Wafuasi wa rais wa Mirsi
Mohammed Morsi, wametoa wito kwa raia wote wa Misri, kushirikiana baada
ya katiba mpya yenye utata kuidhinishwa.
Kiongozi wa chama cha Muslim Brotherhood,
Mohammed Badie, amesema raia wote wa Misiri, wazee kwa kina mama,
Wakristo na Waislamu ni sharti waanza mikakati ya kuujenga upya taifa
lao, kwa hiari.Zaidi ya asilimia sitini ya watu waliopiga kura wakati wa kura ya maamuzi waliunga mkono katiba hiyo, licha ya kuwa ni asilimia thelathini ya wapiga kura wote walishiriki katika zoezi hilo.
Wakosoaji wanasema, katiba hiyo mpya inawapendelea Waislamu na inahujumu azma na nia ya mageuzi ya kisiasa nchini humo.
Rais Hosni Mubarak, aliondolewa madarakani Februari mwaka wa 2011, baada ya kuwa uongozini kwa takriban miaka thelathini.
Baada ya kutolewa kwa matokeo ya kura hiyo ya maoni hiyo jana, mamia ya wapinzani wa katiba hiyo walifunga daraja moja katika mji mkuu Cairo huku wakiteketeza magurudumu ya magari na kukatiza shughuli za usafiri katika barabara hiyo.
Mgawanyiko ulioibuka baada ya kura hiyo ya maoni, umesababisha msukosuko wa kiuchumi na kuna ripoti kuwa raia wengi sasa wakibadilisha fedha zao na kuwa na dola za Kimarekani.
Kuna ripoti kuwa kuna uhaba mkubwa wa sarafu ya dola katika maduka ya forodha.
Kabla ya matokeo hiyo kutangazwa serikali ya nchi hiyo ilitangaza kuwa watu wanaotoka au kuingia nchini humo wataruhusiwa kubeba dola lefu kumi pekee kila mmoja.
Siku ya Jumatatu, benki kuu nchini humo ilitoa taarifa kuwa, ina hazina ya kutosha ya sarafu za kigeni kukithi mahitaji ya wote.
0 comments:
Post a Comment