Welcome to our online store Portal

Template Information

Saturday, August 31, 2013

OFISI YA MKUU WA POLISI YAKUTWA NA KICHWA CHA BINADAMU ALIYEFARIKI

Polisi nchini Kenya
Polisi nchini Kenya wanachunguza kisa ambacho kichwa cha mtu aliyeuawa kilipatikana kimewekwa nje ya afisi ya mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya polisi Johnston Kavuludi jijini Nairobi.
Kifurushi hichi kilichokuwa kimefungwa kwa karatasi ya plastiki, vilevile kilikuwa na mikono miwli ya binadamy iliyojaa damu.
kando ya kifurishi hicho kulikuwa na ilaani iliyoandiskwa ''Kavuludi wewe ndiye utakayefuata''.
Tangu uteuzi wake, kamishna huyo ameongoza harakati za kujaribu kuifanyia marekebisho idara ya polisi ambayo inadaiwa kuwa fisadi zaidi Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa idara ya polisi, hakuna mshukiwa aliyekamatwa kauhusiana na tukio hilo na kuwa bado wangali wanachunguza mwili huo ulikuwa wa nani.
Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na uhasama kati ya tume hiyo inayoongozwa na Kavuludi na ofisi ya mkuu wa polisi, huku zikilumbana kuhusu nani ana madaraka ya kuliendesha idara hiyo.
View detail

Wednesday, August 28, 2013

WANAFUNZI WOTE WAFELI MTIHANI WA KWENDA CHUO KIKUU


Wanafunzi wote walifeli mtihani wa kujiunga na chuo kikuu cha Liberia
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Liberia, wanafunzi wote wamefeli mtihani wao wa mwisho wa sekondari na hivyo kumaanisha kuwa hakuna hata mmoja ambaye atafuzu kuingia chuo kikuu.
Waziri wa elimu wa Liberia amesema ameshinda kufahamu ni kwa nini hakuna wanafunzi hao wamefeli kiasi hicho.
Zaidi ya wanafunzi elfu ishirini na watano walianguka mtihani huo ambao ungewapa fursa ya kujiunga na chuo kikuu cha Liberia ambacho ni moja ya vyuo vikuu vinavyoendesha na serikali.
Lakini wasimamizi wa chuo hicho wameiambia azizicompdoc.blogspot.com kuwa wanafunzi hao hawakuwa makini na ufahamu mzuri wa lugha ya Kiingereza ambayo ilitumiwa kuwatahini.
Taifa la Liberia linaendelea kujinasua kutokana na athari za mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyomalizika zaidi ya miaka kumi iliyopita.
Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, amekiri kuwa mfumo wa elimu nchini humo bado ungali duni na unahitaji marekebisho ya dharura.
Mwandishi wa azizicompdoc.blogspot.com mjini Monrovia, anasema shule nyingi nchini humo havina vifaa vya kimsingi na waalimu waliohitimu.
Lakini hii ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa wanafunzi wote kufeli mtihani huo licha ya kulipa ada ya usajili ya dola ishirini na tano.
Chuo hicho kikuu ambacho kina idadi kubwa ya wanafunzi hakitakuwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wakati muhula mpya utakapoanza mwezi ujao.
Lakini wanafunzi wengi wanasema hawajaamini matokeo ya mtihani huo na waziri wa Elimu Etmonia David-Tarpeh, ameiambia azizicompdoc.blogspot.com kuwa anatarajia kukutana na wasimamizi wa chuo hicho ili kujadili suala hilo.
View detail

Tuesday, August 27, 2013

IRAN YAIONYA MAREKANI KUHUSU KUIVAMIA SYRIA

 Jenerali wa daraja ya juu wa Iran ameionya Marekani kwamba matokeo yanaweza kuwa mabaya iwapo Marekani itapindukia ule aliosema, "mstari mwekundu" nchini Syria.  Matamshi hayo ya naibu mkuu wa jeshi la Iran, Massoud Jazayeri, yalifuata baada ya Rais Obama na waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, kukubaliana kwamba inafaa kujibu kwa uzito iwapo itagundulikana kuwa Syria ilitumia silaha za kemikali dhidi ya watu wake.  Syria imekanusha kuwa ilihusika na lile linalodaiwa kuwa shambulio lilofanywa Ghouta karibu na Damasvus juma lilopita, ambapo silaha za kemikali zilitumiwa.
Hali halisi ya Syria
Jenerali wa daraja ya juu wa Iran ameionya Marekani kwamba matokeo yanaweza kuwa mabaya iwapo Marekani itapindukia ule aliosema "mstari mwekundu" nchini Syria.
Matamshi hayo ya naibu mkuu wa jeshi la Iran, Massoud Jazayeri, yalichapishwa baada ya Rais Obama na waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, kukubaliana kwamba inafaa kujibu kwa uzito iwapo itagundulikana kuwa Syria ilitumia silaha za kemikali dhidi ya watu wake.
Syria imekanusha kuwa ilihusika na lile linalodaiwa kuwa shambulio lilofanywa Ghouta karibu na Damascus juma lilopita, ambapo silaha za kemikali zilitumiwa.
View detail

Friday, August 16, 2013

WAMISRI WAMEGOMA KUDHULUMIWA HAKI YAO

Maandamano Misri
Wananchi wa Misri wakikabiliana na Jeshi la nchi hiyo mapema mchana huu
Maandamano zaidi yamepangwa kuendelea mjini Cairo Misri, ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi wananuia kuandamana baada ya sala ya Ijumaa.
Haya yanajiri siku mbili baada ya maafisa wa usalama Misri kuvunja kambi walimokua wafuasi wa Vuguvugu la Muslim Brotherhood.Katika makabiliano hayo zaidi ya watu 500 waliuawa na maelfu kujeruhiwa.
Wakati huo huo serikali ya mpito ya Misri imemlalamikia Rais wa Marekani Barack Obama kwa kulaani mauaji ya raia waliokuwa wakiandamana.Obama amesitisha mazoezi ya pamoja na jeshi la Misri.Hata hivyo Obama hakutangaza ikiwa Marekani itasimamisha msaada wa dola bilioni 1.3 kwa jeshi la Misri.
Kiongozi wa Mpito wa Misri amesema matamshi ya Obama yanawapa nguvu makundi ya wanamgambo kuendelea kutekeleza vitendo vya kigaidi.Usalama umeendelea kuimarishwa mjini Cairo, huku magari ya kivita yakionekana kushika doria.
Muslim Brotherhood imewaomba wafuasi wake kujitokeza kwa maandamano baada ya sala ya Ijumaa wakiitaja kama siku ya hasira.Upande unaompinga Bw.Morsi umeomba maandamano kupinga vuguvugu la Mosri. Kuna wito watu kulinda makanisa na makaazi nchini Misri.Wakristo wa madhehebu ya Copt wamelengwa katika siku za karibuni.
Makanisa 25, makaazi na biashara za Wakristo zililengwa na wafuasi wa makundi ya kiisilamu hapo Jumatanona Alhamisi. Kuna hofu ya umwagikaji zaidi ya damu baada ya serikali kuonya polisi watatumia risasi kujilinda na kulinda taasisi za serikali.
View detail

Wednesday, August 14, 2013

BAKWATA YATOA TAMKO KWA SERIKALI KUHUSU SHEKH PONDA

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limelaani vikali tukio la polisi kumjeruhi Katibu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislamu, Sheikh Issa Ponda na limetaka kuundwa kwa tume huru kuchunguza tukio hilo huku likimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile kujiuzulu.
Ponda amelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi), akitibiwa majeraha yanayoaminika kuwa ya risasi aliyoyapata Ijumaa iliyopita mkoani Morogoro.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema baraza hilo limesikitishwa na tukio hilo na kusisitiza kwamba, uchunguzi huru unahitajika ili kuhakikisha kuwa wahusika wote wanakamatwa.
“Ieleweke kwamba Bakwata na Sheikh Ponda siyo maadui. Tunatofautiana mawazo tu, linapotokea suala lisilo la haki za binadamu lazima tuwe kitu kimoja,”... Sisi Bakwata Mkoa wa Dar es Salaam, tumesikitishwa na tukio hilo, tunataka tume huru ya kuchunguza kifaa kilichomjeruhi na kuwabaini wahusika ili wachukuliwe hatua za kisheria. Polisi walitakiwa kutumia njia ya weledi katika kumkamata, lakini siyo kumjeruhi kama ilivyotokea.”
Alisema Bakwata inamtaka Shilogile kujiuzulu mara moja ili kupisha tume huru itakayoundwa kuchunguza kwa ufasaha juu ya kujeruhiwa kwa Sheikh Ponda.
Alisema: “Hata kama Sheikh Ponda anatafutwa na polisi, ungetumika weledi wa kumkamata siyo kumjeruhi. Tunaamini polisi ina mbinu nyingi za kuwakamata wahalifu na Ponda kazunguka mikoa mingi ikiwemo Zanzibar walishindwaje kumkamata!” alihoji Sheikh Salum.
Alisema ikithibitika kwamba Sheikh Ponda alijeruhiwa kwa risasi au polisi walihusika, hatua kali zichukuliwe kwa wahusika kwa sababu tukio hilo linahatarisha usalama wa nchi.
Kauli ya Sheikh Salum inafanana na ile iliyotolewa na juzi na Amiri wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Yusuf Kundecha ambaye aliitaka Serikali kuunda tume huru kuchunguza tukio hilo.
Hata hivyo, Polisi imeipa jukumu Kamati ya Haki Jinai chini ya Naibu Kamishna wa Polisi, Isaya Mngulu kuanza kazi ya kuchunguza tukio hilo.
Hatua ya polisi kuanza kuchunguza tukio hilo imepingwa vikali na Sheikh Kundecha ambaye jana alisema haiyumkiniki kushiriki kuchunguza tukio hilo wakati yenyewe inatuhumiwa kuhusika.
“Umeona wapi mtu anampiga mtu halafu huyohuyo anaunda tume eti kuchunguza kipigo na aliyepiga anakuwa ndani ya tume... hii ni sawa na Tume ya Mwangosi ambayo haikuja na majibu. Kinachotakiwa ni kuundwa tume huru ikiwashirikisha Waislamu,” alisema.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alisema jana kuwa Kamati ya Haki Jinai imeshaanza kazi juzi ya kufuatilia tukio hilo kazi kubwa ikiwa ni kuchunguza namna lilivyotokea ikiwa ni pamoja na mazingira yake

Senso alisema timu hiyo imeanza kukusanya taarifa za awali na baadaye itawachukua waliohusika na tukio hilo na kwenda nao eneo la tukio kwa ajili ya kutoa ushahidi.
“Hapa duniani hakuna kinachoshindikana, wote waliokuwapo kwenye tukio tutawapata na watatueleza namna lilivyokuwa na baadaye tutatoa taarifa.”
Kuhusu kama Sheikh Ponda alipigwa risasi, alisema uchunguzi utakapokamilika, taarifa zitatolewa.
Hata hivyo, alisema bado wamemweka chini ya ulinzi na atakapopata ruhusa kutoka hospitali, watamkamata na kumfikisha mahakamani kwa makosa ya uchochezi.
Moi yakwepa
Utata kuhusu madai ya Sheikh Ponda kujeruhiwa kwa risasi umeendelea baada ya jana Msemaji wa Moi, Jumaa Almasi kusema kwamba wanachotibu ni jeraha kwa kuwa alipokewa hospitalini hapo akiwa ameshapatiwa tiba ya awali katika hospitali aliyotoka.
“Kutokana na tiba ya awali aliyopatiwa ikiwa ni pamoja na kushonwa jeraha kabla ya kufikishwa Moi imekuwa vigumu kujua kama jeraha alilokuwa nalo lilisababishwa na kitu gani,” alisema Almasi.
View detail

Tuesday, August 6, 2013

JESHI LA POLISI LATOA TAMKO KUHUSU SIKUKUU YA EID


 
Ndugu Wanahabari,

Jeshi la Polisi Nchini linatoa shukrani kwa wananchi wote wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa dini, wanasiasa, makampuni binafsi ya ulinzi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa njia mbalimbali katika kuhakikisha kwamba nchi yetu ya Tanzania inakuwa salama na raia wote wanaishi kwa amani na utulivu bila hofu ya uhalifu na wahalifu.

Katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki na za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo wanamoishi na sehemu mbalimbali zikiwemo maeneo ya biashara.

Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu. Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha kwamba, wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu, pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.

Aidha, wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara, wanatakiwa kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.

Katika kuhakikisha usalama kwenye kumbi za starehe, wamiliki wa kumbi hizo wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi. Vilevile, wazazi wawe makini na watoto wao na hasa disko toto, ili kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.

Wananchi wanatakiwa kuwa makini hususani watokapo kwenye makazi yao, wasiache nyumba wazi ama bila mtu na pale inapobidi watoe taarifa kwa majirani zao. Wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya bali watoe taarifa haraka kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu nao ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.

Vilevile, Jeshi la Polisi linawatahadhalisha wananchi kuwa makini na matapeli yanayotumia majina ya viongozi, watu maarufu na wafanyabiashara wakubwa ili kujipatia pesa na vitu mbalimbali. Matapeli hao wamekuwa wakitumia ujumbe mfupi wa simu za mkononi kupata taarifa za mtu binafsi hatimae mtu huyo kuibiwa.

Ndugu wanahabari,
Kufuatia agizo la Mhe. Rais la kuwataka watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha silaha hizo, pamoja na watu wote wanaoingia ama kuishi na kufanya shughuli hapa nchini bila kufuata utaratibu (wahamiaji haramu) kutakiwa kuondoka au kuharalisha ukaazi wao, Jeshi la Polisi linawataka watu hao kuendelea kutekeleza agizo hilo la Serikali kabla ya Operesheni kabambe kuanza itakayoendeshwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo Vingine vya Ulinzi na Usalama.

Aidha, baadhi ya watu hao tayari wamekwishasalimisha silaha wanazozimiliki kinyume cha sheria na pia baadhi ya wahamiaji haramu wameanza kuondoka hususani katika mikoa ya Kagera na Kigoma. Hiyo ni hatua nzuri, tunawataka wale wote ambao bado hawajatekeleza agizo hilo, waendelee kufanya hivyo haraka kabla ya muda wa msamaha kumalizika.

Mwisho, napenda kuwahakikishia wananchi kwamba, Jeshi la Polisi linatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria za nchi na hivyo halitawajibika kumwonea huruma ama upendeleo mtu yeyote atakayeenda kinyume na sheria.

NAWATAKIENI WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA EID –EL-FITR

Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
View detail

Thursday, August 1, 2013

ZAO LA BANGI LARUHUSIWA RASMI

Bunge la Uruguay limepitisha mswada wa kuhalalisha bangi. Ikiwa mswada huu utapitishwa na Baraza la Senate, Uruguay itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha uzalishaji na utumiaji wa bangi.
Hatua hii inaungwa mkono na serikali ikisema itapunguza mapato na faida kubwa kwa walanguzi wa mihadarati pamoja na kuwafanya watumizi wa bangi kutotumia dawa kali za kulevya.Chini ya mswada huo ni serikali pekee itakua na kibali cha kuuza bangi.
Pia serikali itatoa utaratibu wa uzalishaji, mavuno, uhifadhi na mauazo ya nje. Wanunuzi wote watanakiliwa kwenye daftari maalum na sharti wawe wametimiza miaka 18 na zaidi. Mteja anaweza tu kununua kilo 40 kwa mwezi kutoka kwa maduka ya dawa au kukuza mimea sita ya bangi.Wageni hawatakubaliwa kununua bidhaa hii.
Wabunge 50 kati ya 96 walipitisha mswada huo. Wanaotetea kuhalalishwa kwa bangi wamesema vita dhidi ya mihadarati havijapiga hatua na ipo haja kuweka mbinu mpya.
Kwa miongo mingi kanda ya Latin America imekumbwa na ghasia za magenge ya mihadarati ambapo maelfu ya watu wamekufa. Matukio ya Uruguay yanatazamwa kwa karibu eneo hilo ikiwa yatasaidia kupunguza machafuko yanayotishia uthabiti wa mataifa mengi. View detail

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop