Monday, September 23, 2013

YANGA YAZIDI KUDONDOKA KILELENI


Vinara Simba wanaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 11 na mabao yao 13 ya kufunga na kufungwa magoli manne, huku JKT Ruvu ikifuatia ikiwa na uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa ikiizidi Azam licha ya kulingana nao pointi 9 sawa na Ruvu Shooting na Coastal Union.
Azam yenyewe imefunga mabao nane na kuruhusu mabao matano, wakati JKT Ruvu imefunga mabao sita na kufungwa mawili na kuwa, ikifuatiwa na ndugu zao Ruvu Shooting waliofunga mabao sita na kufungwa matatu kisha Coastal iliyofunga magoli matano na kuruhusu nyavu zake zitikiswe mara mbili.

Kagera Sugar iliyoanza ligi kwa kusuasua ushindi wake wa jana dhidi ya Ashanti umeiweka katika nafasi ya sita ikiwa na pointi nane na kufuatiwa na Mbeya City wenye pointi saba kisha Yanga yenye pointi zake sita.
Oljoro JKT iliyokuwa nafasi ya pili toka mkiani imechupa hadi nafasi ya 11 mwa msimamo baada ya ushindi wake wa leo dhidi ya JKT Ruvu ikifikisha pointi nne na kuirithisha nafasi hiyo Prisons-Mbeya huku Ashanti wakiendelea kuzibeba timu zote 13 za ligi hiyo ikiwa na poingti moja tu.
MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA HUU HAPA


Mpaka sasa ligi ikijiandaa kuingia raundi ya sita siku ya Jumatano kwa pambano moja tu kati ya Rhino Rangers ya tabora itakayoialika Ashanti United mjini Tabora jumla ya mabao 76 yameshatinga wavuni, huku Tambwe Amissi wa Simnba akiongoza orodha ya wafungaji wenzake akiwa na mabao sita.
Tambwe anafuatiwa kwa mbali na washambuliaji nyota wa Yanga, Jerry Tegete na Didier Kavumbagu na Haruna Chanongo, mchezaji wenzake wa Simba wenye mabao matatu kila mmoja.

Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About