Jengo
la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar
liliopo Maruhubi lililofunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif
Sharif Hamad jana Dec 15 2013.
Makamu
wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad akikata utepe kuashiria
ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha Maendeleo ya
Utalii Zanzibar ikiwa pia ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 50 ya
Mapinduzi huko Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Makamu
wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad akiwahutubia wananchi na
wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar katika sherehe za
ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library (kulia) Waziri wa
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk na (kushoto) naibu
wake Mhe. Bihindi Hamadi Khamis katika sherehe zilizofanyika Chuoni
Maruhubi.
Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza
Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif Hamad (hayupo pichani) katika
sherehe za ufunguzi wa Jengo la ofisi, madarasa na library ya Chuo cha
Maendeleo ya Utalii Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Picha
ya pamoja ya Mgeni rasmin Mukamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Seif Sharif
Hamad Mawaziri mbalimbali na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii
Zanzibar.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Na. Maryam Fumu Maelezo Zanzibar
Makamu
wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema
serikali imekuwa na muelekeo mkubwa wa kuimarisha sekta ya Utalii na
kuleta mafanikio makubwa yanayoweza kuingiza watalii kutoka nchi mbali
mbali duniani.
Alisema
Zanzibar inaimarika mwaka hadi mwaka katika sekta hiyo ambapo hivi sasa
imekuwa ikichangia wastani wa asilimia 80 ya fedha za kigeni katika
kukuza uchumi wa Zanzibar.
Alieleza
hayo katika ufunguzi wa jengo la ofisi, Madarasa na Library ya chuo cha
maendeleo ya Utalii Maruhubi ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za
maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema
kuwa serikali ina malengo makubwa ya kuiendeleza sekta hiyo kwa lengo
la kuwanufaisha Wazanzibar na kufikia dhana ya utalii kwa wote
kupitia katika ngazi zote za wilaya za Unguja na Pemba.
Hata
hivyo Maalim Seif amewataka viongozi kufanya juhudi kwa kukiimarisha na
kuletea maendeleo Chuo hicho kwa kuweka msimamizi mzuri wa historia
ya utamaduni, mila na silka za Wazanzibar ili zienendelee kuchafuliwa.
Pia
makamo wa kwanza wa Rais aliahidi kulichukulia hatua barabara liliopo
chuoni hapo ili liweze kupatiwa ufumbuzi.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho, Bi .Zuleikha Kombo Khamis,
amewaomba viongozi kushirikiana na sekta Utalii katika kukijenga chuo
hicho katika sehemu ilioharibika ili iweze kuwa na mazingira mazuri.
Aidha
Mkurugenzi huyo alisema kuwa changamoto zinazokikabili chuo hicho
ikiwemo ukosefu wa barabara pamoja na mmongonyoko wa ardhi sehemu ya
nyuma ya chuo hicho linapelekea kuharibu maendeleo ya chuo.
Hata
hivyo Bi. Zulekha ameshukuru serikali ya awamu ya saba kwa kuwajengea
Jengo la Ghorofa mbili jambo ambalo linawapa faraja katika kuleta
maendeleo chuoni hapo.
0 comments:
Post a Comment