Serikali ya Uingereza
inatarajiwa kuomba msamaha pamoja na kuwalipa fidia manusura wa harakati
za ukombozi wa Uhuru wa Kenya Mau Mau.
Waliokuwa wanachama wa vuguvugu hilo
waliwasilisha kesi mahakamani kwa mateso na dhuluma walizodai kutendewa
na uliokuwa utawala wa ukoloni miaka ya 50.Zaidi ya wakenya 5,000, waliteswa baadhi wakinyanyaswa na waliokuwa wakoloni wa Uingereza.
Uingereza ilipigana vita vikali dhidi ya Mau Mau, waliokuwa wanadai ardhi na kuondoka kwa utawala wa kikoloni.
Manusura wa vita hivyo wamekuwa wakiidai Uingereza kuwalipa fidia kwa miaka mingi.
azizicompdoc.blogspot.com ina habari kuwa bwana Hague atawaomba radhi waathiriwa wa vita vya Mau Mau, wakati akitangaza kiwango cha pesa watakazotoa kama fidia kwao.
Serikali ya Uingereza awali ilikuwa imesema kuwa madai yote ya vitedno walivyofanya wakoloni ni juu ya serikali ya Kenya tangu kuipa uhuru mwaka 1963 na kuwa kwa sasa haiwezi kutakiwa kulipa.
Lakini mwaka 2011, mahakama iliamuru kuwa, wanaodai fidia, Paulo Muoka Nzili, Wambuga Wa Nyingi na Jane Muthoni Mara, walikuwa na haki ya kudai fidia kutoka kwa Uingereza .
Mawakili wao wanasema kuwa Nzili alihasiwa , huku Bwana Nyingi akichapwa vibaya wakati Bi Mara akiteswa kimapenzi katika kambi za mateso ambako waliokuwa wanapinga ukoloni walikuwa wakifungwa.
Baada ya uamuzi wa kesi hiyo, ilirejeshwa katika mahakama kuu ili kuamua pesa watakazolipwa na ofisi ya jumuiya ya madola.
Duru zinasema kuwa serikali ilikumbwa na wakati mgumu kupata mashahidi na stakabadhi muhimu kuweza kuelezea ukweli katika kesi hiyo.
Lakini Oktoba mwaka jana, mahakama iliamua kuwa waathiriwa waliowasilisha kesi hiyo mahakamani walikuwa na haki ya kufidiwa kwani walikuwa na kesi nzito dhidi ya serikali ya Uingereza.
Watatu hao walikuwa wamesema kuwa wangekubali wahusika wa kesi kuafikiana nje ya mahakama lakini pia walikuwa wanataka kufuata sheria kwani waliona wangepata haki katika mahakama.
0 comments:
Post a Comment