Friday, November 30, 2012

Rasimu ya katiba Misri yaidhinishwa

 Generali Mamdou Shahin (Kulia) akishauriana na maafisa wa kamati ya katiba kabla ya kupigiwa kura
Kamati inayoandika katiba nchini Misri imeidhinisha rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.
Hayo yaliafikiwa katika shughuli iliyochukua saa kumi na sita, na kamati hiyo ilikubaliana kwa kauli moja kupitisha vifungu viwili thelathini na nne.
Rasimu hiyo sasa sharti iidhinishwe na rais Morsi kabla ya kupigiwa kura ya maoni.
Wanasiasa waliberali pamoja na wakristu walisusia shughuli za kamati wakisema walihisi kutengwa.
Akizungumza kwa runinga awali Rais Mohamed Morsi amesema kuwa atajiondolea mamlaka mapya aliyojikabidhi pindi tu watu watakapokubaliana kuhusu katiba.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About