Friday, April 5, 2013

KOREA YA KASKAZINI YAIPA WASIWASI MAREKANI

Jeshi la Marekani likiajiandaa kwa mashambulizi kutoka kwa Korea Kaskazini

Marekani imepeleka mitambo ya kukinga makombora katika kisiwa cha Guam katika bahari ya Pacific huku Korea Kaskazini ikitishia kurusha makombora ya nuklia nchini humo.
Idara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema kuwa mitambo hiyo itakuwa tayari katika kipindi cha wiki kadhaa , na kuongeza kwa zana za kivita ambazo zilipelekwa katika eneo hilo.
Korea Kaskazini ilitaja kisiwa cha Guam kuwa miongoni mwa maeneo yanayolengwa kwa mashambulizi ikiwemo Hawaii na Marekani.
Korea Kaskazini haidhaniwi kuwa na teknolojia ya kutosha kushambulia Marekani kwa zana za nuklia au makombora ya masafa marefu.
Korea Kaskazini inasema kwamba imewaweka wanajeshi wake, tayari kwa shambulio dhidi ya Marekani ikiwemo kutumia zana za nyukilia.
Taarifa hii imejiri wakati Marekani imeimarisha mitambo yake ya kukinga makombora katika kisiwa cha Guam kilichoko bahari ya Pacific.

Idara ya ulinzi ya Korea Kaskazini imesema inatoa taarifa kwa Marekani kwamba jeshi lipo tayari kushambulia bila huruma, kile imetaja kama vitisho vya Marekani dhidi yake.
Utawala wa Pyongyang ulionekana kukerwa na hatua ya Marekani ya hivi maajuzi ambapo wanajeshi wake walifanya mafunzo ya pamoja na ambayo yalihusisha utumizi wa zana za kivita.
Hata hivyo wachanganuzi wamesema Korea Kaskazini haina silaha ambazo zinaweza kushambulia ardhi ya Marekani, japo katika siku za karibuni imefanya majaribio ya makombora ua masafa marefu.
Hapo jana Jumatano, Korea Kaskazini iliwazuia wafanyikazi wa Korea Kusini kuvuka mpaka kuelekea katika viwanda vya pamoja vinavyomilikiwa na nchi mbili, na hivyo kukatiza uhusiano uliobaki kati yake na Kusini.
Baadhi wanaona malumbano ya sasa kama hatua ya Korea Kaskazini kushinikiza Marekani kuanzisha mazungumzo ya pamoja ambayo yataafikia mkataba wa amani.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About