Shahidi wa kwanza kutoka upande
wa mashtaka, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ICC kutoa ushahidi
dhidi ya naibu Rais wa Kenya William Ruto.
Mahakama inamlinda shahidi huyo kwa kutoonyosha sura yake. Kesi dhidi ya Ruto na mshtakiwa mwenzake Joshua Arap Sang, ilianza tarehe 10 mwezi Septemba, baada ya wawili hao kutuhumiwa katika kuhusika na ghasia hizo za mwaka 2007.
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu mashahidi kujiondoa kwenye kesi hiyo wakihofia usalama wao. Mwishoni mwa wiki, mashahidi wanne walijiondoa katika kesi hiyo baada ya kuelezea wasiwasi kuhusu usalama wao ikiwa watatoa ushahidi mbele ya mahakama hiyo.
Wiki jana mkuu kwenye kesi hiyo, aliakhirisha kesi hiyo kwa sababu mashahidi hawakuwa wamefika kwenye mahakama hiyo kutoa ushahidi wao.
Rais Uhuru Kenyatta, anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Novemba kwa mashtaka sawa na hayo.
0 comments:
Post a Comment