Ufuatiliaji wa jengo na eneo kwa dhumuni la kujenga chuo kikuu huria cha Tanzania kwa mkoa wa lindi uliofanywa na mzawa wa lindi Bw Abdulazizi Mnyengema kuanzia tar 05/03/2013 mpaka tar 14/03/2013 ktk mamlaka ya mkoa wa Lindi umezaa matunda baada ya viongozi wa mkoa huo kukubali ombi hilo la mzawa huyo kupitia ofisi yake ya chuo kikuu huria cha Tanzania lindi.
Mamlaka ya mkoa wa Lindi imeamua kuzidi kuuendeleza mkoa huo kwa kuamua
kukubali ombi la Chuo kikuu huria cha Tanzania kulichukua eneo
lisiloendelezwa kwa muda mrefu na kujenga jengo kubwa la chuo hicho na
kuwanufaisha wananchi wa Lindi na Watanzania kwa ujumla.
Kutokana na maamuzi hayo, Chuo kikuu huria kitaanda mapokezi ya eneo
hilo kutoka kwa Mamlaka ya mkoa na kukabizi gari mpya aina ya TATA
kibini mbili (Doble cabin) yenye no za usajili SU 39761 ambayo
itatumika kuchochea maendeleo ya chuo na mkoa kwa ujumla.
Wanalindi wajiandae kupokea na kuzitumia fursa hizi adimu na kuzidi kuwaunga mkono kila wenye nia nzuri na lindi.
|
Lililokua Ghala la kampuni ya usagishaji la Taifa (NMC) lililoridhiwa na mkoa kupewa Chuo kikuu huria cha Tanzania kwa uendelezaji. |
|
Gari mpya iliyonunuliwa kwa ajili ya chuo kikuu huria Lindi
|
|
Eneo la ghala hilo kwa ndani |
|
Eneo la ghala hilo kwa ndani |
|
Gari hiyo mpya kwa ubavuni iliyonunuliwa kwa ajili ya chuo kikuu huria Lindi |
Related Product :
0 comments:
Post a Comment