Welcome to our online store Portal

Template Information

Tuesday, December 18, 2012

Mgogoro Waitikisa Chadema


 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk WilIbrod Slaa (Kulia) akiwa na makada wa chama hicho ambao majina yao hayakupatikana, wakiandaa taarifa kabla ya kuanza kwa siku ya pili ya kikao cha Kamati Kuu jana, Dar es Salaam. Picha na Venance Nestory
MGOGORO mkubwa unakinyemelea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kuelezwa kuwa sekretarieti yake imeyakataa mapendekezo ya Tume ndogo iliyoundwa kuchunguza kukwama kwa miradi mingi ya maendeleo, ukiwamo wa Maji Karatu Vijijini (Kaviwatu), ambayo ilitaka baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa mradi huo wafukuzwe.
Mradi huo wa maji unaelezwa kusababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho hasa baina ya sekeretarieti ambayo inadaiwa kuwakingia kifua baadhi ya watuhumiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ambao wanataka hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba alisema kwamba baadhi ya viongozi wa Chadema Wilaya ya Karatu uliko mradi huo walihojiwa jana, lakini akasema hapakuwa na mpango wowote wa kufukuzana.
“Ninachoelewa ni kwamba waliitwa wakahojiwa na kitakachofuata ni kupewa maagizo ambayo lazima wayafuate na atakayekiuka ndiye atakayefukuzwa,” alisema Mwigamba.
Baadhi ya viongozi wa Chadema Karatu waliotarajiwa kuhojiwa jana ili kupata suluhu ya mgogoro huo ni pamoja na Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse, Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Pareso na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Karatu, Lazaro Maasai na Diwani wa Karatu Mjini, Jubiless Mnyenye.
Viongozi wakuu wa Chadema hawakupatikana jana kwa kuwa muda mwingi walikuwa katika kikao hicho ambacho kilimalizika jana, huku ikielezwa kuwa taarifa rasmi kuhusu yaliyojadiliwa itatolewa leo.
Alipoulizwa kuhusu mgogoro huo, Msemaji wa Chadema Tumaini Makene alisema agenda za kikao hicho zilikuwa wazi na ziliainishwa katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa juzi.
“Hakuna zaidi ya hizo na leo (jana), ni masuala ya Katiba Mpya. Kwenye yatonakayo, masuala mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya nchi yanajadiliwa nchi nzima kwa sababu yanatokana na vikao vilivyopita si Karatu pekee. Angalia usije ukalishwa matangopori,” alisema.
Kumshinikiza Rais
Habari zaidi kutoka katika kikao hicho zinaeleza kuwa kamati hiyo imeazimia kuchukua hatua ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kusimamia utekelezaji wa masuala ambayo yapo katika mamlaka yake ikiwa ni pamoja na kumwajibisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.
Wengine ambao kimesema kinataka wawajibishwe ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Said Mwema, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile.
Kamati hiyo pia imeazimia kuanzia Januari kuwa na operesheni kubwa ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), nchi nzima kushinikiza utekelezaji hatua za kinidhamu kwa watendaji hao na watuhumiwa wa ufisadi wa Fedha za Madeni ya Nje (Epa).

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop