Welcome to our online store Portal

Template Information

Monday, January 14, 2013

Ufaransa itasaidia Mali kwa muda mfupi

Ndege ya kivita ya Ufaransa ikijiandaa kupambana na wapiganaji


Wapiganaji wa kiisilamu walioteka Kaskazini mwa Mali

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius amesema kuwa harakati za jeshi la Ufaransa katika kusaidia wanajeshi wa Mali dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu hazitachukua muda mrefu sana.
Juhudi zao zitadhumu tu wiki chache.
Mnamo Jumapili, Jeshi la wanahewa la Ufaransa liliimarisha mashambulio yake dhidi ya wapiganaji hao hasa kwenye miji ya Gao na Kidal.
Wizara ya Ulinzi ya ufaransa inasema mashambulizi hayo yatakamilika katika muda wa wiki kadhaa.


Maeneo ambayo tayari yametwaliwa na jeshi la Mali kwa usaidizi wa Ufaransa

Mamia ya wanajeshi kutoka mataifa ya Afrika Magharibi wanatarajiwa kujiunga na wanajeshi wa Ufaransa. Tayari Uingereza imetoa ndege mbili za kijeshi kusaidia katika usafirishaji wa wanajeshi na vifaa nchini mali.
Jeshi la Ufaransa lmekuwa likipambana na wapiganaji hao tangu Ijumaa , wakisaidia wanajeshi wa serikali kutwa maeneo yaliyotekwa na wapiganaji hao na hata kufanikiwa kutwa mji wa Konna.
Ufaransa imeitisha mkutano na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, baadaye hii leo.
Akiwahutubia waandishi wa habari,bwana Fabius alikataa kikosi kushirikishwa kwa muda mrefu kama ilivyo nchini Afghanistan chini ya NATO.
''Baadaye tutaweza kuondoka lakini hatuna nia ya kukaa hapa kwa muda mrefu.''
Bwana Fabius alisema kuwa ikiwa Ufaransa isingeingilia mgogoro huu, kulikuwa na tisho la wazi kuwa wapiganaji hao wangeweza kuingia zaidi ndani ya Mali na hata kufika mji mkuu Bamako, huku athari kubwa zikijitokeza.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop