Saturday, January 26, 2013

Ofisi ya serikali yachomwa moto Suez
Hayo yametokea wakati maelfu ya watu wakipita mabara-barani kwenye mhadhara wa mazishi ya wale waliokufa katika mapambano ya Ijumaa - siku ya kuadhimisha miaka miwili ya kuanza ghasia zilizomuangusha Rais Hosni Mubarak.
Wanajeshi wa serikali wanaendelea kupiga doria mjini Suez.
Watu kama 10 walikufa katika ghasia za Ijumaa.
Mjini Cairo, mapambano piya yamezuka kati ya askari polisi na waandamanaji karibu na wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Misri.
Polisi walifyatua moshi wa kutoza machozi kujaribu kuwazuwia waandamanaji wasifike kwenye jengo la wizara.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About