Welcome to our online store Portal

Template Information

Thursday, September 18, 2014

IUFRO2014 Blog Competition

How to Enter and Win

  • Write a blog article that introduces your research or project and how it relates to the overall Congress theme “Sustaining Forests, Sustaining People – The Role of Research”. See the FAQ’s for what makes a good blog post.
  • Submit your blog posting with a maximum word count of 750 along with any photos to blog@iufro.org in a .doc or .docx  file with the subject line “IUFRO2014 Blog Competition”.
  • Ensure to include a caption and credit for any photos submitted.
  • Entries must be received by 30th September 2014 (23:59hrs +12 GMT).
  • To increase your chances of winning, post your story on Twitter with the hashtags #IUFRO2014 and #RoleOfResearch, and encourage friends to comment, “like” and “share” your post on Facebook, and retweet your post on Twitter. The more views, comments, and votes your article receives the greater your chance of winning.
  • The winner who has the most popular article submitted to the #IUFRO2014 Blog Competition will receive a cash prize in the sum of USD 500.
  • Two additional finalists will be selected according to the article they submitted based on a popularity ranking with the most page views, comments and highest votes. These persons will receive a copy of “Forests and Globalization: Challenges and Opportunities for Sustainable Development“.
View detail

Tuesday, August 26, 2014

FURSA YA KUSOMESHWA NA MFUKO WA MWL NYERERE KWA WATANZANIA TUU

http://azizicompdoc.blogspot.com/

With effect from the 2013/14 academic year, the M
walimu Julius K. Nyerere Memorial Scholarship Fund began granting Scholarship in the United Republic of Tanzania. The Fund grants scholarship to top best undergraduate female Tanzanian students to pursue Mathematics and Science studies in Tanzanian universities.
It is also partly used to sponsor both male and female Tanzanians
top best students to pursue undergraduate studies in Economics Information Technology, Accounting and Finance as well as best
students intending to pursue Master’s programmes in those fields
Follow the link for more information
View detail

UMESHAWAHI KUJIULIZA KUHUSU KUPATA MAFANIKIO? MAJIBU ULIYAPATA?

Ulishawahi kujiuliza siku moja kua kwanini watanzania wengi tuna uwezo wa kifikra lakini hatufiki popote kwa mawazo na fikra zetu? Je ulishapata jibu? sasa fuatana mimi kujua jibu la swali hili, ni kutokana na kutofikiria tunaanzaje kutekeleza tunalolifikiria ktk vichwa vyetu, tunaipaje nafasi fikra yetu? tunalipaje nafasi wazo letu? je tunaweza kulielezea wazo letu? lakini haya yote niliyapata majibu ktk mafunzo mafupi niliyohudhuria KINUvation ktk mafunzo yalipewa jina la
Design for Development Bootcamp! ambayo yalinifanya nipanue uwezo wangu wa kiakili, kifikra na kuweza kuyawasilisha yale ninayoyafikiri ili yaweze kunisaidia mimi na watu wanaonizunguka bila kumsahau muajiri wangu kunafaika na elimu niliyoipata. Hakika ni pongezi kwao waliofikiria kutuletea mafunzo kama haya KINUvation chini ya usimamizi mkubwa wa Catherinerose Barretto na  Mr Max Krueger  pongezi kubwa kwa watu hawa
 



http://azizicompdoc.blogspot.com/
Hakika mafanikio hufurahisha sana pale unapoona ulilofikiri linafanikiwa
Akili hutulia sana pale unapojiandaa kuonyesha ulilolifikiria na kulifanikisha


http://azizicompdoc.blogspot.com/
Ni furaha isiyokifani pale ulilionyesha kwa wenzio linafanikiwa

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Hakika maelekezo na mafunzo lazima yafuatwe kabla ya lolote kufanyika

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Inafurahisha kila mtu anapopewa nafasi ya kusikilizwa na kuelezea analolifikiri lingefaa kunufaisha wengine


http://azizicompdoc.blogspot.com/
Hakika akili ukiituma yaweza kukupa majibu sahihi

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Kila mmoja akipewa nafasi kwa wakati wake maendeleo yanaweza kua makubwa zaidi

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Je na wewe umeshafikiria kuutoa ujuzi ulionao kwa wengine tena bila ya malipo?

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Hakika kila aliye na ujuzi wa jambo anapenda na mwingine aupate ujuzi huo, ni suala la furaha

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Ukiona Fursa huna budi kuifuata na kunufaika nayo


View detail

Thursday, August 21, 2014

MWINYI ATEMA CHECHE ZAWAGUSA VIONGOZI WAKUBWA NCHINI


http://azizicompdoc.blogspot.com/
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda (kwanza kushoto) akizungumza kwenye semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda (kwanza kushoto) akizungumza kwenye semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda akizungumza kwenye semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda akizungumza kwenye semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus (wa kwanza kushoto) akiwasilisha mada juu ya Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma kwa wanasemina.
Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus (wa kwanza kushoto) akiwasilisha mada juu ya Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma kwa wanasemina.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amesema bado viongozi wa umma wanatumia madaraka yao na Ofisi zao kwa kujinufaisha wenyewe na kuwasahau wananchi waliowaweka madarakani hivyo kuna kila sababu ya kuleta sheria ya kuziba mianya hiyo kwa viongozi wanaokwenda kinyume na maadili.

Alhaj Mwinyi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Alisema licha ya kuwepo kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 inayotumika sasa bado kumekuwa na wimbi kubwa la mienendo ya matumizi mabaya ya ofisi na madaraka kwa viongozi wa umma kwa kujinufaisha wenyewe kimaslahi.

“…Maana yake ni kwamba umma sasa haupewi kipaumbele unavyo stahiki. Maamuzi ya viongozi yanatolewa kwa maslahi binafsi na hivyo kudhihirisha kuwepo kwa tatizo la mgongano wa maslahi. Viongozi hao waliopewa dhamana na wananchi wanatumia rasilimali za umma ili kujinufaisha binafsi au shughuli zao ambazo wanazo pembeni,” alisema Rais huyo mstaafu.
Alisema hata hivyo sheria ya maadili ya viongozi wa umma imekuwa na mapungufu kwa kuwabana baadhi ya viongozi wa umma na kuwaacha wengine pamoja na watumishi wa umma hivyo kujikuta nao wakijihusisha na mgongano wa kimaslahi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa tayari Serikali imeona mianya hiyo na hivyo kuanza mchakato wa kuja na sheria maalum itakayo dhibiti hali hiyo. “…Nadhani mmewahi kusikia mara kwa mara namna ambavyo Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagiza Serikali kufanya jitihada za dhati ili kuhakikisha kuwa viongozi wa umma wanaacha au wanajiepusha na tabia ya kushiriki zaidi kwenye biashara na kuacha jukumu lao…,” alifafanua Mwinyi akiwaeleza washiriki wa semina hiyo.
Aidha aliipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kuanza mchakato wa kutungwa kwa sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma, ambapo itakapo kamilika huenda ikawa suluhisho la mgongano wa kimaslahi kwa viongozi na watumishi wa umma.

Rais huyo mstaafu aliwataka wanasemina kuijadili rasimu iliyowasilishwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kutoa maoni yao kuiboresha zaidi ili itoke na majibu ya kero ya muda mrefu ya Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.
Kwa upande wake, Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus akiwasilisha mada juu ya Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma kwa wanasemina kabla ya mjadala alisema wataalam wa Sekretarieti hiyo wamefanya utafiti kwenye mataifa mbalimbali na kutoka na mapendekezo ambayo yataongoza mjadala kuelekea kupata sheria nzuri.

Naye Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda akizungumza katika semina hiyo, alisema Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma walioiandaa itajadiliwa na wadau mbalimbali ili kupata maoni kabla ya kuwasilishwa kwenye baraza la makatibu wakuu kuboreshwa zaidi kabla ya mchakato kupanda ngazi za juu.

Aidha aliwataka wananchi na wadau wengine kuendelea kuijadili Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma pindi itakapo wafikia na kutoa maoni kwa lengo la kuiboresha zaidi ili itakapo kamilika iweze kufanya kazi vizuri na kujibu kero zilizopo katika eneo hilo la viongozi wa umma.
“…Mapendekezo ya sheria hii hayalengi kuwafanya viongozi kuwa maskini, bali kasi yao ya ukwasi iendane na hali halisi ya kipato chao. Sheria hii itakapopitishwa itapunguza ubinafsi wa viongozi walioko madarakani kujipendelea wenyewe na maeneo wanayotoka.” Alifafanua Jaji Kaganda.
View detail

Design for Development Bootcamp

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Interested in creating technologies and enterprises that improve the lives of people living in poverty? In this full day hands on workshop you will be introduced to the design cycle and and collaboratively work on solutions to real world problems

The workshop is co-hosted by Kinu and alumnus of this years International Development Design Summit (IDDS) in Arusha, who will introduce you to some of the concepts and tools used at IDDS.

Follow the link for more Information View detail

Wednesday, August 20, 2014

WANAFUNZI WA STASHAHADA YA UALIMU KUNUFAIKA NA MIKOPO


IMG_1680
Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
IMG_1689
Baadhi ya Waaandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Serikali  imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya stashahada maalum ya ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam.
“ Wanafunzi wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na stashahada maalum katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo wote watanufaika na mikopo ya elimu ya Juu.”Alisema Mwaisobwa
Akifafanunua, Mwaisobwa alisema kuwa lengo la mpango huo ni kusaidia kuondoa tatizo la walimu wa masomo ya sayansi hapa nchini .

Aidha Mwaisobwa alibainisha kuwa jumla ya maombi 58,037 ya mikopo  yalikuwa yamepokelewa hadi kufikia Julai 2014 ambapo maombi 37,689 ni waombaji wa kiume na 19,592 ni waombaji wa kike.
Pia Mwaisobwa alibainisha kuwa majina ya wanafunzi watakaopata mikopo kulingana na udahili yatatangazwa kwenye tovuti ya Bodi  ambayo ni www.heslb.go.tz .na taarifa hiyo itatangazwa katika vyombo vya habari.
Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) inakusanya wastani wa shilingi bilioni 3 kwa mwezi ikiwa ni marejesho ya mikopo iliyokwisha tolewa.
View detail

Wednesday, August 13, 2014

MOTO MKUBWA WAZUKA KTK MSIKITI WA MTAMBANI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Moto mkubwa umetokea ktk msikiti wa Mtambani uliopo endeo la Kinondoni "B" na kuunguza eneo lote la juu la msikiti huo ambako kunasadikiwa kulikua na madarasa kwa ajili ya shule inayomilikiwa na msikiti huo, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana ila inasemekana ulianza ktk chumba kimoja walichokua wanalala wanafunzi wa shule hiyo baadhi wa kike na inasemekana  huenda ikawa ni mshumaa ndio ulisababisha moto huo lakini hizi ni tetesi kwa baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo na tunangojea taarifa maalumu kutoka kwa kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni kuthibitisha chanzo cha moto huo. Endelea kutufuatili zaidi kupata taarifa yote ya tukio hili View detail

DR POUL FAUSTIN KIHWELO ATELULIA KUA JAJI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Dr. Paul Faustin Kihwelo ateuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kua Jaji, uteuzi huo utatekelezwa mara moja baada ya majaji wote walioteuliwa kuapishwa kesho Ikulu jijini Dar es salaam, Kabla ya uteuzi huo Dr. Paul Faustin Kihwelo alikua Mhadhir ktk Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ktk kitivo cha sheria na pia ni wakili wa kujitegema.
View detail

Monday, August 11, 2014

Tanzania Youth in Agribusiness Forum – Lindi and Mtwara

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Event Name: Tanzania Youth in Agribusiness Forum – Lindi and Mtwara Road show
Date: August 23, 2014 From 0830 am – 1700 pm
Location/Venue: Double M conference centre
City/Town: Lindi Town
Organized By: Agri-Pro Focus Tanzania, ANSAF, AMSHA and TGFA collaboration with Africare and LIMAS
Phone: AMSHA +255 716 966 447, TGFA +255 753 843 321/ 763846 255
Introduction
On 23rd August 2014, a consortium of organisations under the Agri-ProFocus Tanzania umbrella namely; AMSHA Institute of Rural Entrepreneurship and Tanzania Graduate Farmers Association (TGFA) in partnership with ANSAF, Africare and LIMAS will hold the Lindi and Mtwara road show. The road show aims to embrace agribusiness opportunities for youth employment by bringing key stakeholders in the agriculture sector to share experiences and best practices/achievements made by youth led enterprises and initiatives while addressing opportunities and challenges for youths engagement in agriculture value chains.
The Motto for TYIAF Lindi and Mtwara Road show is: “Kilimo Biashara ndio Mpango Mzima”which translates to “Agribusiness is a whole plan”

This road show follows is a continuation of the fulfilment Tanzania Youth in Agribusiness Forum (TYIAF) objectives which aim to:
1. Acknowledge achievements and address by sharing challenges of Youth Agribusiness Enterprises, youth role models, young Agro entrepreneurs and projects which support youths.
2. Share knowledge on existing opportunities and how best to tap into these opportunities through empowering youth and addressing their challenges.
3. Share the APF Tanzania online platform so that youth can use the platform to share, discuss, network and conducting business through the online market place.
4. Design and implement strategies for business partnership and knowledge sharing so as to engage more youth into Agribusiness.
5. Promote coordination among youth support projects and programs whether public or non state actors
6. Provision of a single multi stakeholder platform where key stakeholders for agriculture and youth development will meet in roundtable to share, exchange experience, realize opportunities and strengthen their efforts in promoting youth employment through entrepreneurship.

Rationale forthe TYIAF Lindi and Mtwara road show;
Currently, there are a number of projects and initiatives as well as policies which support and recognize the youth and their roles in social development. Nevertheless, despite the various efforts to promote the involvement of the youth in agribusiness, it is still not perceived as a viable business or employment option. This could be due to a number of factors including poor or no promotion of agribusiness
Opportunities, lack of incentives, even the conventional education systems which lack of enough practical oriented agribusiness skills, capacity as well as enough information as relate to clear policy implementations and the available agribusiness opportunities that inspired and motivated youths especially Graduates can tap into. But in other side Agriculture sector still offer varieties of entrepreneurial and employment opportunities in its subsector value chains. All this is happening in the face of a rising demand for food as population grows, and investment in agribusiness services for betterment of Agricultural sector growth Register now to attend
View detail

Saturday, August 9, 2014

SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 254 KWA FANI MBALI MBALI

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Procurement Services Agency (GPSA), The Tanzania Buildings Agency (TBA), The
Tanzania Broadcasting Corporation (TBC), Institute of Finance Management (IFM),
Mineral Resources Institute (MRI), Ocean Road Cancer Institute (ORCI), The Institute of
Judicial Administration (IJA), Ministry of Minerals and Energy and Tanzania Commission for
Science and Technology (COSTECH), Public Service Recruitment Secretariat invites
qualified Tanzanians to fill 254 vacant posts in the above public institutions.
On behalf of the Tanzania Automotive Technology Centre (TATC), The Government
Bofya hapa kuona nafasi zilizotangazwa View detail

Sunday, August 3, 2014

HATARI KUBWA YA MADEREVA WA MAGARI KUKOSA AJIRA


http://azizicompdoc.blogspot.com/
Gari linalojiendesha
Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa itaziruhusu gari zisizokuwa na madereva barabarani ifikapo mwezi Januari mwakani.
Serikali hiyo pia imetoa wito miji ya Uingereza zitoe mapendekezo ya kuwania kuwa wenyeji wa moja kati ya majaribio 3 ya magari hayo.
Aidha waziri huyo ameagiza kufanywe mabadiliko ya sheria za barabarani ilikuafikiana na mabadiliko hayo ya teknolojia.
Wizara ya usafiri wa umma nchini Uingereza ilikuwa imeahidi kuruhusu majaribio ya magari hayo mwisho wa mwaka uliopita.
Katibu wa Biashara Vince Cable aliyasema hayo katika hafla ya uzinduzi katika kiwanda cha kutengeneza magari cha Mira,kilichoko Midlands.
"tangazo hili la leo linatoa ithibati kuwa magari pasi na madereva yatakuwa barabarani katika miezi 6 zijazo''.
http://azizicompdoc.blogspot.com/
Uingereza kuruhusu magari bila ya dereva katika miezi 6 ijayo
Waandisi nchini Uingereza wakishirikiana na wanavyuoni kutoka chuo kikuu cha Oxford wamekuwa wakifanya majaribio ya matumizi ya magari hayo yasiyo na madereva.
Wadau hata hivyo wamekuwa wakiibua tahadhari ya maswala ya Bima,na uhalali wa magari pasi na madereva jambo ambalo limewalazimu kutumia barabra za kibinafsi kwa majaribio yao.
''Mimi mwenyewe nilijiskia kuwa salama ndani ya gari hilo lililokuwa bila dereva''alisema bwana Cable.
Wakati huohuo Magari hayo yameruhusiwa kufanyiwa majaribio huko Marekani katika majimbo ya California, Nevada na Florida.
http://azizicompdoc.blogspot.com/
Nissan imeruhusiwa kujaribu magari bila ya dereva
Gari linalonadiwa na kampuni ya mtandao wa Google tayari limetumika kwa zaidi ya kilomita laki tatu hivi katika mabarabara ya umma.
Mwaka uliopita kampuni ya 2013 ilifanya majaribio ya gari lake huko Japan.
Barani Uropa kampuni ya kutengeza magari ya Volvo tayari imepata ithibati ya kujaribu magari yake mjini
Gothenburg Sweden.
View detail

ISRAEL YAZIDI KUWAUA WATOTO NA RAIA WASIO NA HATIA GAZA

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Gaza
Ripoti za hivi karibuni zinaarifu kuwa shambulizi la angani la Israel limewauwa watu saba katika shule moja ya umoja wa mataifa katika mji wa Rafah.
Walioshuhudia wanasema kuwa kombora hilo lilipiga eneo moja karibu na mlango wa shule hiyo.
Usiku kucha Israel ilirusha makombora 13 ya angani yaliowauwa watu 13 waliuawa huku makombora mawili ya roketi yakirushwa nchini Israel.
Msemaji wa Jeshi la Israel Luteni kanali Peter Lerner amesema kuwa baadhi ya wanajeshi wanaondolewa katika eneo la Gaza ,lakini oparesheni hiyo itaendelea.
Wajumbe wa Hamas wamewasili katika mji mkuu wa cairo nchini Misri kwa mazungumzo ya kusitisha vita.
Israel imesema kuwa haipelekwa wawakilishi wake.
Wakati huohuo Msemaji wa umoja wa mataifa katika eneo la Gaza ameonya kuwa maafa makubwa ya kiafya huenda yakazuka katika eneo la Gaza kufuatia wiki tatu za mapigano katika eneo hilo.
Chris Gunness kutoka shirika la umoja wa mataifa linalosimamia misaada amesema kuwa maafisa wa afya katika eneo la Gaza wanaendelea kulemewa.
Amesema kuwa hospitali,zahanati na ambulansi zimeharibiwa na kwamba zile zinazotoa huduma zimezidiwa huku asilimia 40 ya maafisa wa afya wakishindwa kufika kazini View detail

Thursday, July 31, 2014

Bill & Melinda Gates Foundation Grant Opportunity of $5,500,000


http://azizicompdoc.blogspot.com/
The Bill and Melinda Gates Foundation along with the UK Department of International Development (DFID) call Concept Memo from organizations willing to design and manage small grants program to conduct research on the drivers of food choice among poor people in developing countries.
The grant recipient will design and competitively tender a research call and award and manage up to 15 small research grants to the sub-grant recipients.
For more information Follow the Link View detail

Monday, July 28, 2014

NCHI GANI INASWALI EIDY J3 TAR 28/07/2014? PATA TAARIFA ZOTE HAPA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Kutokana na wengi kutokua na elimu ya mwezi ili waweze kufanya maamuzi, mwandishi wetu ameamua kuleta darasa hili kwa wasomaji wetu ili iweze kuwasaidia wenye kujifunza na kua msaada kwao, kumbuka lengo letu ni kuwaelimisha wasomaji wetu Bofya hapa kwa maelezo zaidi View detail

Sunday, July 20, 2014

TAPELI MKUBWA AKAMATWA JIJINI DAR


10500539_819006161445574_7780628803053090260_n

Tapeli lililokubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka washirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.

Kwa mujibu wa Bi. Usia akieleza tukio hilo, alidai kuwa  tapeli huyo alifika asubuhi  akiwa na wenzake sita,  nyumbani kwake  wakasema wanatoka Tanesco wamekuja kucheki mita ya Luku. Hata hivyo  wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung’oa mita, eti waliona kwenye GPS  yao kuwaUmeme hauendi vema.

“wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa kinafyatuka halafu  Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.

Na kuongeza kuwa  vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange. tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuite Polisi,  basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme,  nikawaambia naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi chuo nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani, tukawakuta wameondoka.

Mzee akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City, tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo, tukaandikisha maelezo. tunasubiri hatua itakayofuata.
10417599_819006198112237_2101442257557265538_n

View detail

MAJINA YA WANAOITWA KAZINI AJIRA ZA SERIKALI

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb. Na. EA.7/96/01/G/35 01 Julai, 2014
KUITWA KAZINI
http://azizicompdoc.blogspot.com/

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu
waombaji kazi wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 04
hadi 12 Juni, 2014 kuwa walioorodheshwa katika tangazo hili wamefaulu
usaili na wanatakiwa kuripoti kwa Mwajiri kama ilivyoonyeshwa katika
tangazo hili. Bofya hapa kuendelea kusoma
View detail

Thursday, July 3, 2014

OFA MAALUM YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KWA VIFAA VYA TEKNOLOJIA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Kutokana na mahitaji makubwa ya vifaa vya teknolojia nchini, Azizi Matelephone and Electronics imekuletea vifaa vipya na kwa bei nafuu kwa ofa maalumu kwa mwezi mtukufu wa ramadhani, kuona vifaa unavyoweza kuvipata Bofya hapa View detail

Wednesday, June 25, 2014

SISTA WA KANISA KATOLIKI APIGWA RISASI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Wananchi wakiangalia sehemu ambayo majambazi walimpiga risasi Sista Clencensia Kapuli Ubungo, Riverside, Dar es Salaam jana. Picha na Michael Matemanga 

Majambazi wamemuua kwa risasi Sista wa Kanisa Katoliki Clencensia Kapuli (50) na kupora kiasi kikubwa cha fedha ambacho hakijajulikana.
Pia, katika tukio hilo lililotokea jana saa nane mchana eneo la Riverside, Ubungo, Dar es Salaam, dereva aliyekuwa akimwendesha Sista Kapuli, Patrick Mwarabu alikatwa kidole gumba kwa risasi.
Sista Kapuli wa Shirika la Mtakatifu Maria wa Parokia ya Mwenyeheri Anwarite, Makoka Jijini Dar es Salaam alikuwa mhasibu wa parokia hiyo ambayo inamiliki Shule ya Sekondari Mwenyeheri Anwarite na Chuo cha Ufundi Stadi Makoka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura aliyefika katika Kituo cha Polisi Urafiki kufuatilia tukio hilo alisema Sista Kapuli na sista mwenzake wakiwa katika gari aina ya Toyota Hilux, walikuwa wakitoka Benki ya CRDB, Tawi la Mlimani City kuchukua fedha na walipita Riverside ndipo walipopatwa na mkasa huo.
“Bado hatujajua ni kiasi gani cha fedha kimechukuliwa kwa kuwa Sista Kapuli ndiye alikuwa mhasibu na ndiye aliyekwenda kuchukua fedha hizo, subirini tutakapokwenda benki kuuliza ni kiasi gani cha fedha alichukua na tutawajuza,” alisema Wambura.
Kamanda huyo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ukisubiri taratibu za mazishi.
Shuhuda wa tukio hilo, Gadi Kinyamagolo alisema masista hao walikwenda Riverside kununua mchele katika moja ya maduka ya jumla.
“Mara baada ya kumaliza kununua mchele kama kilo 10 hivi walipanda katika gari wakiwa wawili na kabla ya kuondoka zilifika pikipiki mbili zikiwa na watu wanne, zikasimamisha gari hilo huku mmoja akiwa amevalia kininja na mwingine aliyevaa kawaida, wote wakiwa na silaha. Wengine wawili walibaki kwenye pikipiki.
“Kisha nikaona wanapasua kioo cha nyuma ambapo kulikuwa na sista mmoja na mwingine alikuwa mbele, wote wakiwa na mikoba ambayo majambazi hao waliiomba,” alisema Kinyamagoro na kuongeza:
“Walianza kuwaambia tupe mikoba huku majambazi hao mmoja akiwa amesimama upande wa dereva na mwingine upande wa pili wa gari alipokuwa sista aliyeuawa lakini masista wale hawakutoa mikoba hiyo.”
Kinyamagoro alisema: “Baada ya mabishano, sista aliyekuwa nyuma alifungua mlango na kukimbilia katika duka walilonunua mchele na yule aliyekuwa mbele alipofungua mlango akitaka kukimbia alipigwa risasi shingoni na kutokea upande wa pili na kuanguka nje ya gari.
“Baada ya tukio hilo majambazi hayo yalichukua mikoba miwili na kuondoka nayo. Kwa kuwa mimi nilikuwa karibu nililala chini na eneo hili lilikuwa kimya, watu walikimbia na wengine tulilala tukaacha wafanye kazi yao.”

Shahidi mwingine, Saidi Juma alisema: “Wakati majambazi hao wakiondoka palikuwa na watu wawili waliovalia sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakipita eneo hilo, waliulizwa na majambazi wanafanya nini huku wakiwa wameonyeshwa bunduki. Walinyoosha mikono juu na kuachwa, kisha majambazi wakapanda pikipiki zao na kutokomea.
“Wakati majambazi wakiondoka watu hao waliruka na kulala mtaroni kukwepa kupigwa risasi. Majambazi walipofika hapo mbele (mbele kidogo ya eneo la tukio), walimpiga risasi muuza machungwa na kumjeruhi begani.”
View detail

Tuesday, June 24, 2014

POLISI WATANGAZA HALI YA HATARI KUHUSU NGOMA YA KIGODORO

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, jana. Picha na Venance Nestory 

Jeshi la Polisi nchini limetangaza kuanzishwa kwa operesheni maalumu ya kuwasaka wasanii wa ngoma wanaocheza wakiwa uchi maarufu kama kigodoro na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Pia, litafanya operesheni ya kuwasaka madereva wa bodaboda, bajaji na baiskeli za matairi matatu wasiofuata sheria za usalama barabarani.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senso alisema “Tunalaani vikali vikundi vya ngoma ambavyo hivi karibuni vimeibuka kwa wingi na huwa vinafunga mitaa na barabara huku wanawake wakicheza wakiwa uchi.’’
Hivi karibuni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipiga marufuku ngoma za aina hiyo.
Alisema kuwepo kwa vikundi hivyo ni uvunjaji wa sheria na maadili ya nchi, jeshi hilo litawasaka popote walipo ili kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Alisema vikundi vya ngoma vinatakiwa kufuata utaratibu unaowekwa na halmashauri za maeneo husika ili kuzuia mianya ya kukiuka maadili.
Akizungumzia tukio la juzi la wachezaji wa kigodoro kudai kupigwa risasi eneo la Mwananyamala, alisema hakuna msanii aliyepigwa risasi, waliumia wakati wa purukushani zilizotokea polisi walipokuwa wakiwatawanya watazamaji wa ngoma hiyo.
“Hata ripoti ya daktari kutoka Hospitali ya Mwananyamala inaonyesha wacheza ngoma hao hawakupigwa risasi kama wanavyodai wao,” alisema Senso.
Akizungumzia operesheni ya bodaboda alisema, “Imekuwa  kawaida kwa madereva wa vyombo hivyo kupita barabarani wakati taa nyekundu zikiwa zinawaka hali ambayo husababisha ajali nyingi. kutokea.”
Alisema kuanzia Januari mpaka Juni, mwaka huu, ajali 1,449 zilizosababishwa na vyombo hivyo zilitokea na kusababisha vifo 218 huku watu 1,304 wakijeruhiwa.
View detail

MAKAMU WA RAIS WA CHINA APOKELEWA TANZANIA NA DKT BILAL

 

1
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo juni 23, 2014 akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita. (Picha na OMR).
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 23, 2014 akiongozana na Ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.  Wa pili (Kulia) ni Balozi wa Tanzania, nchini China, Luteni General Abraham Shimbo.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo June 23, 2014. Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.
4.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia) na baadhi ya Mawaziri wake, akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao, aliyeongozana na ujumbe wake  wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 23, 2014 kwa ajili ya mazungumzo.  Li Yuanchao, yupo nchini kwa ziara ya siku sita.
5
Baadhi ya Mawaziri waliofika katika mazungumzo hayo Ikulu jijini Dar es Salaam, na baadhi kusaini mikataba na watu wa China.
6
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kulia) akisainiana mkataba na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, wa Makabidhiano ya gari la matangazo la Shirika la Utangazaji la TBC, yaliyofanyika mapema mwaka huu. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao.
7
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, (kulia) akisainiana mikataba miwili na Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara ya Wau wa China, Li Jinzao, ya makubaliano ya ushirikiano wa Kitaalamu utakaoiwezesha China kuwapa mafunzo Wanariadha wa Tanzania nchini China na wa makubaliano ya awamu ya tatu ya Ushirikiano wa kiufundi baada ya China kusaidia na kukamilisha Ujenzi wa Uwanja wa Taifa. Shughuli hiyo ya kutiliana saini imefanyika leo Juni 23, 2014, Ikulu jijini Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Li Yuanchao. View detail

SUMATRA YAKAMATA MABASI 25 YA UDA JIJINI DAR

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Mabasi mengine 25 ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), yamekamatwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Majini na Baharini (Sumatra), kutokana na kuendelea kukaidi amri ya kuwataka wafuate sheria za usafirishaji wa abiria jijini.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mfawidhi wa Sumatra, Conrad Shio alisema mpaka sasa wameshayakamata mabasi 40, kati ya hayo, 15 yalikamatwa wiki iliyopita.
Madereva wa mabasi hayo wanadaiwa kufanya makosa tofauti ikiwa ni pamoja na kutokuwa na leseni ya uchukuzi wa abiria jijini Dar es Salaam, inayotolewa na mamlaka hiyo, stika na vibao vya kuonyesha njia wanazokwenda.
Shio alisema walipoyakamata awali na kuyaachia, uongozi uliahidi kutekeleza maagizo waliyopewa na Sumatra lakini hawajayatekeleza mpaka sasa.
Alisema pia wamesitisha kwa muda kazi ya kuyakamata na sasa wanaendelea na mazungumzo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema baada ya mazungumzo hayo, atakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kuzungumzia hatua zaidi ambazo watachukua au kile ambacho watakuwa wameafikiana kwa vyombo vya habari.
“Tumeona tusitishe operesheni hii ya kuyakamata mabasi haya ili kutoa nafasi ya mazungumzo chini ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa na iwapo mwafaka usipofikiwa tutajua cha kufanya” alisema Shio.
Kulingana na makosa ambayo yamekutwa katika mabasi hayo, kila basi litalazimika kulipiwa Sh250,000 na kwa mabasi 40, Uda watalazimika kulipia Sh10 milioni. Wiki iliyopita, Sumatra ilianzisha operesheni ya kuyakamata mabasi ya Uda kutokana na  malalamiko ya wananchi kuwa yamekuwa yakivunja sheria na hayana stika wala vibao vinavyoonyesha njia wanazopita.
View detail

Saturday, June 21, 2014

SAMSUNG, BIDHAA MAALUM KWA MAZINGIRA YA AFRIKA


Print
Ukuaji endelevu wa uchumi wa Tanzania umeona ongezeko la kampuni za nje zikiingia nchini zikiwa na nia ya kuzindua bidhaa au huduma zao kwa Watanzania walio wengi. Mafanikio kwa bidhaa na huduma hizi yanategemea mambo mengi kuanzia mazingira hadi uhitaji, kuonyesha kwamba zinakubalika katika soko.

Kampuni moja ambayo imeona mafanikio yaliotulia na kua mtoa huduma tegemezi kwa Watanzania, ni kampuni ya vifaa vya umeme ya Samsung. Kupitia bidhaa zao mbalimbali wameshuhudia mauzo ya zaidi ya bidhaa zao 50,000 ndani ya mwaka mmoja. Katika mwaka ambao unatarajiwa kua wa mafanikio kwa kampuni hii Wanatazamia kudaka asilimia 30 ya soko la vifaa vya kielektroniki.
Takwimu hii inaweza kuja kama mshangao lakini ikiwekwa kwenye mtazamo halisi inajenga picha yenye uwazi. Mafanikio haya yanatokana na utafiti katika soko la Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla.  Ukichanganya mambo kama vile uhitaji wa vifaa vinavyo okoa gharama na zenye uwezo wa kuhimili mazingira ya Kiafrika. Kampuni ya Samsung imeendelea kua mbele kutokana na ubunifu wa bidhaa ambazo kwa pamoja zajulikana kama “Built for Africa”. Sehemu ya friji ndio inazidi kupendwa na wateja wengi katika miaka michache iliopita kutokana na kuaminika na uwezo wa kuhimili mazingira ya Kiafrika. Katika kujengea mafanikio hayo, Samsung inaangalia kulenga soko kupitia aina mpya za friza zinazofaa kwa matumizi ya nyumbani na biashara. Uhitaji wa kuwa tofauti na asili ya uongozi ndio inaweka jina sokoni mpaka sasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Tanzania Bw. Dongha Jang aliunga mkono kauli zilizotajwa alipohojiwa na kusema “Samsung daima inatafuta kuunganisha wateja wake na bidhaa zake kwa kutoa bidhaa zinazosaidia kustawisha maisha ya mtumiaji. Sisi lengo letu ni kuleta teknolojia ya kisasa katika mfumo ambao ni muhimu zaidi kwa soko la Tanzania.” Mr. Jang alifafanua zaidi kuhusu uzinduzi wa bidhaa kadha moja kwa moja kwenye soko la Tanzania “katika hiki kipindi cha miaka michache iliopita tumeona umuhimu wa kuleta bidhaa mpya moja kwa moja kwa watumiaji wetu wa Tanzania kuliko kutegemea uzinduzi kwenye soko la kimataifa”. Miongoni mwa bidhaa Bw. Jang alizokuwa anaongelea katika msemo wake ni uzinduzi sambamba wa bidhaa mbili muhimu za nyumbani ambazo ni Samsung Duracool freezer na Triangle AC.

Uzinduzi huo ulikuwa sehemu ya mkakati wa kudumisha nafasi ya Samsung kama kiongozi wa vifaa vya umeme katika majumba ya Watanzania. Samsung Duracool freezer na Triangle AC zina sifa zinazoruhusu ufanyaji kazi kwa kiwango cha juu ukizingatia mazingira magumu ya Tanzania ikiwemo usambazaji wa umeme usioaminika na gharama zinazo panda. Samsung wanakuja na ahadi ya kurahisisha maisha kwa kuwa na bidha zenye gharama nafuu kwa mtumiaji.
Katika soko ambalo halitabiriki kama la Tanzania, kampuni hii ya vifaa vya umeme imeweza kutambua maeneo yaliokuwa ya maslahi kwa wateja wake kimahesabu. Hii ni dhahiri leo kupitia uwepo wake katika mitaa mbalimbali nchini. Katika mazingira ambayo hayana uhakika wa mafanikio kwa wote, Samsung inaendelea kushinikiza mipaka ya ubunifuu wa bidhaa  ambazo “zimetengenezwa kwa ajili ya Africa”.
View detail

RAIS KIKWETE KURUDIA KAZI YA UALIMU BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE

Jakaya-Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anakusudia kurejea darasani kushika tena chaki kwa kuwa mhadhiri kwenye Chuo cha Taifa cha Ulinzi – National Defence College (NDC) cha Dar Es Salaam.
Rais Kikwete amelieleza hilo mchana wa jana, Ijumaa, Juni 20, 2014, wakati alipotoa Mhadhara (Lecture) kuhusu Usalama wa Taifa (The Security of the Nation) mbele ya wanafunzi wa Chuo hicho kilichoko Kunduchi, Dar Es salaam.
Rais Kikwete amewaambia wanafunzi wa kozi ya pili ya Chuo hicho kutoka nchini na nchi za jirani za Uganda, Kenya na Rwanda: “Najisikia mwenye raha sana kuweza kurudi darasani kutoa mhadhara huu. Tukio hili linanikumbusha enzi zangu katika Chuo cha Kijeshi cha Monduli (TMA). Ni matarajio yangu pia kuwa nitaweza kurudi kuwa mhadhiri katika Chuo hiki baada ya kukamilisha kazi yangu ya sasa.”
Rais Kikwete ambaye alizungumza kwa kiasi cha saa mbili, alianza mhadhara wake baada ya kupata maelezo kuhusu maendeleo ya Chuo hicho na baadaye akajibu maswali ya wanafunzi ambao walimwuuliza kuhusu mambo mbali mbali yanayohusiana na usalama wa nchi.
NDC kilianzishwa rasmi Septemba 2, mwaka 2012 na Chuo hicho kilizinduliwa Rais na Rais Kikwete Septemba 10, mwaka huo huo, 2012 wakati alipotembelea Chuo hicho kwa mara ya kwanza kufuatia juhudi kubwa za uongozi wake kuhakikisha kuwa chuo cha namna hiyo na cha aina yake kinaanzishwa nchini. Rais pia alifungua kozi ya kwanza ya Chuo hicho.
Kundi la wanafunzi wa kwanza kwenye Chuo hicho lilimaliza mafunzo yake Julai 23, mwaka 2013 na sasa chuo hicho kinaendesha kozi ya pili yenye wanafunzi 30. Chuo hicho tayari kimepata usajili kamili wa NECTA ambako kina uwezo wa kutoa shahada ya uzamili katika masomo ya Strategic Studies.
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop