![Rais Francois Hollande](http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/01/11/130111121937_hollande_speech_304x171__nocredit.jpg)
Rais wa Ufaransa Francois Hollande
Jeshi la Mali limekuwa likishirikiana na lile la Ufaransa kupambana na wapiganaji wa kiisilamu Kaskazini mwa nchi
Rais wa Ufaransa Francois
Hollande anatarajiwa kuzuru Mali, ambako makabiliano ya wiki tatu kati
ya waasi na wanajeshi yamekuwa yakiendelea.
Wapiganaji hao walipata pigo kubwa kufuatia mashambulizi ya angani dhidi yao yaliyowalazimisha kutoroka.Bwana Hollande ataenda mjini Bamako kukutana na Rais wa Mpito Dioncounda Traore.
Aidha rais Holland atazuru Timbuktu,moja ya miji iliyokombolewa na wanajeshi wa Ufaransa wakishirikiana na wale wa Mali, Jumamosi wiki iliyopita.
0 comments:
Post a Comment