Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya
Jinai cha Afrika Kusini (hawk) Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania
hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya
bali kemikali aina ya ephedrine.
Hata hivyo mahakama ilibaini kuwa Melissa hana
hatia kwa kuwa ilionekana amemsindikiza Masogange, aliyemuomba amsaidie
kubeba mzigo huo.
Mosagange alilipa faini ya Shilingi 2.5 milioni
(R15, 000), huku akiahidi kumaliza nusu yake ambayo juhudi zilikuwa
zinafanyika amalize kulipa jana Ijumaa.
“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kusaidia
kubeba baadhi ya mabegi, lakini haikuwa mizigo yake. Mizigo yote
iliandikwa jina la Agness Masogange na si Melissa,” alisema Kapteni
Ramaloko.
Kapteni Ramaloko alisema, Melissa alijitetea kuwa
hakuwa amesafiri na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na
Masogange alimuomba amsaidie mizigo hiyo kwani ilikuwa mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote
ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria hivyo mahakama
iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela miezi 30 (miaka miwili na miezi
sita) au alipe faini ya R30, 000(Sh 4.8 milioni).
Hata hivyo alilipa faini na nusu ya fedha hizo ilishalipwa na nyingine ilikuwa inakaribia kulipwa.
Ingawa Kamishana Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti
Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa juzi Alhamisi
alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za
kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka
ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS) Marika Muller, alieleza kuwa timu ya
SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5, mwaka huu ni
methamphetamine.
0 comments:
Post a Comment