Mali yaomba msaada kufadhili harakati za kijeshi |
Zaidi ya wajumbe 100 wanakutana mjini Brussels, Ubeljiji kuchangisha fedha kutolewa kama msaada utakaotolewa kwa nchi ya Mali. Hili ndilo kongamano la kwanza tangu wanajeshi
wa Ufaransa kuanzisha opesheni kazkazini mwa Mali dhidi ya wapiganaji wa
kiiisilamu waliotwaa nusu ya maeneo ya nchi.
Wanajeshi wa Ufaransa waliingia ndani ya Mali kukabiliana na wapiganaji wa kiisilamu wenye uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda.
Wapiganaji hao walifanikiwa kuthibiti maeneo ya kaskazini mwa Mali kutokana na udhaifu wa serikali iliyolaumiwa kuwa kujihusisha zaidi na ufisadi. Kipao Mbele kwa sasa ni jinsi ya kufanya mageuzi kwenye jeshi na tasisi nyingine za taifa.
Kumekua na shinikiza kwa Mali kuandaa uchaguzi mkuu wa kidemokrasia ifikapo mwezi Julai, japo raia wengi wameelezea ugumu wa kuafikiwa hilo.
Shirika la misaada la Oxfam limesema kwamba Mali itahitaji msaada kwa miaka 15 ijayo, ili kuafikia malengo yanayotarajiwa.
Licha ya juhudi za sasa, kungali na msukosuko wa kisiasa Mali, Kaskazini mwa Mali waafrika Weusi wamelalamikia kugabuliwa na jamii za kiarabu na Tuareg.
Kwa upande mwingine Tuareg na Waarabu wamelalamikia kubaguliwa na serikali Kuu iliyoko Bamako. Wafadhili wanasema ni muhimu kuwepo, na maridhiano kati ya jamii zote.mak
0 comments:
Post a Comment