Waasi nchini Jamuhuri ya Afrika
ya Kati, wamekaribia mji mkuu wa nchini Bangui na wamepuuzilia mbali,
tangazo la rais wa nchini hiyo Francois Bozize, siku ya Jumapili,
kuanzisha mazungumzo ya amani na viongozi wao.
Msemaji wa waasi wa Eric Massi, ameiambia azizicompdoc.blogspot.com
kuwa, ni vigumu sana kwao kumuamini rais Bozize, kwa sababu wanajeshi
wake wanaendelea na harakati za kuwashambulia wapiganaji wao mjini
Bangui.Amesema, ikiwa jeshi la kutunza amani la Muungano wa Afrika , halitatumwa mjini Bangui, waasi hao wataingia na kutoa ulinzi wa wafuasi wao.
Lakini serikali ya nchi hiyo imekanusha madai hayo, ya kuwafanya mashambulio dhidi ya wafuasi wa waasi hao.
Siku ya Jumapili, rais Bozizi alitangaza kuwa yuko tayari kuunda serikali ya muungano wa kitaifa na waasi hao na kuwa hatawania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2016.
0 comments:
Post a Comment