Thursday, May 9, 2013

SHEKH PONDA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA

Mahakama ya Kisutu leo hii imetoa hukumu ya Shekh Ponda kwa kumuhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja (1) na kuwaachia huru wenzake 49, kutokana na hukumu hiyo kauli yake ya Allah ndio hakimu mkuu kuliko wote ameidhihirisha pale alipowaona wafuasi wake wakimlaki kwa furaha huku wakiendelea kupiga TAQBIR na kusema hakika Allah ndiye pekee wa kumuomba na kila uongo na Unafiki utajitenga na ukweli utajidhihirisha!!! wakati ukifika hakuna wakupinga! alimalizia kwa kusema ALLAH AQBAR!! 

Ulinzi mkali uliimarishwa ili kudhibiti hatua yoyote isiyo ya kawaida ktk kumlaki shekh Ponda ambae amekadiriwa kua na wafuasi takribani 10,000 kwa mkoa wa Dar es salaam pekee na wengine wakiwa mikoani, kutokana na hilo ulinzi ktk eneo la mahakama uliimarishwa na kua tayari kwa lolote litakalojitokeza kutokana na furaha za wafuasi hao wa Shekh Ponda.
Baadhi ya Umati wa wafuasi wa Shekh Ponda  mjini Dar es salaam


Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About