Welcome to our online store Portal

Template Information

Thursday, February 27, 2014

WARIOBA AWEKEWA KINGA YA KUTOHOJIWA

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Kamati ya Kupitia Rasimu ya Kanuni za Bunge la Katiba imependekeza Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba asiulizwe maswali wakati wa kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba.
Akiwasilisha mapendekezo hayo jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Costa Mahalu alisema wanataka Jaji Warioba afanye kazi moja ya kusoma Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya bungeni.
Profesa Mahalu alisema baada ya hapo wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba watakuwa na kazi ya kujadili kwa kina Rasimu ya Katiba kabla ya kuipitisha au kuikataa.
Pendekezo kuhusu Jaji Warioba kusoma Rasimu bungeni imo katika Kanuni ya Pili ya kanuni ndogo ya (d) ya Rasimu ya Kanuni, ambayo inampa nafasi Jaji Warioba kuwasilisha kazi aliyoifanya na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
View detail

KIKWETE ANGURUMA WARAKA WA CCM

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Waraka unaodaiwa kuandaliwa na CCM kwa ajili kuwaelekeza wajumbe wake kwenye Bunge Maalumu la Katiba kutetea msimamo wa Serikali mbili umepokewa kwa hisia tofauti huku Rais Jakaya Kikwete akitakiwa kujitokeza hadharani kueleza msimamo wake.
Waraka huo uliibuliwa na Blog hii jana ukibainisha sura ya Serikali mbili inayotakiwa na CCM, likiwamo pendekezo la kuanzisha Baraza la Wawakilishi la Tanzania Bara.
Miongoni mwa waliozungumzia waraka huo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa ambaye amemtaka Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kutoka hadharani na kuweka wazi msimamo wake kuhusiana na mchakato wa Katiba Mpya.
Dk Slaa alieleza kushangazwa kwake na hatua ya CCM kuandika waraka aliodai umebadili vipengele vyote muhimu katika Rasimu ya Pili ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba baada ya kukusanya maoni kwa wananchi.
Pia amemtaka Rais Kikwete kutozindua Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kwa madai kwamba kiutaratibu, linajitegemea na hata katika historia ya Katiba zilizowahi kuandikwa hazijawahi kusainiwa na rais.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea ubunge katika Jimbo la Kalenga, Iringa kupitia Chadema, Grace Tendega uliofanyika katika Kijiji cha Tanangozi, Kata ya Mseke.
Alisema Rais Kikwete na chama chake wanataka kubadili mambo yote muhimu yaliyoandikwa katika Rasimu ya Pili inayojadiliwa mjini Dodoma, huku akijua kuwa zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania ndiyo waliotoa maoni.
Wengine wauponda
Mjumbe wa Bunge la Katiba, James Mbatia alisema ushawishi katika jambo lolote siyo dhambi, lakini hakutarajia ushawishi huo kufanywa na CCM, tena katika jambo nyeti kama mchakato wa Katiba.
“Kama suala ni Serikali tatu, hayakuwa mapendekezo ya Jaji Warioba, bali ya tume nyingi zilizowahi kuundwa na Serikali inayotokana na chama hicho tawala. Kuna Tume za Jaji Robert Kisanga, Francis Nyalali, William Shelukindo, Amina Salum Ali na sasa Joseph Warioba. Zote hizi zimependekeza Serikali tatu.”
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema CCM kutengeneza waraka huo ni sawa na `utekaji nyara’ wa maoni ya wananchi na kuweka maoni ya wana CCM katika Katiba Mpya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo-Bisimba alisema kitendo cha CCM kutengeneza waraka wake ni kukwamisha upatikanaji wa Katiba bora.

“Hakukuwa na sababu ya kuweka Tume ya Mabadiliko ya Katiba iwapo nao wanakuja na waraka wao, tunatakiwa kuboresha yaliyomo kwenye rasimu ili tuweze kupata Katiba yenye maoni ya watu,” alisema.
Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Gaudence Mpangala alisema iwapo CCM kimesambaza waraka huo, kinafanya makosa kwa kuendeleza misimamo isiyokuwa na hoja za msingi kwa Watanzania... “CCM kusambaza waraka huo ni dalili mbaya za kuleta machafuko miongoni mwa wajumbe...”
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Nicholas Mgaya alisema hatua ya CCM kusambaza waraka huo ni kutapatapa kwa kuwa yaliyomo hayatawezekana kupitishwa na Watanzania.
Mgaya alisema waraka huo umevunja Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayozuia kusambaza maoni ya makundi katika mchakato huo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alisema tatizo siyo kuwa na msimamo wa chama kupitia waraka huo, bali kuusambaza... “Sijaupata waraka huo lakini kitendo cha kuusambaza tu kisheria ni makosa, walitakiwa kutumia nafasi na wajumbe wake kupeleka hoja hizo bungeni,” alisema Kibamba.
Wabunge CCM wanena
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema katika hali ya kawaida, kila kundi katika jamii lina fikra zake kuhusu mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na haki ya kupendekeza kile ambacho linaona kinafaa kuongezwa au kuondolewa na kwamba kuwa na mtazamo tofauti kuhusu jambo fulani ni kitu ambacho hakizuiliki.
“Binafsi ningependa kupata waraka kutoka kila kundi ili nisome na kujua mawazo mazuri yaliyopendekezwa. Ukipitia ni wazi kuwa utakutana na mambo mazuri tu. Hili ni jambo ambalo lipo wazi kabisa.”
Hata hivyo, Ndugai ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa (CCM) alisema chama hicho hakijagawa rasimu yoyote.
Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla alisema hana hakika iwapo waraka huo umesambazwa kwa wajumbe.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy naye alisema hajauona waraka huo, kauli ambayo iliungwa mkono na Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage.
Jana, Blog hii ilichapisha taarifa za kuonekana kwa waraka huo, ambao pamoja na mambo mengine, umetoa mapendekezo katika ibara 42 za Rasimu ya Katiba ya Tume na kupangua hoja mbalimbali ikiwamo ya muundo wa muungano huku ikitaka mfumo wa Serikali mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho.
View detail

MAGHOROFA MANNE DAR YATUMIA UMEME ZAIDI YA UTUMIWAO MTWARA

http://azizicompdoc.blogspot.com/

http://azizicompdoc.blogspot.com/

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Ghorofa nne za kisasa zilizopo Dar es Salaam, zinatumia kiasi kikubwa cha umeme kuliko ule unaotumiwa katika Mkoa wa Mtwara.
Majengo manne ya PSPF Twin Tower, Uhuru Height, Viva Tower na Benjamin Mkapa Tower yote kwa pamoja yanatumia megawati 12 za umeme wakati mkoa huo unatumia megawati nane.
Kiasi hicho cha umeme kinachotumiwa na majengo hayo ni karibu sawa na umeme unaotumiwa na mkoa huo na Lindi kwa pamoja.
Aidha, majengo matatu ya PSPF Twin Tower, Uhuru Height na Viva Tower kwa pamoja yanatumia umeme mwingi kuliko ule unaotumiwa na baadhi ya mikoa nchini kama Ruvuma, Manyara, Singida, Kigoma na Rukwa.
Akizungumza katika mahojiano maalumu hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco, Felchesmi Mramba alisema PSPF peke yake linahitaji megawati tano na Uhuru Height megawati 2.5, Viva Tower megawati 2.5 na Benjamin Mkapa Tower megawati mbili.
Alitaja matumizi ya umeme katika mikoa hiyo na megawati zake kwenye mabano kuwa ni Manyara (10) Mtwara (8), Singida (7), Lindi (5.5), Kigoma (6), Ruvuma (4.7) na Rukwa (6.8).
Alisema Dar es Salaam inaongoza kwa kutumia umeme mwingi na kwamba mahitaji ya nishati hiyo yamekuwa yakiongezeka kutokana na ukuaji wa haraka wa sekta ya ujenzi.
Dar es Salaam pekee, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) matumizi yake ni kati ya megawati 450 na 500 kwa siku, kiasi ambacho ni zaidi ya nusu ya umeme unaozalishwa na shirika hilo.
Alisema hivi sasa umeme unaozalishwa ni wastani wa megawati 1,100, huku sehemu kubwa ya nishati hiyo ikitokana na mitambo inayotumia gesi na mafuta.
Kutokana na hali hiyo, alisema Tanesco imeamua kutekeleza miradi 13 ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umeme ikiwamo kuongeza uwezo wa njia za kusambaza na kukarabati. Pia kujenga vituo vipya vya kupozea umeme katika sehemu mbalimbali za Dar es Salaam.
“Baadhi ya majengo makubwa Dar es Salaam yanahitaji umeme mwingi. Unakuta jengo moja kama haya maghorofa linahitaji megawati nyingi za umeme kuliko zinazotumiwa na baadhi ya mikoa,” alisema Mramba na kuongeza:
“Ndiyo maana tunatekeleza miradi mingi ya kuongeza uwezo wa njia za kusambaza umeme maana mfumo tulionao sasa ni chakavu na hauwezi kuhimili kiasi cha umeme kinachotakiwa na watumiaji wa makundi mbalimbali.”

Mramba alisema uchakavu wa miundombinu na mahitaji makubwa ya umeme ni miongoni mwa sababu za umeme kukatika ovyo na kwamba njia za kuusafirisha hazina uwezo wa kuhimili kiasi kinachotakiwa.
Ili kukabiliana na hali hiyo, alisema shirika lake linatekeleza miradi inayojumuisha ukarabati wa vituo vya kusambaza umeme ambao utahusisha vituo vikubwa na vidogo katika maeneo ya Mwananyamala, Jangwani Beach, Kigogo, Tegeta, Muhimbili, Luguruni, Mikocheni, Kurasini, Mbagala, Gongo la Mboto na Kipawa.
Mramba alisema Kituo cha Gongo la Mboto kitahudumia wakazi wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani, Segerea na Kinyerezi na katika Kituo cha Kipawa, Tanesco itaweka ‘saketi’ mbili kutoka Ubungo ili kutosheleza mahitaji ya viwandani na kusaidia kuwapo kwa umeme wakati wote endapo njia (line) moja itapata hitilafu.
“Njia (line) nyingine itaanzia kwenye Kituo cha Ilala, karibu na TBL kwenda katikati ya jiji mpaka Makumbusho na kurudi Ubungo. Mradi huu utakamilika Aprili, mwaka huu.

Pia utahusisha eneo la Mwenge, Tandale, Mikocheni, Masaki, Oysterbay ili wakazi wa maeneo hayo wapate umeme wa uhakika,” alisema.
Pamoja na vituo hivyo, Tanesco inajenga kituo cha kisasa eneo la Mikocheni, ambacho kitatumika kubaini maeneo yenye matatizo katika njia za usambazaji wa umeme... “Hivi sasa line (waya) ya umeme ikikatika, hatuwezi kujua tatizo liko wapi mpaka mafundi wetu wafuatilie na kufika katika eneo husika, lakini kituo hiki kitatuwezesha kutumia mfumo wa kompyuta kuonyesha eneo lenye kasoro.”
Habari zaidi soma Jarida la Uchumi ndani.
View detail

Wednesday, February 26, 2014

KUA WA KWANZA KUISHI KTK APARTMENT MPYA NA ZENYE UBORA TANZANIA

UAMUZI WA MUSEVENI WAZUA JAMBO MAREKANI

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Siku moja baada ya Rais Yoweri Museveni kusaini sheria inayotoa adhabu kali kwa wapenzi wa jinsi moja, Marekani imesema inaangalia upya uhusiano wake na nchi hiyo kama ilivyoainisha awali.
Katika taarifa yake iliyotolewa jijini Washington DC jana, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry alisema Serikali ya Rais Barack Obama itahakikisha ushirikiano wowote na Uganda utachujwa kupitia sheria za kupinga ubaguzi ambazo inazisimamia.
“Sheria imeshapitishwa, tunaanza kuchuja uhusiano wetu na Uganda kwa kuangalia mambo muhimu, ikiwemo maeneo tunayowawezesha,” alisema Kerry katika taarifa yake jana.
Awali, akitia saini muswada huo kuwa sheria juzi, Rais Museveni alipuuza vitisho vya Marekani na kusema mataifa ya nje ambayo yamekuwa yakimtaka asisaini muswada huo pamoja na viongozi wa kidini hawana nafasi katika mambo ya ndani ya nchi yake.
“Watu  kutoka nje hawawezi kutuamuru tufanye au tusifanye mambo yetu. Kama hawataki kwenda nasi, basi wanaweza kuchukua misaada yao,” alisema.
Akizungumzia onyo lililotolewa na baadhi ya viongozi wa kidini akiwemo Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini, Museveni alisema: “Kumbuka hata Yesu aliuawa na maaskofu, ndiyo maana huwa sisikilizi watu hao (viongozi wa kidini).”

Wakati Marekani na baadhi ya washirika wao wakitishia kuzuia misaada kwa Uganda, mataifa mengi ya Afrika, isipokuwa Afrika Kusini yana sheria kali za kupiga marufuku wapenzi wa jinsi moja. Sheria zimekuwa zikitekelezwa kwa muda mrefu sasa.
Shirika la Haki za Binadamu, Amnesty International linasema uhusiano wa kimapenzi wa watu wa jinsi moja umeharamishwa kisheria katika nchi 38 kati ya 54  barani humo  na adhabu ya kifo imehalalishwa nchini Mauritania, Sudan na Somalia.
Nchi zilizoweka sheria kali kuwabana wapenzi wa jinsi moja ni pamoja na Uganda ambayo imepiga marufuku wapenzi wa jinsi moja na  kutoa adhabu ya hadi kifungo cha maisha gerezani kwa wale wanaorudia vitendo hivyo.
Sheria hiyo inazuia kutangaza masuala yahusuyo wapenzi wa jinsi moja na kuwataka watu kuwatenga na kuwakataa mashoga.
Nigeria,  pia imeweka sheria maalumu iliyoanza kutekelezwa Januari mwaka huu. Sheria hiyo inatoa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 14 jela kwa wapenzi wa jinsi moja wanaoishi pamoja

Pia, inatoa kifungo cha hadi miaka 10 kwa kuonekana hadharani wakijiachia kama wapenzi.
Katika eneo la Kaskazini linalotawaliwa chini ya sheria za Kiislamu, wapenzi hao wanakabiliwa na adhabu ya kifo.
Cameroon ni miongoni mwa nchi zenye sheria za aina hiyo, ambapo wapenzi wa jinsi moja wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka mitano jela.
Gambia imekuwa na mfumo wa sheria dhidi ya wapenzi wa jinsi moja wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 14 jela na kazi ngumu.
Nchini Zambia pia, wapenzi wa jinsi moja walipigwa marufuku tangu enzi za utawala  wa  Waingereza na waliobainika, walikabiliwa na kifungo cha hadi miaka 14 jela.
Kwa upande wa Senegal, yeyote atakayetiwa hatiani kwa kujihusisha na kitendo chochote kisichokuwa cha asili na mtu wa jinsi yake anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela.
Nchini  Tunisia, vitendo vya  uhusiano ya wapenzi wa jinsi moja kwa watu wazima hukabiliwa na adhabu ya hadi miaka mitatu jela.
Nako Morocco, wenye tabia hiyo hukabiliwa na kifungo cha kuanzia miezi sita hadi miaka mitatu jela.
Kule Algeria, yeyote anayetiwa hatiani kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsi moja anakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela, lakini wengi huweza kushikiliwa kwa muda usiojulikana.
Nchini Zimbabwe, Rais Robert Mugabe amekuwa akisisitiza kwamba wapenzi wa jinsi moja ni wabaya kuliko nguruwe na mbwa.
Hata hivyo, inadaiwa kwamba makundi ya watu wa aina hiyo yanaruhusiwa katika baadhi ya maeneo.
Nako Malawi, Novemba mwaka 2012, Rais Joyce Banda alizuia sheria za kupiga marufuku wapenzi wa jinsi moja hadi zitakapojadiliwa bungeni. Kwa sheria iliyopo, wanaume wanakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 14 jela na wanawake hadi miaka mitano jela.

Nchi nyingine zikiwamo Chad, Gabon, Ivory Coast na Mali hazijapiga marufuku, lakini Afrika Kusini iliruhusu ndoa za jinsi moja mwaka 2006.
Pamoja na hatua hiyo, wapenzi wa jinsi moja wamekuwa wakidhibitiwa ipasavyo kwa kuadhibiwa iwe wanaume au wanawake ili kuwarejesha kwenye mfumo wa kawaida.

Jarida moja nchini Uganda limechapisha orodha ya majina na watu 200 liliowataja kuwa wapenzi wa jinsia moja, siku moja baada ya Rais Yoweri Museveni kutia saini sheria inayowabana watu wa namna hiyo.
Jarida hilo lililopewa jina la Red Pepper lilichapisha majina hayo jana pamoja na picha za wahusika katika ukurasa wake wa mbele, chini ya kichwa cha habari: “WAANIKWA!”
Orodha hiyo inajumuisha wanaharakati maarufu wa haki za mashoga wa Uganda, akiwemo Pepe Julian Onziema ambaye mara kadhaa alionya kwamba sheria hiyo ya kuwabana wapenzi wa jinsi moja itaibua machafuko. Msemaji wa Polisi wa Uganda, Patrick Onyango alisema hata hivyo hakuna wahusika waliokamatwa tangu Rais Museveni alipotia saini sheria hiyo juzi, lakini tayari hakuna msalie mtume kwa wale watakaotiwa nguvuni.

Akitia saini muswada huo kwenye Ikulu ya Eenrebbe mbele ya wanahabari na maofisa wa juu wa Serikali yake juzi, Museveni mbele ya maofiosa wa juu wa Serikali yake na waandishi wa habari, alisema adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wale watakaopatikana na hatia kwa mara ya kwanza haiepukiki. Pia, adhabu ya maisha jela itatolewa kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja zaidi ya mara moja kati ya watu wawili waliokubaliana kufanya hivyo.
Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi.
View detail

Tuesday, February 25, 2014

MTANZANIA MMOJA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KETE 71

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Polisi Kikosi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wamemkamata mkazi wa Temeke, Mwanahamisi Salim (27) kwa tuhuma za kumeza kete 71 za dawa za kulevya aina ya heroini zenye thamani ya zaidi ya Sh60 milioni.
Mkuu wa Upelelezi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Hamad Hamad alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa alasiri ya Februari 20, mwaka huu akijiandaa kupanda Ndege ya Shirika la Emirates kwenda Hong Kong, China.
“Tulipomhoji alitueleza kuwa dawa hizo alikuwa anazipeleka kwa marafiki zake kutoka Nigeria ambao wanaishi Hong Kong lakini bado tunaendelea kumhoji ametoa wapi huo mzigo,” alisema Hamad.
Alisema katika siku za karibuni, wamebaini kuwa watuhumiwa wengi wanaokamatwa ni wanawake.
Alisema wengi wa wanawake hao wanadai wanakwenda kununua vifaa vya saluni.
Kamanda wa Polisi, Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Godfrey Nzowa alisema dawa zilizokamatwa ni heroini.

Katika hatua nyingine; taswira ya Tanzania imeendelea kuchafuka baada ya Kituo cha Kimataifa cha Televisheni cha France 24 kutoa ripoti inayoonyesha ukubwa wa tatizo la dawa za kulevya nchini.
Ripoti hiyo inakuja zikiwa zimepita wiki mbili tangu Gazeti la The Mail on Sunday kuandika habari za kukithiri kwa ujangili wa meno ya tembo na pembe za faru.
Taarifa ya kituo hicho ilieleza kuwa Tanzania inaonekana kuwa kituo cha dawa za kulevya kutoka Afghanistan na Pakistan.
Mmoja wa waandishi walioandaa ripoti hiyo, Jaouhar Nadi alisema tatizo la dawa za kulevya Tanzania ni kubwa na hakuna mikakati ya makusudi ya kupambana nalo.
“Zanzibar kwa mfano, kuna watumiaji 10,000 wa dawa za kulevya, yaani katika kila familia moja kuna mteja mmoja. Kuna ‘mateja’ wapatao 250,000 nchi nzima na jitihada za Serikali zinaonekana kuwa dhaifu,” alisema Nadi alipokuwa akihojiwa na France 24 na kuongeza: “Zanzibar kwa mfano, hakuna programu yoyote ya Serikali zaidi ya ile iliyoanzishwa na taasisi ya Kimarekani.”

Nadi alisema licha ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuanzisha Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, bado uingizwaji wa dawa hizo umekithiri.
“Mamlaka zinashughulikia suala hilo, walianzisha tume miaka ya 1990. Hata hivyo, usafirishaji wa dawa za kulevya bado ni mkubwa,” alisema na kuongeza:
“Inakadiriwa kuwa biashara hiyo huingiza zaidi ya Dola 165 milioni na tani 22 za heroini huingizwa nchini humo kila mwaka. Hizo ni fedha nyingi na watu wanaamini kuna rushwa hasa kwa viongozi wa juu na wabunge.
“Majina ya wakubwa wanaohusika na biashara hiyo yanafichwa. Wengi wanaamini ni kazi ya wafanyabiashara wakubwa wa dawa hizo.”

Akizungumzia madai hayo Kamanda Nzowa alipinga utafiti huo na kusema jitihada kubwa zimefanyika... “Kama ni kweli kuna tatizo kubwa kiasi hicho, hao waandishi walipaswa watuambie dawa hizo zinauzwa bei gani, kwa sababu ninavyojua ni kwamba, huko mitaani dawa zinauzwa bei ghali mno. Kilo moja inafikia hadi Sh50 milioni, sasa utasemaje kwamba matumizi ya dawa yameongezeka?”
“Ni kweli tatizo la dawa za kulevya lipo, pia ukamataji ni mkubwa. Kwa mfano, mwaka jana tu tumekamata kilo 1,882 za heroini. Februari 4, mwaka huu tumekamata kilo 201 na wenzetu wanaodhibiti baharini wamekamata kilo 350 za dawa hizo. Hiyo pekee inajenga hofu kwa waingizaji. Itakuwaje waendelee kuleta?”
Alisema majina ya watu wanaohisiwa yamekuwa yakifanyiwa kazi ikiwa pamoja na kuwafikisha mahakamani... “Mwaka jana kuna gazeti moja la Kiswahili lilifanya utafiti na mimi pia nilizungumza nao. Baada ya hapo tulikamata watu 266. Baada ya kuwapekua hatukuwakuta na ushahidi, lakini bado tuliwafikisha mahakamani kwa kuwa walikuwa na dalili za kuhusika,” alisema na kuongeza:
“Tunapata taarifa mbalimbali na tunawashukuru wananchi, lakini wanapaswa watupe kwa siri siyo kutangaza hadi wahusika washtuke. Hii ni vita ya dunia nzima, siyo Tanzania tu.”
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Zanzibar, Mohamed Aboud alisema hana taarifa za kutosha kuhusu utafiti huo, lakini hali siyo mbaya kiasi hicho.
“Ni kweli kuna tatizo la dawa za kulevya hapa Zanzibar na watu wengi wameathirika, lakini sidhani kama ni kwa kiasi kikubwa hivyo. Bado tunafuatilia utafiti huo ili kujiridhisha na kutoa taarifa rasmi,” alisema Aboud.
View detail

Monday, February 24, 2014

PATA MUDA WA MAONGEZI WA 10,000 BURE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU


http://azizicompdoc.blogspot.com/ 
Kutokana na kujua umuhimu wa wadau wetu, Tunatarijia kufikisha wasomaji 50,000 ambayo ni kihesabio cha waliotembelea blog hii ambacho ni tofauti na wale wanaoweka kihesabio cha uongo ili waonekane wametembelewa na watu wengi kwa kipindi kifupi wakati si kweli . Tunakuomba uingie ktk blog yetu, upande wa kulia juu utaona meneno WALIOTEMBELEA BLOG HII, kwa chini utaona idadi ya watu waliotembalea, atakaeweza kuipiga picha 50,000  na kusajili Email yake pale palipoandikwa andika email yako uhabarike kila siku na kututumia kwa Email: mnyengema@gmail.com picha hiyo , atazawadiwa muda  wa maongezi wa 10,000. na kama yuko dar utazawadiwa na mafunzo mafupi (training) ya Web2.0 ya siku 2 bure wahi sasa wanaoshindania ni wengi

View detail

SAKATA LA MJUMBE FEKI BUNGE LA KATIBA LACHUKUA SURA MPYA

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Ofisi ya Bunge la Katiba, imemwandikia barua mwajiri wa Amina Mweta, ambaye alisaini posho ya Bunge hilo ili akatwe posho aliyoichukua katika mshahara wake.
Akizungumza na Blog hii jana katika Ofisi za Bunge mjini hapa, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk Thomas Kashililah, alisema Bunge limechukua hatua hiyo baada ya Mweta kuwajibu kuwa fedha walizompatia alikuwa ameshazitumia.
“Yeye (Amina Mweta), ni mwajiriwa wa Halmashauri ya Mwanga, tulichokifanya ni kumwandikia barua mwajiri wake ili akatwe katika mshahara wake,” alisema na kuongeza: “Atajua mwenyewe kama atalipa kwa kukatwa kidogo kidogo ama yote, lakini lazima ailipe posho hiyo aliyoichukua, kwa sababu alichukua na kuweka sahihi.”
Blog hii lilikuwa la kwanza kuripoti baada ya kutokea utata huo wa majina mawili ya wajumbe kufanana huku ikielezwa kuwa wote walikuwa wamesaini fomu za fedha za posho ya kujikimu ya Sh80,000 kwa siku kwa muda wa siku 13 unaomalizika Februari 28 mwaka huu ikiwa na maana kwamba kila mmoja alilipwa Sh1,040,000.
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel, awali, alipoulizwa kuhusu utata huo alisema mjumbe halali ni yule aliyetoka Songea.
Hata hivyo, alisema kinachowashangaza ni kwamba yule mwenzake wa Mwanga alipotakiwa kurudisha fedha alizopewa kimakosa alisema ameshatumia sehemu kubwa na kubakiza Sh50,000 tu.
Akizungumza na Blog hii, Mweta kutoka Mwanga alisema alipigiwa simu na Ofisi ya Bunge Maalumu la Katiba na kupongezwa kwa kuteuliwa na Rais kuwa mjumbe. “Mimi ni personal secretary (katibu muhtasi) wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na nilipigiwa simu na Ofisi ya Bunge wiki iliyopita nikipongezwa kwa uteuzi huo,” alisema.
Alisema alipofika na kujisajili baada ya kutoa kitambulisho chenye jina lake, alipewa kitambulisho na kisha kupewa malipo yake ya posho.
Naye Mweta kutoka Songea alisema alipigiwa simu na Katibu Mkuu wa COTWU kwamba aliteuliwa na Rais kuwa mjumbe na kutakiwa kuripoti bungeni.
Tayari Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limeeleza kusikitishwa na utata wa watu hao wawili wenye majina yanayofanana kuwasili katika Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma kwa nafasi ya ujumbe wa Bunge hilo, huku likisema halimfahamu Amina Mweta wa Kilimanjaro.
Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya mapema alikaririwa na Blog hii akisema kuwa mazingira ya tukio hilo yamewatisha, hivyo kulazimika kumwandikia barua Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ili kumthibitisha mjumbe wao halali.
View detail

MAJAMBAZI WANNE WAUAWA ARUSHA


LiberatusSabas
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas.
Watu wanne ambao bado hawajafahamika wanaume wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 35 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa baada ya kupigwa risasi na askari Polisi. Tukio hilo lilitokea jana tarehe 21.02.2014 muda wa saa 1:00 jioni katika bar moja iitwayo Pama iliyopo maeneo ya Makao Mapya jijini hapa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba, tukio hilo lilitokea mara baada ya jeshi la polisi Mkoani hapa kupata taarifa toka kwa raia wema kwamba watu hao walikuwa wanapanga kwenda kufanya tukio la uhalifu katika kituo kimojawapo cha kuuzia mafuta kilichopo jijini hapa ambapo ufuatiliaji wa taarifa hiyo ulianza.

Ilipofika muda huo askari hao walikwenda katika bar hiyo na mara baada ya majambazi hao kuwaona askari hao walihisi wanafuatiliwa ndipo mmojawao ghafla alitoa bastola  na kufyatua risasi tatu ambapo moja ilimparaza askari mmoja aitwaye F. 1416 D/Ssgt Richard katika mkono wake wa kushoto
 “Kufuatia hali hiyo askari nao waliamua kujibu mapigo kwa kupiga risasi ambapo wanne kati ya watano walijeruhiwa na mmojawao alifanikiwa kukimbia akiwa na silaha inayosadikiwa kuwa ni SMG”. Alisema Kamanda Sabas.
Kamanda Sabas alisema kwamba, majambazi hao walifariki dunia wakiwa njiani kuelekea hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya matibabu na miili yao imehifadhiwa hospitalini hapo kwa ajili ya utambuzi toka kwa ndugu na jamaa wa karibu.

Aidha Kamanda Sabas alisema, katika eneo la tukio askari hao walipata bastola moja aina ya Star yenye namba 42640 FNH PISTOLE MODEL KAL 7.65 ikiwa na risasi tatu katika magazine, maganda matatu ya risasi pamoja na begi moja dogo la mgongoni lenye rangi nyekundu likiwa na risasi nne hivyo kufanya jumla ya risasi saba kupatikana.
Bado Jeshi la Polisi Mkoani hapa linaendelea na upelelezi kuhusiana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kumtafuta mtuhumiwa mmoja aliyekimbia.
Kufuatia tukio hilo Kamanda Sabas aliendelea kuwashukuru wananchi wa Arusha kwa ushirikiano wao mkubwa wanaoutoa kwa jeshi la Polisi Mkoani hapa na kuwasihi waendelee kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu hali itakayosaidia kukomesha matukio ya uhalifu mkoani hapa.
 Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
View detail

HARAMBEE YA UJENZI WA WODI YA DHARULA YA WATOTO MUHIMBILI

p6
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa baada ya kuwasili katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p23
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo  na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa katika hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p24
Mkurugenzi wa Radio One Bw. Deo Rweyunga akitangaza mchango wa makampuni ya IPP ya kununua kifaa cha thamani ya dola elfu 50 katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p25
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru mwakilishi wa UNICEF nchini kwa mchango wa dola za kimarekani 100,000 huku  Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjmin William Mkapa wakishuhudia katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p30
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru mwakilishi wa NSSF Bw. Juma Kintu kwa mchango wa mfuko huo katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p32
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 10 toka kwa wawakilishi wa PPF ukiwa   mchango wa mfuko huo katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p37
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Bi  Lucy Kimei kwa kuwasilisha shilingi milioni tatu kama mchango wa familia ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt Charles Kimei   katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p48
Rais mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa  akimshukuru mwakilishi wa taasisi ya WAMA Bi. Caroline Mthapula  kwa mchango wa taasisi hiyo  katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.
p49
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Bw. Lumbila Fyataga, mwakilishi wa Ofisi ya Rais, Ikulu,  kwa mchango wa kununua kifaa cha kuwapa joto watoto wachanga (Infant radiation warmer)  katika  hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa wodi ya dharura kwa watoto pamoja na vifaa vyake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kati ya kiasi cha shilingi 1bn/ zilizohitajika, jumla ya shilingi 602,080,000/- zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika usiku wa Jumamosi Fabruari 22, 2014 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es salaam.(Picha na IKULU).
 
 
View detail

SUALA LA POSHO BUNGE LA KATIBA LACHUKUA SURA MPYA

 ONGEZEKO LA POSHO LIMEKWAMA;Binafsi namshukuru sana mungu!Taarifa rasmi ambazo nimezithibitisha kutoka katika vyanzo muhimu na vya kuaminika vya bunge, serikali na wadau wengine zinathibitisha kuwa ishu ya ongezeko la posho imekwama na KUFA KIFO CHA MENDE.Hii ina maanisha kwamba wajumbe wa bunge maalum la katiba watalipwa shs 300,000 tu kwa siku kama ilivyokuwa hapo awali.Narudia tena kwamba jambo hili limekwama na halitakuwepo.Leo saa 2.00 asubuhi nilipanga kuanzisha zoezi la kukusanya SAINI za wajumbe wote wanaopinga ongezeko la posho, ni kazi ambayo ingenigharimu siku tatu kuisimamia.Natangaza rasmi kusitisha zoezi la kukusanya saini kwa sababu ULAFI huu wa posho uliopendekezwa na baadhi ya wabunge wa CCM umekatishwa kwa maslahi ya umma.Nawaomba watanzania wote kuelekeza mijadala yetu kwenye rasimu ya katiba na tuondoke kwenye suala la posho ambalo limefika mwisho.Nataraji leo, Mwenyekiti wa muda wa bunge maalum atathibitisha kuwa hakuna ongezeko la posho.Nawashukuru sana Wabunge na Wawakilishi wa Chama cha Wananchi CUF ambao walinitia moyo na kuchangia gharama za mabango maalum yenye picha za kuonesha mateso ya kina mama wanapojifungua, na lile la kuonesha watoto wa shule walivyokaa juu ya mavumbi(ambayo yangetumika katika zoezi hili).Namshukuru sana Prof. Ibrahim Lipumba na Zitto Kabwe kwa kuniunga mkono katikati ya jambo hili. Nawashukuru baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba ambao walikuwa tayari kusaini PETITION leo hii na waliopinga ULAFI huu.Mungu ibariki Tanzania.
Taarifa rasmi ambazo nimezithibitisha kutoka katika vyanzo muhimu na vya kuaminika vya bunge, serikali na wadau wengine zinathibitisha kuwa ishu ya ongezeko la posho imekwama na KUFA KIFO CHA MENDE.
Hii ina maanisha kwamba wajumbe wa bunge maalum la katiba watalipwa shs 300,000 tu kwa siku kama ilivyokuwa hapo awali.
Narudia tena kwamba jambo hili limekwama na halitakuwepo.

Leo saa 2.00 asubuhi nilipanga kuanzisha zoezi la kukusanya SAINI za wajumbe wote wanaopinga ongezeko la posho, ni kazi ambayo ingenigharimu siku tatu kuisimamia.
Natangaza rasmi kusitisha zoezi la kukusanya saini kwa sababu ULAFI huu wa posho uliopendekezwa na baadhi ya wabunge wa CCM umekatishwa kwa maslahi ya umma.
Nawaomba watanzania wote kuelekeza mijadala yetu kwenye rasimu ya katiba na tuondoke kwenye suala la posho ambalo limefika mwisho.

Nataraji leo, Mwenyekiti wa muda wa bunge maalum atathibitisha kuwa hakuna ongezeko la posho.
Nawashukuru sana Wabunge na Wawakilishi wa Chama cha Wananchi CUF ambao walinitia moyo na kuchangia gharama za mabango maalum yenye picha za kuonesha mateso ya kina mama wanapojifungua, na lile la kuonesha watoto wa shule walivyokaa juu ya mavumbi(ambayo yangetumika katika zoezi hili).
Namshukuru sana Prof. Ibrahim Lipumba na Zitto Kabwe kwa kuniunga mkono katikati ya jambo hili. Nawashukuru baadhi ya wajumbe wa bunge la katiba ambao walikuwa tayari kusaini PETITION leo hii na waliopinga ULAFI huu.
Mungu ibariki Tanzania.



View detail

Friday, February 21, 2014

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013 HAYA HAPA

http://azizicompdoc.blogspot.com/
 Matokeo ya kidato cha nne ambayo yalikua yanasubiriwa kwa hamu kubwa na wazazi pamoja na watoto wao ambao ni watahiniwa wa mtihani huo leo yametoka rasmi na kumfanya kila mmoja kufarijika au kuhuzunika kutokana na uhalisia wa matokeo. Kutokana na umuhimu huo mkubwa wa suala hili tumeamua kukuwekea rasmi matokeo hayo ktk Blog yako pendwa na yenye kukujali mwananchi wa kawaida.
Bofya hapa kuona matokeo ya Kidato cha nne 2013 View detail

PADRE AFIA NYUMBA YA KULALA WAGENI, MCHUNGAJI AFIA NYUMBANI KWA MSHIRIKA WAKE

Mchungaji Geoffrey Maingi wa Kanisa la Redeemed Gospel aliyefia nyumbani kwa mshirika wake
Kiongozi wa Kanisa amekutwa akiwa amefariki dunia kwenye nyumba ya kulala wageni jijini Nairobi na kufanya vifo vya kutatanisha vya viongozi wa kidini kufikia wawili wiki hii.
Katika tukio la juzi, Padri wa Kanisa Katoliki, Otto Myer (70) ambaye ni raia wa Italia, alikutwa akiwa amefariki saa tano usiku chumbani mwake kwenye nyumba ya kulala wageni ya the Consolata huko Westlands, Nairobi.
Mwili wa padri huyo ulipatikana kwenye chumba hicho kando yake kukiwa na dawa, na baadhi ya jirani zake walisema alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mfupi.
Juzi, Mkuu wa Polisi Jimbo la Nairobi, Benson Kibue alisema maofisa wake wanachukulia kifo chake kuwa cha ghafla, hasa kutokana na kwamba amekuwa akiugua kwa siku kadhaa.
“Hatutaharakisha kusema kilichomuua. Kwa sasa tunajua hiki ni kifo cha ghafla, ikizingatiwa kuwa amekuwa akiugua. Upasuaji wa maiti ndio utakaoeleza zaidi kilichomfanya afariki,” akasema Kibue.
Lakini maofisa wa polisi waliofika mahali hapo pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa gesti hiyo ambao hawakutaka kutajwa, walisema kwamba chumbani alimokufa padri huyo mlikuwa na dawa pamoja na pombe.
Wakizungumza na waandishi wetu, walisema kwamba padri huyo alikuwa ameenda katika hospitali ya karibu kutafuta tiba siku ya Jumanne.

Kifo cha Padri Myer kilitokea saa chache baada ya kifo cha mchungaji Geoffrey Maingi wa Kanisa la Redeemed Gospel nyumbani kwa mmoja wa washirika wake katika Mtaa wa Buruburu, Nairobi.
Sawa na Padri Myer, Kasisi Maingi pia alikuwa na umri wa miaka 70 na pia alifariki dunia kwenye vyumba katika hali ya kutatanisha.
Kwenye kisa cha Buruburu, Kasisi Maingi  alisemekana kuegesha gari lake nje ya duka la jumla la Tuskys na kwenda nyumbani kwa mwanamke mshirika wa Kanisa lake, ambaye alikiri kuwa mbali na kuwa kiongozi wake wa kiroho, yeye pia alikuwa rafiki yake.
Mwanamke huyo alisema kuwa mchungaji huyo alikuwa nyumbani kwake kwa maombi. Tukio hilo lilishuhudiwa katika mtaa wa Buruburu mjini Nairobi Kenya.
Mwili wa Maingi, ulikutwa ndani ya chumba cha mwanamke huyo, baada ya kufariki kutokana na sababu ambazo hazijulikani.
View detail

WhatsApp KUUZWA IKIWA NA WATUMIAJI WAKE WOTE DUNIANI

http://azizicompdoc.blogspot.com/
Facebook na WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana.
Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook imesema kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa kima cha dola bilioni kumi na sita, na nyongeza zaidi ya dola bilioni tatu zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na wafanyikazi wake.
Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa.
WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS.

WhatsAp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji milioni mia nne hamsini.
Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo litafanya Facebook kuwa na thamani kubwa.
View detail

WADAU WA TEHAMA WAFANYA MKUTANO DAR


02 SAYANSIMtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) Dkt. Jabir Kuwe Bakari akitoa mada kuhusu matumizi ya “Broadband” katika shughuli za Serikali wakati wa mkutanao wa wadau wa Tehama nchini katika ukumbi wa NSSF Waterfront leo jijini Dar es salaam.01 SAYANSI

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. John Mngodo akiogea na wadau wa Tehama wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau hao leo jijini Dar es salaam. 





06 SAYANSI

Mkuu wa kitengo cha cha ICT Broadband cha Taifa-TTCL Adin Mgendi  akitoa mada juu ya Wakati ujao tunaotaka kuuona wakati wa mkutanao wa wadau wa Tehama nchini leo katika ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es salaam na kubainisha kuwa TTCL imepanua wigo wa kutoa huduma ya mtandao wa mawsiliano(internet) ndani na nje ya nchi, katika nchi jirani zinazonufaika na huduma hiyo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi na Zambia. 

05 SAYANSI

Kaimu Mkurugenzi wa ICT Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ally Simba (kulia) akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutanao wa wadau wa Tehama nchini katika ukumbi wa NSSF Waterfront leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Smile Communication Tanzania Ltd Mark Redman, na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Operesheni Mfuko wa Huduma za Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Albert Richard.

07 SAYANSI

Baadhi  ya wadau wa Tehama  nchini wakifuatilia na kumsikiliza Mgeni rasmi  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. John Mngodo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau hao leo jijini Dar es salaam.

04 SAYANSI

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. John Mngodo akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano na wadau wa Tehama nchini leo jijini Da es salaam.(Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO)
View detail

Thursday, February 20, 2014

MUSEVEN APIGA MARUFUKU UVAAJI WA VIMINI NA MAZIWA NJE!

 
http://azizicompdoc.blogspot.com/
Kwasasa Uganda, imekua nchi ya kuigwa kwa jambo jema, nchi hiyo imepiga marufuku Vazi la “KIMINI” yani Nguo Fupi kwa wanawake wote nchini humo.
Taarifa hiyo imetoka mara baada ya Rais Yoweri Museveni, kusaini mswada huo na kuwa sheria ya nchi, inadaiwa kuwa kuzuia mavazi hayo kutasaidia sana kupunguza vitendo vya Ubaki na Ngono zembe kutoka na ushawishi wa mavazi hayo kwa jamii.
 
Hii kitu ya kutovaa nguo fupi na zile za kuonesha maziwa nje, inaonekana kuwabana wasanii wa kike moja kwa moja, maana wengi wao ndio kichocheo kikubwa kwa jamii. Waziri alifunguka na kusema kuwa   “hatutaki uhusike kufanya watu wakutamani au watamani kufanya ngono, hatutaki ushawishi chochote kwa jinsia ya kiume, kuwa na tabia njema kwa kuvaa kiheshima”.
 
Pia vyombo vya habari vya Uganda vimekatazwa kuonesha watu wakipigana mabusu sambamba na wanawake kuvaa hayo mavazi katika vipind View detail

MTU NA MKEWE WAZUA BALAA BUNGE LA KATIBA

http://azizicompdoc.blogspot.com/

Chama cha National League for Democracy (NLD) Zanzibar kimemtaka, Rais Jakaya Kikwete kufuta uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupitia chama hicho kwa madai kuwa walioteuliwa katika chama hicho ni mtu na mkewe na kufanya uteuzi huo kukosa sura ya Muungano.
Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa NLD - Zanzibar, Khamis Haji Mussa katika taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari mjini hapa juzi, kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Dk Emmanuel Makaidi amewasilisha majina mawili, la kwake na la mkewe, Modesta Ponera kwa ajili ya uteuzi.
Alisema NLD - Zanzibar kilianza kufuatilia taratibu za uwasilishaji wa barua tangu Desemba 27, mwaka jana kwa kumwandikia barua Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ baada ya kupokea maelekezo ya Ikulu ya Tanzania kwamba majina ya Zanzibar yatafanyiwa kazi visiwani na ya Bara yangepelekwa Ikulu Dar es Salaam.
Alisema kwa mujibu wa utaratibu huo, vyama vyote vyenye usajili wa kudumu vilitakiwa kila kimoja kutoa mtu mmoja kutoka Tanzania Bara na mwingine Zanzibar ili kuwa na sura ya kitaifa, lakini Dk Makaidi alikiuka utaratibu huo.
 
Akizungumzia tuhuma hizo, Dk Makaidi alikiri kuwa Ponela ni mke wake, lakini akasema ni mwanachama wa NLD, hivyo ana haki ya kuteuliwa.
Alisema alipeleka majina manne Ikulu na kwamba upande wa Zanzibar ulitakiwa kufanya hivyo kupitia Ikulu ya Zanzibar... “Walifanya uzembe, hawakupeleka majina ya wanachama wa NLD, matokeo yake nikapeleka majina manne, tukapata uwakilishi.”
 Alisema mkewe ni mwanachama wa NLD hivyo ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi yoyote kulingana na sifa zake... “Wanalalamika nini hata chama tawala cha CCM, Rais Jakaya Kikwete ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mkewe Salma pia ni mjumbe wa Nec.”
Alisema Ponela kuwa mkewe hakumfanyi akose haki zake za msingi na kwamba sifa zake na elimu ndivyo vilivyomfanya Rais amteue.
Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Florens Turuka alipoulizwa alisema Ikulu haina taarifa za suala hilo lakini wanaamini vyama vya siasa vilikaa na kupendekeza majina manne na kuyawasilisha Ikulu, ndipo Rais alipoteua wajumbe mawili kati yake.

Siku mbili baada ya kuanza kwa Bunge hilo, baadhi ya wajumbe wametaka waongewe posho kwa maelezo kuwa kiasi wanachopewa sasa cha Sh300,000 kwa siku hakiwatoshi kutokana na kupanda kwa gharama za maisha Dodoma.
Wajumbe hao walitoa kauli hiyo jana katika kikao cha kuwasilisha na kujadili rasimu ya kanuni za Bunge hilo ambacho kilianza saa nne asubuhi.Kwa kiasi kikubwa, kikao hicho ambacho awali waandishi wa habari walizuiwa kuingia, kilitawaliwa na hoja ya kuongezwa kwa posho za wajumbe na kuungwa mkono na wajumbe wengi bila kufuata utaratibu maalumu uliokuwa ukisisitizwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho.
“Wajumbe wengi walikuwa wakisimama na kutaka kuzungumza bila kufuata utaratibu maalumu. Jambo hilo liligeuza ukumbi wa Bunge kuwa kama soko,” kilisema chanzo chetu. Baadhi ya wajumbe waliopata nafasi ya kuzungumzia nyongeza ya posho hizo ni Mbunge wa Kishapu (CCM), Suleiman Nchambi na Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa.
Katika ufafanuzi wake kwa waandishi wa habari, baada ya kikao hicho kuahirishwa kwa muda, Ndassa alisema: “Bunge ndiyo linalotengeneza Katiba ya nchi. Nasikitika kuwa kiwango cha fedha ambacho tunalipwa ni kidogo na hakitoshi kwa sababu kuishi katika Mji wa Dodoma ni gharama kubwa.”
Ndassa alisema kati ya Sh300,000 wanazolipwa wajumbe hao, posho ya kikao ni Sh220, 000 na 80,000 ya kujikimu na kwamba kiasi hicho hakitoshi.
“Mfano ni siku ya Jumamosi na Jumapili. Katika siku hizo mbili wajumbe wote hawalipwi Sh220,000 za posho za kikao na wakati huohuo wanatakiwa kuwalipa madereva wao, kununua mafuta ya gari, chakula na malazi,” alisema.
Aidha, alisema kitendo cha wajumbe kutakiwa kulipwa Sh220, 000 baada ya kusaini katika kitabu cha mahudhurio mara mbili kwa siku ni sawa na udhalilishaji.
“Nilimweleza mheshimiwa mwenyekiti kwamba wajumbe tupo 600 na kulingana na hali halisi wote hatuwezi kuhudhuria kikao kila siku, zipo siku ambazo baadhi yetu wanakuwa na shughuli nyingine na wapo watakaougua, sasa na hao wasilipwe Sh220,000 kweli?” alihoji.
Alisema Serikali inatakiwa kulitazama suala hilo kwa kina kwa maelezo kuwa linaweza kuibua mvutano unaoweza kusababisha wajumbe hao kushindwa kuijadili Rasimu ya Katiba kama inavyotarajiwa na wengi.
“Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba walikuwa wakilipwa Sh500,00 kwa siku, lakini wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanalipwa Sh220,000 tena mpaka wahudhurie kikao. Hii siyo sawa kabisa,” alisema.
Alisema madereva wa Tume hiyo ya Katiba walikuwa wakilipwa Sh220,000 kwa siku... “Posho yangu ni sawa na aliyokuwa akilipwa dereva wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Sielewi kabisa maana hata viwango vyetu vya posho ni tofauti na wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar, wao wameongezewa posho.”
Alisema jambo hilo litaibua ubaguzi kwa sababu wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wanaweza kuwasilisha malalamiko yao kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda na kuongezewa posho lakini wajumbe 201 walioteuliwa na Rais hawana mahali pa kulalamika ili kuongezewa posho.
Pamoja na Ndassa kutotaka kuweka wazi, kumekuwa na madai kuwa wajumbe kutoka Zanzibar wameongezewa Sh120,000 na Baraza la Wawakilishi, hivyo kuwafanya kupata Sh420,000 kwa siku.

Hata hivyo, Katibu wa Baraza hilo, Yahya Khamis Hamad alikana madai hayo akisema hakuna fedha za ziada walizolipwa.
Alisema malipo waliyosaini wakiwa Dodoma yaliyotokana na kuhudhuria vikao vya Kamati za Baraza, lakini si nyongeza ya posho.
Akizungumzia suala hilo Nchambi alisema: “Sisi tumeshazoea maisha ya Dodoma na tunaishi hivyohivyo tu licha ya kuwa fedha ni ndogo. Ila hawa wenzetu ambao ni wageni hali zao ni mbaya.
“Wajumbe wapo hapa kwa ajili ya kutengeneza moyo wa nchi yao na wakati tunakuja hapa Dodoma tulielezwa wazi kuwa tusiende kuishi katika nyumba za wageni za vichochoroni. Sasa kwa mantiki hiyo hiki kiwango cha fedha tunacholipwa kitatosha kweli?
“Hapa bungeni wapo maprofesa walioacha kazi zao zinazowaingizia fedha nyingi na kuja kuandika Katiba. Kitendo cha kuwalipa fedha kidogo kinaweza kuwakatisha tamaa.”
Kificho alihitimisha mjadala huo kwa kusema suala hilo la posho litawasilishwa serikalini kuona namna ya kulifanyia kazi.
Baada ya wabunge kutoka kwenye mjadala huo, Mjumbe, Kabwe Zitto alisema anasikitika kwamba tangu siku ya kwanza, suala la posho linashika kasi... “Kiukweli inavunja moyo sana… Ni dhahiri wajumbe lazima walipwe lakini malipo ya posho ndiyo kipaumbele kweli?”
View detail

KAULI YA RAIS KIKWETE KUHUSU USHOGA


Akihojiwa  na CNN nchini Uingereza hivikaribuni wakati akihudhuria mkutano uliolenga kuongeza mapambano dhidi ya
ujangili, Rais Jakaya Kikwete amepigilia msumari wa moto akisema Tanzania haiko tayari kukubaliana na matakwa ya baadhi ya nchi za magharibi zinazotaka nchi za Afrika ziwe na sheria zinazoruhusu ushoga.

"Itachukua muda kwa watu wetu kukubaliana na tamaduni za watu wa magharibi, nakumbuka Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron aliwahi kuzungumza sana kuhusu suala hilo na likaleta shida na tafrani kubwa kwa watu wetu," alisema.

"nafikiri kwa watu wetu sidhani kama huu ni muda muafaka wa kujadili suala hilo,hatulitaki na halikubaliki" alisema alipokuwa akihojiwa na mtangazaji wa CNN, Christiane Amanpour.

Amannpour alitaka kujua msimamo wa Rais Kikwete kuhusu haki za mashoga na harakati zinazofanywa ili kuufaya ushoga kama moja ya haki za msingi za binadamu.
View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop