RAIS
Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu kurudi nchini Marekani,baada ya kumaliza
ziara yake ya siku mbili hapa nchini iliyoanza jana.
Rais Obama na mwenyeji wake Rais Jakaka Kikwete, leo walifanya ziara ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo.
Tunapenda kuungana na Rais Jakaya Kikwete na watanzania wote wapenda amani katika kumshukuru Rais wa Marekani Barack Obama kwa kuichagua Tanzania.
Pia tunawapongeza watanzania wote kwa kuonyesha umoja wetu na hata kuzika itikadi zetu za kisiasa na hata kupelekea TV zaidi ya 1000 duniani na radio zaidi ya 3000 duniani kuitazama Tanzania.
0 comments:
Post a Comment