Wanajeshi wanaendelea na
upekuzi katika eneo kulipotokea utekaji nyara katika kiwanda cha mafuta
cha Amenas. Ndani ya kiwanda hicho zaidi ya maiti ishirini zilizoteketea
kiasi cha kutoweza kutambulika zilipatikana.
Kufikia sasa idadi ya waliofariki katika kisa hicho imefikia 80.Hata hivyo, bado haijabainika ni wangapi miongoni mwa waliopfariki walikuwa mateka.
Taarifa zaidi zinarifu kuwa Maiti za mateka kutoka Japan, Norway, Uingereza, Marekani na Malaysia bado hazijatambuliwa huku maafisa wa usalama wakisema kuwa watekaji nyara watano tayari walithibitishwa kuuawa na wapiganaji.
Takriban mateka 48 wameaminika kuuawa katika siku nne za sokomoko kwenye kiwanda cha gesi nchini Algeria.
Wanamgambo 5 inaarifiwa walikamatwa hiyo Jumapili
Maafisa wa utawala awali walisema Jumamosi kuwa watekaji nyara 32 waliuawa.
Hata hivyo makomando waliweza kumaliza vurugu hilo siku ya Jumamosi. Maafifa walisema kuwa idadi kamili ya watu waliofariki itatolewa baadaye.
Jeshi lililazimika kufanya operesheni hiyo baada ya wanamgambo hao kuanza kuwaua mateka.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na rais wa Marekani, Barack Obama, wamelaumu magaidi kwa kusababisha vifo vya mateka.
Na Jumapili, waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, alitaja kitendo cha wanamgambo hao kama kitendo cha vita.
0 comments:
Post a Comment