WANAFUNZI IFM WAVAMIA WIZARA YA MAMBO YANDANI, WALALAMIKIA KUKOSA ULINZI KWENYE HOSTELI ZAO NA KUSABABISHA WANAFUNZI WAWILI WAKIUME KUBAKWA
|
Wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha
cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani
walipovamia leo majira ya saa nne nanusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa
ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na
kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa
walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku
waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na
kubakwa hali iliyosababishwa wanafunzi
hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama
mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.
|
|
Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya
Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova akimsikiliza Rais wa Serikali
ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya
Mambo ya ndani ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni
kwenye Kituo walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao.
Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.
|
|
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mitaa
ya Posta jijini humo wakielekea kwenye kivuko cha Kigamboni ili kwenda
kumuonyesha Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es
Salaam Suleiman Kova.
|
|
Wakianza maandamano kuelekea Feli kwaajili ya kuvuka kwenda Kigamboni. |
|
Kova akitoa
maelezo kwa waandishi wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya
kupata taarifa hizo ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja
kwenda Kigamboni kufuatilia tukio hilo kwa pamoja. |
|
Mitaani Posta. |
|
Hadi kieleweke! |
|
Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni. |
|
Kova akishangiliwa wakati wa safari kuelekea Feri. |
|
Kwenye Kona ya feri kuwania geti ili waingie bure! |
|
Wakajazana kupita kiasdi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue! |
|
Pamoja na kutakiwa kupungua hapa
wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. Picha zote
na Raha za Pwani, hii ni sehemu ya kwanza tutawaletea sehemu ya pili ya
tukio hili ambalo hadi hivi sasa filamu inaendelea hapa feri na
ikielekea Kigamboni. Picha na Saidi Powa. |
Related Product :
Why Shop on Bongo Online?
We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be
0 comments:
Post a Comment