Takriban watu 55 wanaaminika kuzama majini baada ya meli walimokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya Somalia.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR, limethibitisha tukio hilo.Shirika hilo la UNHCR, limesema meli hiyo ilikuwa imebeba kupita kiasi wakati ilipopigwa na dhoruba muda mfupi baada ya kuondoka kutoka bandari ya Bossasso, Kaskazini Mashariki mwa Somalia.
Meli hiyo inaaminika kuwa ilikuwa inaelekea Yemen na ilikuwa imebeba wahamiaji haramu kutoka Ethiopia na Yemen.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa ajali hiyo ndiyo mbaya zaidi katika Guba ya Aden tangu Februari mwaka wa 2011 wakati wahamiaji haramu 57 kutoka Somalia walipozama baharini.
0 comments:
Post a Comment