiyo wakihofia usalama wao. Mwishoni mwa wiki, mashahidi wanne walijiondoa katika kesi hiyo baada ya kuelezea wasiwasi kuhusu usalama wao ikiwa watatoa ushahidi mbele ya mahakama hiyo.
Wiki jana mkuu kwenye kesi hiyo, aliakhirisha kesi hiyo kwa sababu mashahidi hawakuwa wamefika kwenye mahakama hiyo kutoa ushahidi wao.
Rais Uhuru Kenyatta, anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Novemba kwa mashtaka sawa na hayo.
View detail

KAMBI YA KIJESHI MAREKANI YASHAMBULIWA NA WATU 12 WAPOTEZA MAISHA

Aaron Alexis
Mtu aliyewaua watu 12 katika kambi ya kijeshi nchini Marekani na kisha mwenyewe kuuawa, katika makabiliano na polisi, ametajwa kuwa mwanajeshi wa zamaji wa jeshi la wanamaji.
Aaron Alexis, 34, kutoka Fort Worth, Texas, aliuawa na polisi baada ya kuvamia kambi hiyo na kuwaua watu kiholela , mjini Washington DC.
Watu wengine wanane walijeruhiwa kwenye uvamizi huo ulioanza mapema asubuhi mnamo Jumatatu.
Rais Barack Obama aliamuru bendera kupeperushwa nusu mlingoti katika Ikilu ya White House na Capitol Hill.
Alisema anaomboleza kwa sababu ya mauaji mengine ya halaiki na kulaani kitendo hicho cha uoga.
Haijulikani kwa nini Aaron Alexis aliamua kufanya shambulizi hilo na kuwaua watu kati ya umri wa miaka 46-73.
Awali polisi walichukua hatua baada ya ripoti za watu wengine kujihami wakishirikiana na Alexis, lakini baada ya msako mkali wakasema kuwa hakuna dalili kwamba Alexis alikuwa na wenzake..
Valerie Parlave wa shirika la ujasusi la FBI alisema kuwa Alexis, aliyekuwa ameajiriwa na mwanakandarasi aliyekuwa anafanya kazi kwenye mtandao wa internet wa FBI, alikuwa na pasi ya kuingia kwenye eneo hilo.
View detail

Monday, September 16, 2013

Dr Jabir Kuwe Bakari ajitoa Bodi ya Bandari

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ameipangua Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuwaondoa wajumbe sita kati ya wanane kwa lengo la kuondoa migongano isiyo na tija ndani ya mamlaka hiyo.

Amewateua wajumbe wapya watatu na kusababisha iwe wajumbe watano ambao ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Mwakilishi wa wafanyakazi wa TPA ambao hakuwataja majina.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana, wajumbe waliondolewa ni Julius Mamiro, John Ulanga, Caroline Kavishe, Dk. Hildebrand Shayo na Asha Nasoro.
Dk. Mwakyembe pia amekubali ombi maalum la Dk. Jabiri Kuwe Bakari ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa e-Government, la kujitoa kwenye ujumbe ili aelekeze nguvu zake katika kuiimarisha taasisi yake ambayo huduma zake zitanufaisha idara na taasisi zote za Serikali ikiwamo TPA.

Katika mabadiliko hayo, Dk. Mwakyembe  amewabakiza wajumbe wawili ambao ni Saidi Sauko na Jaffer Machano. View detail

Thursday, September 12, 2013

MBIO ZA MWENGE ZATUA LINDI


 
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge taifa Juma Ali Simai akimkabidhi Mwenge wa Uhuru  mkimbiza mwenge namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mama Salma Kikwete wakati mwenge huo ulipowasili leo katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja. Wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Dk. Mohamed Nassor.
 Mkimbiza  Mwenge namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mchinga Mhe Said Mtanda wakati mwenge huo ulipowasili leo katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja. Kiongozi wa Mbio za Mwenge taifa Juma Ali Simai (hayupo pichani) alipongeza Mbunge huyo kutokana na moyo wake wa kujitoa na kushiriki katika mbio za mwenge mkoani Lindi na kuwataka wabunge waige mfano.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Taifa Juma Ali Simai akimkabidhi Mwenyekiti wa klabu ya kupinga  rushwa katika chuo cha Ufundi VETA kilichopo Manispaa ya Lindi Abdallah Makwinya kifurushi chenye nakala  mbalimbali zinazoeleza jinsi ya kupambana na rushwa chuoni hapo. Kushoto ni Mkimbiza  Mwenge namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
 Afisa kutoka Ofisi ya TAKUKURU mkoani Lindi Amos Ndege akielezea umuhimu wa klabu ya kupinga  rushwa  iliyopo katika chuo cha Ufundi VETA jinsi itakavyosaidia kutoa elimu kwa vijana. Wanaomsikiliza kwa makini ni Mkimbiza  Mwenge namba moja katika manispaa ya Lindi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Taifa Juma Ali Simai.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Taifa Juma Ali Simai akifungua  darasa litakalotumiwa na  klabu ya kupinga  rushwa katika chuo cha Ufundi VETA kilichopo Manispaa ya Lindi kwa ajiili ya kutoa elimu kuhusiana na madhara ya rushwa kwa jamii. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Dk. Mohamed Nassor.
 Mama Salma Kikwete akijumuika na viongozi wa Serikali na vyama vya siasa wa manispaa ya Lindi wakijiandaa kuupokea Mwenge wa Uhuru kutoka wilaya  ya Lindi zoezi hilo limeafanyika leo katika eneo la katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja. Ukiwa katika Manispaa ya Lindi Mwenge huo utafungua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5.
Wakimbiza Mwege Taifa, Viongozi wa Serikali wa wilaya ya Lindi na Askari Polisi  wakielekea  kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa viongozi manispaa ya Lindi  zoezi hilo limefanyika leo katika eneo la Mto Mkavu – Mbanja.
View detail

UFARANSA YAIONYA MAREKANI KUHUSU SYRIA

Rais Vladmir Putin ni mshirika mkubwa wa serikali ya Syria
Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ametoa ombi la moja kwa moja kwa raia wa Marekani kuhusu mgogoro unaoendelea nchini Syria.
Katika tahariri ya gazeti la New York Times, Putin ameonya kwamba shambulio lolote la jeshi la Marekani dhidi ya Syria litasababisha kuzuka kwa wimbi jipya la ugaidi na huenda likasababisha kubadilika kwa mfumo mzima wa sheria na utulivu wa kimataifa.
Amesema kuwa mamilioni ya watu wanaiona Marekani kama mfano wa taifa lenye demokrasia lakini hutumia sana nguvu.
Tahariri hiyo inachapishwa siku ambapo maafisa wakuu wa Marekani na Urusi wanatarajiwa kujadili yaliyomo katika pendekezo la Urusi la kudhibiti kimataifa silaha za kemikali za Syria.
Wakati huo huo kumekuwa na mapigano mazito nchini Syria katika kujaribu kuudhibiti mji mkongwe wa kikristo Maaloula, licha ya taarifa zinazoeleza kwamba kikosi cha serikali kiliudhibiti kutoka kwa wanamgambo wenye misimamo mikali ya dini ya kiislamu.
Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa rais wa Syria Bashar al-Assad, imependekeza kudhibiti silaha za kemikali zilizo nchini Syria.
Japan iliwahi kutumia silaha za kemikali dhidi ya wachina mwaka 1930, Mussolini akatumia silaha hizo nchini Ethiopia wakati wa vita vya pili vya dunia huku jeshi la Misri likitumia silaha hizo nchini Yemen miaka ya sitini.
Lakini yote haya hayawezi kufananishwa na kilichotokea eneo la Halabja. Mwezi Machi mwaka 1988, aliyekuwa rais wa Iraq Saddam Hussein aliamuru kutumiwa kwa gesi ya sumu dhidi ya wakurdi na kuwaua watu zaidi ya 5,000 papo hapo.
View detail

Tuesday, September 10, 2013

MAKAMU WA RAISI KENYA ATUHUMIWA ALIMILIKI JESHI LA KIVITA

Bwana Ruto na wafuasi wake alipokuwa anaondoka Kenya kuelekea Hague
Naibu rais wa Kenya William Ruto amekana mashitaka ya uhalifu katika kesi inayoendeshwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC , Hague Uholanzi.
Bwana Ruto -- ambaye anatuhumiwa kupanga ghasia za baada ya uchaguzi uliokuwa na utata wa mwaka 2007 -- amekana mashtaka hayo sawa na mshitakiwa mwenza katika kesi hiyo mtangazaji Joshua Arap Sang.
Mwendesha mkuu wa mashtaka katika ICC, Fatou Bensouda, alimtaja Ruto kuwa mwanasiasa shupavu ambaye alipanga kufanya uhalifu dhidi ya binadamu ili kujinufaisha kisiasa.
Amesema kuwa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, Ruto aliunda jeshi lake la kivita kumpigania dhidi ya mahasimu wake madai ambayo yamekanushwa na wakili wa Ruto bwana Khan
Bwana Ruto na Rais Uhuru Kenyatta pamoja na mwandishi wa habari Joshua Arap Sang, wanatuhumiwa kwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, kufanya mauaji kuchochea na kupanga ghasia hizo.
Rais Uhuru Kenyatta ambaye pia anatuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, anatarajiwa kufikia katika mahakama hiyo mwezi Novemba
View detail

Sunday, September 8, 2013

CHAMA CHA UPINZANI CHASHINDA NCHINI AUSTRALIA


Tony Abbott na familia yake wakipiga kura

Chama cha Australia cha Liberal-National kimeshinda katika uchaguzi mkuu.
Katika hotuba yake ya kukubali ushindi, kiongozi wa chama hicho, Tony Abbott, aliwaambia wafuasi kwamba ataunda serikali ya kuaminika na yenye uwezo wa utendaji.
Alisema baada ya mwaka kodi ya uchafuzi wa mazingira itafutwa, mashua zinazopeleka wakimbizi Australia kutoka Asia zitakuwa hazipo, na bajeti itakaribia kuwa na ziada.
Alipokiri kushindwa, kiongozi wa chama cha Labor, Kevin Rudd, alisema kuwa alimpigia simu Bwana Abbot kuitakia mema serikali mpya kwa changamoto kubwa inazokabili.
Aliwaambia wafuasi wake kwamba atajiuzulu kama kiongozi wa chama.
View detail

Friday, September 6, 2013

JE UNAHITAJI KAZI? NI MUHITIMU WA FANI MBALIMBALI? CHUO KIKUU HURIA KIMETANGAZA NAFASI ZA KAZI 41 KWA AJILI YAKO!

THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA
VACANCY ANNOUNCEMENT
The Open University of Tanzania (OUT)
The Open University of Tanzania (OUT) is a public university, established by the Act of Parliament No 17 of 1992. Since 1st January, 2007, the University has been operating under the OUT Charter Inc. of 2007, which is in line with the Universities Act No. 7 of 2005. Its stated mission is to continuously provide open and distance education, research, and public services for sustainable and equitable socio-economic development of Tanzania in particular, and the rest of Africa. The Open University of Tanzania operates through its temporary headquarters in Kinondoni, Dar es Salaam and its 27 regional centres in each region of Tanzania Mainland and two coordination centres in Zanzibar and Pemba Islands.
The University hereby invites applications from competent and suitably qualified persons, to enhance its human resource capacity needed to fulfill its mission, as follows Read more
View detail

WABUNGE WA CHADEMA WAGEUZA BUNGE UWANJA WA MAPAMBANO

Mbunge wa Mbeya mjini akijizuia kutolewa bungeni baada ya kufanya vurugu
Mbunge wa Mbeya mjini atolewa nje kwa kufanya vurugu bungeni
Jana, Bingwa wa Dunia wa uzani wa kati (super middle), unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF), Francis Cheka alitembelea Bunge baada ya kutwaa taji hilo karibuni na jana hiyohiyo, Bunge hilo lilishuhudia ngumi kavukavu katika vurugu kubwa pengine kuliko zote zilizowahi kutokea katika ukumbi wake.


Katika masumbwi hayo yasiyo rasmi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anadaiwa kumpiga kichwa Askari wa Bunge na kumchania sare na kung’oa kipaza sauti.
Mbilinyi jana alisema alikuwa anatafutwa na polisi huku akisema hilo limemshangaza akidai kwamba yeye ndiye aliyeshambuliwa na askari huyo.
Vurugu hizo zilitokea baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru kutolewa nje kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Katika vurugu hizo Mbilinyi alibebwa juujuu na polisi hadi nje ya ukumbi huku akiwa hana viatu.

Pamoja na tafrani hiyo, Ndugai alisema wakati akihitimisha kikao cha Bunge kipindi cha asubuhi kuwa amewasamehe wabunge wote waliohusika na kosa hilo la utovu wa nidhamu na kuwaruhusu kurejea kipindi cha jioni kuendelea na Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Hata hivyo, wabunge wote CUF, NCCR-Mageuzi na Chadema ambao baada ya tukio hilo walitoka nje ya ukumbi, hawakurejea na baadaye walitoa msimamo wa pamoja wakisema hawatashiriki katika mjadala huo.

Msimamo huo ulitolewa na Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mbunge wa CUF, Habib Mnyaa.
Mbowe alisema wameamua kususia majadiliano hayo kuonyesha msimamo wao wa kupinga kupitisha mambo yasiyo na masilahi kwa nchi.
“Hatuko tayari kushiriki katika uchakachuaji wa Katiba... Matumizi ya nguvu ya polisi kamwe hayatatupatia Katiba nzuri,” alisema. Alisema kambi rasmi ya upinzani inalaani vikali kitendo cha Ndugai kuruhusu Bunge kunajisiwa kwa kuruhusu polisi kuingia ndani kinyume na kanuni.

Mnyaa alisema kitendo cha wadau wa Zanzibar kutoshirikishwa katika kutoa maoni yao katika muswada huo wa marekebisho ni dharau kubwa.
Mbatia alisema Tanzania haiwezi kuingia Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kutumia Katiba ya sasa kwa sababu tayari kuna mgongano wa kikatiba kati ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu alimtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kutoa ushahidi kama Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kulingana na mapendekezo ya taasisi zao.

Kuanza kwa tafrani
Sakata hilo lilianza saa 6:45 mchana muda mfupi baada ya kukamilika kwa kura kuamua kama Bunge liahirishwe au la kutokana na hoja iliyotolewa na Mbunge wa Mkoani (CUF), Ali Hamisi Seif (CUF). Waliotaka liahirishwe walipata kura 59 na waliokataa 159.
Baada ya Ndugai kutangaza matokeo hayo na kutaka shughuli za Bunge ziendelee, Mbowe aliposimama na kusema ana hoja Naibu Spika alimwamuru akae chini.

Baada ya Mbowe kusisitiza ana hoja na kumwomba Spika amsikilize ndipo Ndugai alipomwamuru atoke nje na alipokaidi alisema:” Naomba askari wote waliopo katika mazingira haya (ya Bunge) waingie ndani ya ukumbi wa Bunge”.
Baada ya kitambo kifupi, Mbowe akiwa bado amesimama alitoa maagizo atolewe nje: “Kiongozi wa upinzani atolewe nje.”
Polisi waliingia ndani ya Ukumbi wa Bunge lakini Wabunge wa Kambi ya Upinzani kwa umoja wao, walimzinga Mbowe asifikiwe na askari hao.

Baada ya kuona polisi wanaelekea kushindwa, Ndugai alitoa maagizo mengine: “Askari hamjaletwa humu ndani kufanya majadiliano mnatakiwa kuhakikisha kiongozi wa upinzani anatolewa nje”.
Alisema yeye ndiye anayeendesha kikao hicho hivyo lazima Mbowe atolewe nje.
Hapo ndipo wabunge hao wa upinzani walipoanza kuimba: “Hatutaki kuburuzwa hatutaki kuburuzwa… hatutaki kuonewa,” huku wakiendelea kumzinga Mbowe.
“Askari wote mliopo humu ndani naomba mnisikilize… Sasa naagiza kwa mara ya mwisho... nasema kiongozi wa upinzani atolewe nje.”

Ngumi zarushwa
Baada ya kauli hiyo ya Ndugai, ndipo polisi walipotumia nguvu hasa kwa Mbilinyi na Mbunge wa Maswa Mashariki (Chadema), Silvester Kasulumbai.
Katika patashika hiyo, inadaiwa kwamba Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali alipigwa ngumi ambayo ilimfanya apepesuke hadi sakafuni.
Kilichomponza Mbilinyi ni hatua yake ya kusogelea Siwa. Polisi waliokuwa karibu, walimbeba juujuu hadi nje ya ukumbi.
Wakati akitolewa nje ya ukumbi, alijaribu kujizuia kwa kushika kipaza sauti kinachotumiwa na upande wa upinzani hadi kikang’oka.
Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Mozza Abeid, alivuliwa hijabu katika vurumai hizo wakati polisi walipokuwa wakitumia nguvu ili kumfikia Mbowe.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, Mbowe aliamua kutoka nje huku akisindikizwa na polisi pamoja na wabunge wa vyama hivyo na alipofika nje ya ukumbi alipokewa na polisi wa kawaida waliomweka chini ya ulinzi kabla ya kumwachia baada ya ombi la Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini.
Kutokana na hali ya mambo kuwa tete, askari wa Bunge waliwaondoa wageni waliokuwa wamekaa katika kumbi za wageni wakiwamo wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari huku baadhi ya wabunge wa CCM waliokuwa na simu za kisasa za mkononi na kompyuta mpakato (Ipad) wakichukua picha za tukio zima.
Inadaiwa kwamba baada ya kutoka nje ya ukumbi, Mbilinyi alimtwanga ngumi mmoja wa askari waliomtoa kwa nguvu kabla ya kuamuliwa na wabunge na polisi.
Wakati wote huo, wafanyakazi wa Bunge na wageni walionekana wakiwa wamejikusanya katika makundi wakitafakari na kushangaa yaliyokuwa yakitokea.


Balaa lilivyoanza
Akitumia Kanuni ya 69(1), Mbunge wa Mkoani (CUF), Ali Hamisi Seif, alitaka kuahirishwa kwa mjadala wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013 kutokana na ukweli kuwa Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala ya Bunge ilipaswa kukusanya maoni ya wadau mbalimbali nchini ikiwamo upande wa Zanzibar jambo ambalo halikufanyika wakati wa maandalizi ya muswada huo.
“Ilipaswa sheria hii inapotaka kufanyiwa marekebisho iende tena kulekule Zanzibar lakini jambo la kusikitisha kamati inayohusika na masuala ya Katiba haikwenda. Mimi ni mjumbe wa kamati na tuliitwa Dar lakini ratiba waliyotupa haikuonyesha kama tungekwenda Zanzibar,” alisema. Mkosamali naye aliomba mwongozo kwa Spika, akisema kwa kuzingatia matakwa ya kiapo cha Spika au Naibu alipaswa kuendesha Bunge kwa haki bila upendeleo.

“Kanuni inasema Spika ama Naibu Spika ama Mwenyekiti ataendesha shughuli za Bunge kwa haki, uadilifu, bila chuki wala upendeleo wowote kwa kuongozwa na Katiba ya nchi,” alisema na kuongeza: “Kwa kuwa sisi tumekuweka hapo ili uendeshe Bunge kwa uadilifu, usiburuzwe na chama chako na uzingatie miongozo yote kwa wakati. Kwa nini usitumie mamlaka yako kuondoa muswada huu”?
Mbunge wa Peramiho (CCM), Jenister Mhagama aliomba mwongozo kwamba kwa kuwa bado kuna malalamiko basi waipe Serikali nafasi ya kuthibitisha kwamba majadiliano ya kamati yalikamilika.

Lissu katika kuomba mwongozo wake, alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala, Pindi Chana alilidanganya Bunge alipowasilisha maoni ya kamati kwamba wadau wa muswada huo walishirikishwa jambo ambalo alisema si kweli.
Lissu alisema hakuna Mzanzibari aliyefika mbele ya kamati hiyo kutoa maoni kuhusu muswada wowote.
Hata hivyo, Chana alijibu akisema wadau wa Zanzibar walitoa maoni yao na kukabidhi nyaraka mbalimbali kwa Spika kuthibitisha kauli yake hiyo. Alivitaja vyama vya Jahazi Asilia na ADC kuwa vilihojiwa.
Kwa upande wake, Lukuvi alimshambulia Lissu kwa kauli yake ya juzi kwamba uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete ulikuwa na walakini. “Lissu alisema jana (juzi) kwamba wapo wadau ambao walisema ijapokuwa waliandikiwa barua ya kuwasilisha majina matatu kila moja ili Rais ateue mmoja lakini hakuna mjumbe aliyeteuliwa”.

Alitaja majina ya walioteuliwa kuwa ni Maria Kashonda (Tec), Jesca Mkuchu (CCT), Humphrey Polepole (Civil Society) na Profesa Palamagamba Kabudi (Kundi la Wasomi).
Lukuvi aliwataja wengine waliopendekezwa na taasisi zao na Rais kuwateua kuwa ni Mwamtumu Malale (Bakwata) na Dk Sengondo Mvungi (NCCR) na Profesa Mwesiga Baregu wa Chadema.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Fredrick Werema alisema katika mchakato wa muswada huo, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iliwasilisha maoni yake mbele ya kamati.
Alisema Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi aliwasilisha kwa kamati mapendekezo ya SMZ, Mei mwaka huu na mapendekezo hayo ikiwamo uteuzi wa wajumbe 166 yalizingatiwa.

Waacha muswada, wapiga vijembe
Baada ya kurejea katika kikao cha Bunge cha jioni jana, wabunge wa CCM waliopewa fursa ya kuchangia mjadala wa muswada huo walitumia muda mwingi kuwajadili wabunge wa kambi ya upinzani. View detail

Wednesday, September 4, 2013

WAHITAJI KUMILIKI BLOG? SULUHISHO NI HILI

WADAU HII NI PICHA YA BLOG TEMPLATE AMBAYO IKO SOKONI INAUZWA KWA ANAETAKA KUIMILIKI, NI NZURI KWA RADIO STATION, DJs, RADIO PRESENTER, WAMILIKI WA KUMBI ZA STAREHE NA WENYE BIASHARA AU KAZI ZINAZOFANANA NA HIZO. BOFYA HAPA KUIANGALIA
WASILIANA NASI KWA NO 0653 33 29 24 FACEBOOK , EMAIL: mnyengema@gmail.com

View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop