Shehena ya meno ya tembo yanaswa Uganda
Maafisa nchini Uganda wamekamata
shehena meno ya tembo yenye uzito wa tani mbili, ambacho ni kiwango
kikubwa kukamatwa kwa miaka mingi iliyopita.
Chama cha Wanyama Pori nchini Uganda kimesema meno yapatayo 832 yenye thamani ya dola milioni 6.7 yamekamatwa.Kuna mahitaji ya meno ya tembo kutoka barani Afrika kwenda nchi Asia kwa ajili ya kutengeneza mapambo.
Meno hayo ya tembo yalikuwa yakielekea kwenda kusafirishwa katika bandari ya Mombasa nchini Kenya.
Baadhi ya meno hayo yalikuwa yamekatwa vipande vipande na kufunikwa na chupa za plastiki kwenye makreti na kubandikwa maandishi kuonyesha kwamba ni bidhaa zinazokwenda kuchakatwa (recycling).
Chama hicho cha Wanyama pori kimemwambia mwandishi wa habari wa azizicompdoc.blogspot.com kuwa Uganda imeanza kutumiwa na majangili kama njia ya kupitisha bidhaa za wanyamapori kutoka nchi za Sudan Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
0 comments:
Post a Comment