Waasi wa DRCongo wagoma kuondoka Goma

Waasi wa DRCongo wagoma kuondoka Goma
http://3.bp.blogspot.com/-c82acwUdHt4/ULMIwulktoI/AAAAAAAAAiE/oWCHfNJC3OU/s72-c/congo.jpg


Waasi wa M23 wamekataa pendekezo la viongozi wa mataifa ya eneo la Maziwa Makuu la kuwataka wakomeshe mapigano na kuondoka mjini Goma.
Waasi hao wanaipinga serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kupigana nalo katika eneo la mashariki mwa taifa hilo.
Viongozi hao walitoa pendekezo hilo kutoa fursa mazungumzo ya amani yafanyike ili kutafuta suluhu kwa mgogoro huo.
Hatua ya waasi hao kuuteka mji wa Goma yapata wiki moja iliyopita imezua wasiwasi kwamba huenda yakatokea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Awali, serikali ilisema haiwezi kufanya mazungumzo na waasi hao hadi pale watakapoondoka mjini Goma.
Kupitia taarifa, marais wa Rwanda, Kenya, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliiambia M23 "ikomeshe mapigano mara moja na iondoke Goma", na hali kadhalika "ikome kusema kwamba inakusudia kuipindua serikali."
Marais hao pia walipendekeza kawmba:-
  • Serikali hiyo iyaangalie "matakwa halali ya M23"
  • M23 ijiondoe katika maeneo iliyoteka na kusogea takriban 20 km kutoka Goma katika kipindi cha siku mbili
  • Kuundwa kwa kikosi cha pamoja cha wanajeshi kutoka nchi za eneo, serikali, na waasi watakaokuwa katika kiwanja cha ndege cha Goma
  • polisi wa Goma warudishiwe silaha na kurudi kazini
  • walinda amani wa Monusco wawekwe katika eneo huru, kati ya Goma and waasi M23
Share this product :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger