Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akiwaonesha
waandishi wa habari(hawapo pichani)moja ya silaha walizokamatwa nazo
watuhumiwa .
Waaandishi wa habari wa Mkoa wa Kilimanjaro wakisikiliza maelezo toka
kwa kamanda wa polisi wa mkoa huo Robert Boaz(hayukopichani).
Baadhi ya viongozi waandamizi wa jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro.
JESHI la polisi mkoani kilimanjaro linawashikilia watu wawili kwa
tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Robert Boaz amewataja
watuhumiwa hao kuwa ni, Mohammed Shani (24) na Emmanuel Jumanne (30),
wote wakazi wa Bomangombe na Sanya juu wilayani Hai.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kamanda Boaz amesema kuwa
januari 19 mwaka huu majira ya saa kumi jioni huko Bomangombe
mtuhumiwa wa kwanza Mohammed Shani alikamatwa akituhumiwa kujihusisha
na matukio mbali mbali ya unyanganyi kwa kutumia silaha.
Boaz amesema mtuhumiwa huyo alipohojiwa alikiri kuwa anayo silaha
ambayo huitumia kwenye matukio mbali mbali ya uhalifu akiwa
anashirikiana na wenzake ambapo aliweza kuwaonyesha polisi sehemu
alipokuwa ameihifadhi silaha hiyo.
Kamanda Boaz, amesema kuwa silaha iliyokutwa na mtuhumiwa huyo ni,
Bunduki aina ya MARK IV ambayo imefutwa namba za usajili na kukatwa
kitako na mtutu pamoja na vifaa vya kutendea uhalifu kama kinyago
(mask) 1,maboshore 2, masweta 2,pamoja na risasi 13.
Kamanda Boaz, amesema baada ya kuhojiwa, Mtuhumiwa alimtaja alimtaja
mtuhumiwa wa pili Emanuel Jumanne na kuelekeza chumba anamoishi na
kilipopekuliwa ilipatikana bunduki moja aina ya shortgun
iliyotengenezwa kienyeji na risasi mbili za shortgun, kofia ya jeshi
la polisi, boshore 1,begi dogo lililokuwa limehifadhia bunduki hiyo.
Aidha kamanda aliongeza kuwa msako ulianza na kufanikiwa kumkamata
mtuhumiwa huyo akiwa wilayani Karatu ambapo kwa pamoja walikiri
kufanya matukio mbali mbali katika maeneo ya Bomangombe na Sanya juu
na Moshi.
Boaz aliongeza kuwa makosa mengine ni madereva wasiokuwa na
leseni,ulevi,kutokuwa na motor vehicle licence,kutokuwa na bima na
kupakia abiria kwenye magari ya mizigo.
Amesema kiasi hicho cha fedha kimetokana na tozo za notification na
lengo kuu likiwa ni kupunguza ajali za vifo na majeruhi.
0 comments:
Post a Comment