Welcome to our online store Portal

Template Information

Saturday, December 15, 2012

Baada ya mauaji Obama atoa nasaha

Kufuatia ya moja kati ya mauaji makubwa kutokea katika historia ya Marekani, wanasiasa akiwemo Rais Barack Obama, wametaka sheria kuhusu umiliki wa bunduki nchini Marekani zibadilishwe, ili kuepusha maafa kama hayo siku za usoni.
Rais Obama akifuta machozi baada ya taarifa za mauji ya watoto wadogo

Akizungumza baada ya mauaji ya watoto na watu wazima 26 katika shule moja ya msingi katika jimbo la Connecticut Ijumaa, Rais Obama aliyeonekana kujawa na huzuni, alitoa wito kuchukuliwe hatua ya maana kuzuwia mauaji kwa kutumia bunduki.
Hakutoa maelezo zaidi.
Taarifa zaidi zimejitokeza kuhusu yaliyotokea katika mauaji hayo katika shule ya msingi ya Sandy Hook mjini Newtown.
Mshukiwa mwenye umri wa miaka 20 - aliyeitwa Adam Lanza - alimuuwa mama yake nyumbani kwake, kabla ya kuelekea katika shule hiyo na kuwafyatulia risasi wanafunzi.
Walioshuhudia walisema walisikia zaidi ya milio mia moja ya risasi na kuwaona watoto waliokuwa wakihofia maisha yao wakilikimbia jengo.
Wanafunzi hao walikuwa kati ya umri wa miaka mitano na kumi.
Wakaazi wa Newton wamekesha wakiomboleza.
Rais Obama ametoa amri kuwa bendera zipepee nusu mlingoti kwenye majengo ya taifa.
Akizungumza juu ya mauaji hayo, waziri mkuu wa Australia, Julia Gillard, alisema tukio hilo limezidi kusikitisha kwa vile waliouwawa ni watoto.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop