Friday, August 16, 2013

WAMISRI WAMEGOMA KUDHULUMIWA HAKI YAO

Maandamano Misri
Wananchi wa Misri wakikabiliana na Jeshi la nchi hiyo mapema mchana huu
Maandamano zaidi yamepangwa kuendelea mjini Cairo Misri, ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi wananuia kuandamana baada ya sala ya Ijumaa.
Haya yanajiri siku mbili baada ya maafisa wa usalama Misri kuvunja kambi walimokua wafuasi wa Vuguvugu la Muslim Brotherhood.Katika makabiliano hayo zaidi ya watu 500 waliuawa na maelfu kujeruhiwa.
Wakati huo huo serikali ya mpito ya Misri imemlalamikia Rais wa Marekani Barack Obama kwa kulaani mauaji ya raia waliokuwa wakiandamana.Obama amesitisha mazoezi ya pamoja na jeshi la Misri.Hata hivyo Obama hakutangaza ikiwa Marekani itasimamisha msaada wa dola bilioni 1.3 kwa jeshi la Misri.
Kiongozi wa Mpito wa Misri amesema matamshi ya Obama yanawapa nguvu makundi ya wanamgambo kuendelea kutekeleza vitendo vya kigaidi.Usalama umeendelea kuimarishwa mjini Cairo, huku magari ya kivita yakionekana kushika doria.
Muslim Brotherhood imewaomba wafuasi wake kujitokeza kwa maandamano baada ya sala ya Ijumaa wakiitaja kama siku ya hasira.Upande unaompinga Bw.Morsi umeomba maandamano kupinga vuguvugu la Mosri. Kuna wito watu kulinda makanisa na makaazi nchini Misri.Wakristo wa madhehebu ya Copt wamelengwa katika siku za karibuni.
Makanisa 25, makaazi na biashara za Wakristo zililengwa na wafuasi wa makundi ya kiisilamu hapo Jumatanona Alhamisi. Kuna hofu ya umwagikaji zaidi ya damu baada ya serikali kuonya polisi watatumia risasi kujilinda na kulinda taasisi za serikali.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About