Saturday, March 9, 2013

MATOKEO RASMI YA UCHAGUZI MKUU KENYA KUTANGAZWA LEO 
Ubashiri wa Uhuru na RailaTume ya uchaguzi nchini Kenya imesema itatangaza matokeo yaliosalia ya urais siku ya Jumamosi saa tano asubuhi (11am), Afrika Mashiriki.
Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa uchaguzi huo na vile vile kama mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya kutangazwa kuwa rais wa nne wa Kenya.
Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Tume Isaack Hassan.
Ingawa kumesailia maeno yasiozidi kumi, lakini kamshna hiyo amesema lengo la tume ni kuhakiki matokeo yote na kuondoa dosari zozote ambazo pengine zimejitokeza kabla ya kumtangaza mshindi.
Miongoni mwa masharti hayo ni kuwa kabla ya mtu kutangazwa kuwa rais katika duru ya kwanza ya uchaguzi lazima awe amepata asilima 50+1 ya kura zote zilizopigwa.

Vile vile mgombea huyo pia lazima awe ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili azungumzie maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo uliahirishwa hadi siku ya Jumamosi , baada ya tume ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About