Tuesday, September 24, 2013

KENYA BADO HALI SI SHWARI


Vikosi vya usalama nchini Kenya vinasema viko katika mkondo wa lala salama katika kuweza kudhibiti jengo zima la Westgate. Hadi sasa serikali inasema kuwa mateka wote wameokolewa huku wanamgambo sita waliosalia wakiuawa usiku wa kuamkia leo.

 
Polisi wakikabiliana na wanamgambo hao waliokuwa wameteka jengo la Westgate
Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa usalama idadi kamili ya magaidi waliouawa ni tisa
Duru kutoka shirika la AFP zinasema kuwa majeshi ya Kenya yangali yanakabiliana na gaidi mmoja au wawili ambao wamesalia ndani ya jengo la Westgate.
Inaarifiwa magaidi hao walijitawanya wakiwa ndani ya jengo hilo kila mmoja akijificha sehemu yake katika ghorofa ya juu zaidi ya jengo hilo.
Milio ya risasi na milipuko ilisikika mapema leo asubuhi kutoka katika jengo hilo.
Ukabilianaji huo ulitokea baada ya serikali ya Kenya kutangaza kudhibiti jengo hilo zima huku hali hiyo ikishuhudiwa kwa siku ya nne.
Serikali ilisema kuwa mateka wote wameokolewa ingawa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu hali ilivyo sasa.

Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About