Makamu wa Rais
Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda
mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo
alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake.Akiwa nachini Marekani
Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban ki
Moon nakufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania
katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali.(picha na Freddy Maro).
Makamu wa Rais
Dk.Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Rais Dkt.Jakaya Kikwete Mrisho
mara baada ya kumlaki muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea
jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya
yake nchini Marekani. Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Bwana Ban Ki Moon na kufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa
majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amewasili nchini jana, Ijumaa, Desemba 27, 2013, akitokea New York,
Marekani.
Rais Kikwete amekuwa New York kwa wiki moja kwa shughuli za kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam,
Rais Kikwete amelakiwa na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Makamu wa
Rais, Mheshimiwa Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
0 comments:
Post a Comment