Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na Rais
Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura Bush wakiwa jukwaa
la viongozi na watu mashuhuri baada ya Kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo
cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na duniani, Mheshimiwa
Nelson R Mandela jana Desemba 10, 2013 katika uwanja wa FNB jijini
Johannesburg.(PICHA NA IKULU).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
jana, Jumanne, Desemba 10, 2013, ameungana na viongozi wa mataifa mbali
mbali duniani na maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini Kuadhimisha
Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa kiongozi mashuhuri wa Afrika Kusini na
duniani, Mheshimiwa Nelson R Mandela.
Maelfu
kwa maelfu ya wananchi wamehimili mvua kubwa iliyokuwa inanyesha kwa
nguvu kwenye Uwanja wa Michezo wa FNB mjini Johannesburg kumwaga Mzee
Mandela ambaye alikuwa ishara kuu ya upinzani wa siasa za ubaguzi wa
rangi za makaburu wa Afrika Mashariki.
Mheshimiwa
Mandela ambaye alifariki duniani Ijumaa iliyopita, Desemba 5, 2013,
alikuwa Kamanda wa Jeshi la Ukombozi la Chama cha African National
Congress la Umkhoto we Sizwe akafungwa jela kwa uhaini kwa miaka 27 na
utawala wa Makaburu.
Baada
ya kutoka jela mwaka Februari 1990, Mzee Mandela alichaguliwa kuwa Rais
wa Kwanza wa Afrika Kusini ya mwaka 1994. Lakini Mheshimiwa Mandela
alitumikia kipindi kimoja tu cha miaka mitano na kukataa kutumikia
kipindi cha pili.
Kiasi
cha viongozi 91 kutoka sehemu duniani wamehudhuria Kumbukumbu hiyo
iliyokuwa na kila aina ya mchanganyiko wa hisia – wengine wakiwa na
majonzi na wengine wakicheza na kuimba kwa muda wote wa shughuli hiyo
iliyochukua kiasi cha jumla ya saa tano.
Mbali
na Rais Kikwete ambaye amefuatana na Mama Salma Kikwete, marais wengine
mashuhuri duniani waliohudhuria Kumbukumbu hiyo ni Mheshimiwa Barack
Obama wa Marekani, Mheshimiwa Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu
wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa (UN) Ban Ki Moon.
Kumbukumbu
hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa zamani wa Marekani wakiwemo marais
watatu wa zamani wa Marekani – Mheshimiwa Jimmy Carter, Mheshimiwa Bill
Clinton na Mheshimiwa George W Bush na mawaziri wakuu wawili wa zamani
wa Uingereza, Mheshimiwa Tony Blair na Mheshimiwa Gordon Brown.
Rais
Kikwete leo, Jumatano, Desemba 11, 2013, ataungana na viongozi wenzake
katia katika kutoa heshima za mwisho na kuuaga rasmi mwili wa Marehemu
Mandela ambao utawekwa kwenye Majengo ya Urais wa Afrika Kusini ya Union
Buildings mjini Pretoria.
0 comments:
Post a Comment