Rais Hugo Chavez wa Venezuela afariki dunia

Rais Hugo Chavez wa Venezuela afariki dunia
http://4.bp.blogspot.com/-BdYwPG68dko/UTdbvjekr5I/AAAAAAAABKE/lDP1NsIKIow/s72-c/rais.jpg

Wafuasi wa Hugo Chavez wamekuwa wakimuombea aweze kuugua pole

Katika taarifa kwa taifa, makamu wa rais wa Venezuela Nicholas Marduro ametangaza kufariki dunia kwa rais Hugo Chavez, 58, kufuatia kuugua muda mrefu maradhi ya Saratani. Rais Chavez ametoweka katika hadhira ya nchi hiyo kwa muda mrefu ambapo alikuwa anapokea matibabu nchi jirani ya Cuba.
Alirejea , mjini Caracas mnamo Februari 18 kwa mara ya kwanza tangu maradhi yake yamzidie ambapo alipelekwa hospitali ya kijeshi kuendelea kupokea matibau. Hata hivyo maelezo zaidi hayakutolewa juu ya afya yake. Waandamanaji waliandamana katika mji mkuu Caracas mwishoni mwa juma wakidai kuwa watu wa Venezuela wanapaswa kupewa habari zaidi kuhusu afya ya rais wao.
Bwana Chavez amekua uongozini nchini Venezuela kwa miaka 14 na anatazamiwa kuleta mageuzi makubwa yaliyolenga zaidi kuimarisha maisha ya raia wa pato la chini.

Ujumbe wa Jeshi
Taarifa kutoka kwa jeshi imesema kuwa wataendelea kuilinda hadhi ya nchi na kuimarisha usalama. Pia jeshi limeahidi kuendelea kuwa waaminifu kwa makamu wa rais Nicholas Marduro na wakatoa wito kwa raia kuwa watulivu
Share this product :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger