Wednesday, April 3, 2013

NAULI MPYA ZATANGAZWA RASMI NA SUMATRA

VIWANGO VIPYA VYA USAFIRI WA DALA DALA NA MABASI TOKA SUMATRA 

 Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.


SUMATRA ina wajibu kisheria kuhakikisha pamoja na mambo mengine kuwa maslahi ya watumiaji na watoa huduma za usafiri yanalindwa ili kuwepo na huduma endelevu ya usafiri ulio bora, salama na wenye kukidhi mahitaji.  Aidha SUMATRA ina jukumu la kujenga na kulinda mazingira mazuri na ya kuvutia kwa watoa huduma ili huduma ya usafiri inayotolewa inakuwa katika kiwango na gharama zinazoendana na huduma zenyewe.  Bofya Hapa Kuona viwango vya nauli
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About