Monday, January 7, 2013

Zuma atuma wanajeshi zaidi Bangui


Afrika Kusini imethibitisha kwamba imetuma wanajeshi zaidi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati huku wapiganaji wanaendelea kusonga dhidi ya serikali.
Wanajeshi wa Afrika Kusini wakipanda ndege nje ya Pretoria

Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za nje mjini Pretoria alieleza kuwa wanajeshi 120 zaidi wametumwa kulinda wanajeshi wa Afrika Kusini ambao tayari wako Jamhuri ya Afrika ya Kati kulifunza jeshi la serikali.
Ofisi ya Rais Zuma inasema kuwa serikali imeidhinisha jumla ya wanajeshi 400 kutumwa huko.
Wapiganaji na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wanatarajiwa kuanza mazungumzo katika siku za karibuni.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About