Zuma akutana na Tiangaye Pretoria

Zuma akutana na Tiangaye Pretoria
http://4.bp.blogspot.com/-6BsKbYAUI6Y/UX185zUlxyI/AAAAAAAABxM/nnYalR5gdlQ/s72-c/azx.jpg

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na waziri mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nicolas Tiangaye, wamekutana mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria, na wamekubaliana kuzidisha uhusiano baina ya nchi mbili hizo.
Uhusiano uliharibika baada ya wanajeshi 13 wa Afrika Kusini kuuwawa mwezi March wakati wapiganaji walipoiteka serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliarifu kuwa wanajeshi hao walipelekwa huko ili kampuni za biashara za Afrika Kusini zipate kandarasi za madini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wakuu wa Afrika Kusini walikanusha hayo.
Share this product :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger