Friday, November 23, 2012

Mkuu wa polisi auawa Benghazi

Afisa mmoja mkuu wa usalama nchini Libya amepigwa risasi na kuuawa nje ya nyumba yake mjini Benghazi.
Wizara ya usalama wa ndani nchini humo imeelezea kuwa Bwana Farraj al-Dursi , ambaye alikuwa mkuu wa polisi mjini humo, amefariki kutokana na majeraha ya risasi baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Kumekuwa na visa vingi vya mauji mjini Benghazi katika siku za hivi punde.
Mnamo mwezi Septemba, balozi wa marekani mjini Benghazi aliuawa pamoja na wamarekani watatu katika ubalozi huo.
Col Dursia aliteuliwa kuwa mku wa polisi mjini humo muda mfupi baada ya shambulio lililotekelezwa kwenye ubalozi wa Marekani, ambalo balozi wa Marekani na maafisa watatu waliuawa.
Maafisa kadhaa wa Ulinzi wameuawa na watu wasiojulikana mjini Benghazi, mji ambao maandamano na machafuko yaliyomuondoa madarakani Muamarr Gaddafi yalianza.
Mwandishi wa BBC mjini Tripoli, anasema wengi wa maafisa hao wanalengwa kwa sababu wanakisiwa kuwa na uhusiano na serikali ya ya zamani ya nchi hiyo.
Kabla ya serikali, ya Gadaffi kuondolewa madarakani, Kanali, Dursi alifahamika kuwa afisa aliyehusika na kitengo cha kupambana na dawa za kulevya.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About