Monday, October 7, 2013

JESHI LA MISRI LAPATA PIGO

Kuna wasiwasi kuwa wanajeshi na vikosi vya usalama vinalengwa kwa mashambulizi ya Misri
Watu waliojihami nchini Misri wamewaua wanajeshi watano (5) katika eneo la Mkondo wa Suez mjini Ismailiya.
Maafisa wa usalama wanasema kuwa washambuliaji waliwafyatulia risasi wanajeshi hao walipokuwa wanaketi karibu na kizuizi cha barabarani kaskazini mwa mji huo.
Maafisa wa usalama wanasema kuwa wanajeshi wamekuwa wakilengwa kwa mashambulizi katika siku za hivi karibuni.
Wakati huohuo, mlipuko mkubwa uliotokana na bomu liliokuwa limetegwa ndani ya gari limelipuka na kuwaua watu wawili.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About