KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye.
*Asema sasa ni fundisho kwa watakaolala
*ziara za Kinana zimesaidia sana kutatua kero
*Bado moto wa ziara hizo haujapamba
*2015 CCM kurejesha viti vya ubunge, Udiwani vilivyoko upinzani
KATIBU
wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amesema amepokea kwa faraja
kubwa, hatua ya mawaziri wanne kuenguliwa nyadhifa zao kwa ridhaa ya
Rais Jakaya Kikwete.
“Najisikia
vizuri, maana kwa kitendo cha mawaziri hao wanne kuchuliwa hatua,
ninaamini kitasaidia wale wengine waliolala nao waamke. Bila shaka sasa
hakuna atakayelala na akilala anajua itakula kwake.”, alisema Nape
akijibu swali la mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Emmanuel
Buhohela, kwenye kipindi cha ‘mahijiano’ cha televisheni hiyo, mjini Dar
es Salaam, leo asubuhi.
Mtangazaji huyo alitaka kujua, Nape kama kiongozi wa ngazi ya juu CCM, amejisikia au kupokeaje hatua ya Bunge
kumuomba
Rais kuwawajibisha mawaziri hao wanne na kisha Rais kuridhia ombi hilo
kwa kutengua uteuzi wake wa nafasi za mawaziri hao jana.
Mawaziri
waliofutiwa uteuzi wao na Rais na nafasi walizotoka zikiwa kwenye
mabano ni, Dk. Emmanuel Nchimbi (Waziri wa Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai
(Waziri wa Ulinzi), Mathayo David Mathayo ( Mifugo na Maendeleo ya
Uvuvi) na Khams Kagasheki (Maliasili na Utalii) ambaye ndiye pekee
pamoja na uteuzi wake kutenguliwa na Rais lakini alitangaza kujiuzulu
akiwa Bungeni, jana.
Kutenguliwa
kwa uteuzi wa mawaziri hao kulitangazwa rasmi Bungeni jana jioni, na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hatua inayoaminika kuwa imetokana na
shinikizo la bunge, baada ya Kamati yake ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili
na Mazingira kubaini ‘uozo’ katika operesheni iliyofanyika hivi karibuni
ya tokomeza ujangili.
Chini
ya Mwenyekiti wake, James Lembeli, Kamati hiyo ilieleza kwamba pamoja
na mambo kadhaa iliyoyaeleza kuwa ya hovyo yaliyojitokeza kwenye
operesheni hiyo, vitendo vingi ikiwemo ubakaji na udhalilishaji
vilifanyika ambapo ni kinyume na utu na haki za binadamu.
Kufuatia
kadhia hiyo, Kamati hiyo kupitia kwa Lembeli, iliwataka mawaziri
wanaohusika kutazama kama wanafaa kuendelea na nyadhifa zao au
wajiuzulu, na pia Kamati hiyo ikaenda mbali zaidi kwa kumuomba Rais
Jakaya Kikwete kuchukua hatua ya kuwawajibisha.
Akizungumzia
zaidi hatua hiyo, Nape alisema, pamoja na mawaziri hao kuwajibika,
lakini ipo haja ya kwenda mbali zaidi kwa kutazama mifumo na sheria
zilizopo sasa kwa kuwa inaonekana navyo ni miongoni mwa vyanzo vya
vikwazo katika utekelezaji wa utawala bora.
“Kwa
mfano leo hii, mawaziri wameng’oka, sawa ni jambo jema, sitetei, lakini
inawezekana kabisa kuna mifumo na sheria ambazo zilimkwaza Waziri huyu
kutimiza wajibu wake. Mfano, alihitaji kumfukuza mtu kazi kwa kuzembea
jambo fulani, lakini malmaka ya kufukuza kazi mtumishi yapo kwa Katibu
Mkuu wa Wizara, hapa atafanyaje!”, alisema Nape na kuongeza;
“La
msingi hapa ni lazima sasa hatua hizi ziende mpaka chini huku kwa
watendaji, ili isiwe mawaziri wanawajibishwa tu kwa sababu ya dhamana
zao za kusimamia kisiasa, huku watendaji wanazidi kuvuta shuka bila hofu
wakati baadhi yao ni sehemu ya matatizo”.
Akijibu
swali kuhusu ziara za Katibu Mkuu na sekretarieti ya CCM mikoani, Nape
alisema, ziara hizo ndiyo kwanza zimeanza, na mado moto wake mkubwa
zaidi unakuja hasa itakapokaribia uchaguzi mkuu wa 2015.
Nape
alisema, ziara hizo, zimeonyesha matunda makubwa sana, klwa kuwa
zimesaidia kupunguza kero nhyingi katika maeneo zilikofanyika.
Alitoa
mfano wa ziara hiyo ilivyoweza kuondoa msongamano wa malori wilayani
Tunduma mkoani Mbeya, akisema kwamba wakati Kinana na msafara wake
wanaingia tunduma walikuta msongamano ni mkubwa sana kutokana na
wafanyakazi wanaohudumia malori hayo kufanya kazi kwa mda mfupi.
“Baada
ya kuiagiza serikali isimamie wafanyakazi wa eneo hilo wafanya kazi kwa
saa 24, kwa zamu, siku ya pili yake ya agizo hilo, msongamano
ulionekana kupungua sana na kuleta nafuu kwa madereva na wafanya
biashara kwa jumla pale Tunduma”, alisema Nape.
Nape
alisema, pia kutokana na ziara hizo, mgogoro uliokuwa mkubwa baina ya
wananchi na wenye mgodi wa machimbo Nyamongo, umepungua kwa asilimia 90
sasa, na hali imekuwa ya kuridgisha sana.
Akizungumzia
wabunge wanaodaiwa kulipwa posho bila kuzifanyia kazi, Nape alisema,
kurudisha fedha pekee hakutatosha, kwa upande wa CCM ambayo ndiyo yeneye
wabunge wengi itabidi ichukue hatua zaidi dhizi ya waliohusika na
kadhia hiyo bila kuoneka mtu.
Kuhusu
ajira kwa vijana, Nape alaisema ili kutimiza hilo, ni lazima viwanda
vifufuliwe kwa dhati kabisha, ikiwa ni kuchukua hatua za kuwanyang’anya
wawekezaji waliochukua viwanda mbalimbali kwa lengo la kuviendeleza
lakini baadhi yao majengo ya viwanda hivyo wakayafanyia shughuli zingine
tofauti ikiwemo kuyageuza maghala.
Nape
aliitaka pia serikali kupunguza au kuondoa kabisa urasimu katika
kupokea wawekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi hapa nchini
akisema, kwamba, kwa sasa vikwazo na urasimu bado ni vingi sana kiasi
kwamba wawekezaji waanakwazika na hivyo kupunguza kasi ya uwekezaji
ambao wakiongezeka haraka ajira kwa vijana nazo zitakua haraka.
Alisema,
hatua ya sasa inayofanywa na CCM kusimamia serikali ni ya kawaida
kabisa kwa kuwa kazi hiyo haipaswi kufanya na wapinzani kwa kuwa sera
inayotekelezwa siyo yao, na wahaijui.
Nape
aliahidi kwamba katika uchaguzi zijazo CCM itakomba viti vyote vya
ubunge na udiwani vililivyopo sasa chini ya wapinzani, akisema, kwamba,
baada ya wapinzani kujaribiwa wameshindwa kuonyesha matunda yoyote ya
kusaidia wananchi na hivyo kutokuwa mbadala wa CCM.
0 comments:
Post a Comment