Mwenyekiti
wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya
klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga.
Mwenyekiti
wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi
na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki
dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Akiongea
na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa
wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia
sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini
isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
“Mechi
ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata
pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya
milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi
tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea”
alisema Manji.
Aidha
amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika
tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi
Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi
mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji
wengi timu ya Taifa.
Manji
pia alisema anawapa hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la
jana, amesema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi
kwa hilo.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokeza katika
mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye
anasafiri leo kwenda nje ya nchi majukumu yote amemkabidhi makamu
mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.
Habari kwa hisani ya Youngafricans.co.tz
0 comments:
Post a Comment