Welcome to our online store Portal

Template Information

Wednesday, January 16, 2013

Mashambulizi makali dhidi ya waasi Mali

Wanajeshi wa Ufaransa wanasema waasi wangali wanaudhibiti mji wa Konna

Wanajeshi hao wanaelekea kaskazini wakiwa na mitutu ya bunduki tayari kwa makabiliano.
Kwa wakati mmoja watu walisimamisha msafara huo na kuwapungia mikono wanajesho hao wa ufaransa.
Hadi kufikia sasa juhudi za ufaransa dhidi ya waasi hao zimeimarishwa kwa mashamulizi ya ndege za kivita na helikopta.
Hata hivyo hatua hiyo hainaonekani kuzaa matunda kwani kungekuwa na mafanikio tu endapo mabomu hayo yanayorushwa yangekuwa yakiwalenga waasi wanaohusika kwani kwa sasa wana uwezo wa kujipanga upya.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa msafara huo utavamia miji ya Diabalay ama Konna ambayo inakaliwa na wapiganaji wa kiislamu.

Wakati ufaransa ilipoanza kuwashambulia wapiganaji hao Mashariki mwa Mali ilisemekana kuwa mamia ya wanajeshi wa Ufaransa walikuwa wakishiriki.
Wakati huohuo, maafisa katika jeshi la Ufaransa, wamekanusha madai yaliyotolewa awali na jeshi la Mali, kuwa wameweza kuudhibiti mji wa Konna uliokuwa umetekwa na waasi.
Ufaransa, ilianza harakati zake za kijeshi kusaidia jeshi la Mali dhidi ya waasi Ijumaa iliyopita baada ya wapiganaji wa kiisilamu kuuteka mji wa Konna na kuanza kuukaribia mji mkuu.
Mji mwingine wa Kati ,Diabaly, ulitekwa na waasi Jumatatu iliyopita.
Wanajeshi wa Ufaransa wakishirikiana na wa Mali, wameanza kuelekea katika mji huo kuanza operesheni yao ya ardhini dhidi ya waasi.
Mwezi Machi mwaka jana wapiganaji wa kiisilamu wakishirikiana na waasi wa Tauareg, waliteka Kaskazini mwa Mali.
Hivi karibuni wapiganaji hao walio na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda, walidhibiti eneo hilo na kuanza kuweka sheria kali za kiisilamu.
Pindi mpango wa serikali wa kuutwaa mji huo , waasi nao wakaanza kuelekea Kusini mwa nchi.
Rais Francois Hollande

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, alisema kuwa Ufaransa ina lengo moja tu, kuhakikisha inaondoka Mali, baada ya nchi hiyo kuwa salama na kuhakikisha kuwa hakuna tisho lengine la kigaidi dhidi ya nchi hiyo.
Hatua ya wanajeshi kuteka mji muhimu wa Konna wiki jana , ndiyo ilichochea Ufaransa kuchukua hatua za kijeshi kusaidia Mali.

Ndege za Ufaransa, zilianza kufanya mashambuliziya angani dhidi ya wapiganaji hao siku iliyofuata hadi Jumamosi.

Maafisa walisema kuwa jeshi la Mali lilisema limeweza kudhibiti mji wa Konna na kwamba wapiganaji
100 waliuawa.
Lakini waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian, aliambia waandishi wa habari mjini Paris kuwa mji huo bado uko mikononi mwa waasi.
Ndege za kijeshi za mali ziliweza kuzuia waasi waliokuwa wameingia eneo lililo katikati mwa miji ya Douentza na Gao.
Duru hata hivyo zinaarifu kuwa jeshi la Mali halina uwezo mkubwa wa kudhibiti waasi kivyao

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop