Milio mikubwa ya risasi na
milipuko imesikika huku juhudi za usalama zikiendelea katika jengo la
Westgate ambako wanamgmbo wa Al shabaab wameteka jengo hilo pamoja na
wakenya wachache ambao wangali kuokolewa.
Kwa mujibu wa waziri wa usalama Joseph Ole
Lenku, vikosi vya usalama vimeweza kudhibiti jengo hilo nje na ndani na
kwamba ni mateka wachache waliosalia katika jengo hilo.Westgate ni jumba la kifahari lenye maduka na mikahawa karibia themanini .
Milio hiyo ilidumu kwa dakika tatu na kufuatiwa na moshi mkubwa juu ya jengo hilo. Hakuna taarifa kamili kuhusu kilichosababisha moshi huo.
Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.
Aidha wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wangali ndani ya jengo hilo.
Ripoti zinasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa risasi pamoja na milipuko imesikika katika jengo hilo kwa takriban dakika 15.
Harakati za kuendelea kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora.
Rais Kenyatta amesema kuwa jeshi linajitahidi kuhakikisha kuwa linakabiliana vilivyo na wanamgambo hao.
Awali jeshi la Kenya lilisema limeweza kudhibiti jengo hilo lote ingawa bado limetaja hali kuwa tete mno hasa katika kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya jengo hilo.
Ripoti zinasema kuwa watu 69 wamefariki katika shambulizi hilo la Al Shabaab kufikia sasa huku 175 wakijeruhiwa. Baadhi wametibiwa na kuondoka hospitalini. Baadhi ya majeraha waliyopata ni majereha ya risasi na kutokana na guruneti ambalo Al shabaab waliwarushia wale waliokuwa ndani ya mikahawa siku ya Jumamosi.
Kundi hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo kutokana na hatua ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini Somalia ili kukabiliana na wapiganaji hao.
wakenya wamejitakia hakuna kulalama mnapeleka majeshi nchi ya watu kwa ajili ya uroho wa fedha za wamarekani ukichezea nyuki kubali manundu
ReplyDelete