Friday, October 4, 2013

SEHEMU YA 3: WAJUA FUKUTO KUHUSU RASIMU YA KATIBA?

MAMLAKA YA MWANANCHI UTII NA HIFADHI YA KATIBA
(g) utu, heshima na haki nyingine zote za binadamu
zinahifadhiwa na kudumishwa kwa kuzingatia mila na
desturi za kitanzania na kwa kufuata mikataba mbalimbali
iliyoridhiwa na Jamhuri ya Muungano;
(h) mamlaka za nchi zinatoa fursa na haki zilizo sawa kwa
wananchi wote, wanawake na waume, bila ya kujali rangi,
kabila, nasaba, dini au hali ya mtu;
(i) aina zote za dhulma, vitisho, ubaguzi, unyanyasaji,
rushwa, uonevu au upendeleozinaondolewa nchini;
(j) utajiri wa rasilimali na maliasili za Taifa unaelekezwa
katika kuleta maendeleo, kuondoa umaskini, ujinga na
maradhi; na
(k) nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na
kujitegemea.
Mamlaka na
utii wa Katiba 8.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba za Washirika wa
Muungano kwa mambo yasiyo ya Muungano, Katiba hii itakuwa sheria
kuu katika Jamhuri ya Muungano.
(2) Mtu yeyote, chombo, taasisi, jumuiya na wakala wowote wa
mamlaka ya nchi na mamlaka binafsi zinao wajibu wa kuzingatia
masharti ya Katiba hii na kuyatii.
(3) Sheria yoyote, mila, desturi au uamuzi wowote wa chombo
cha dola, ofisa wa Serikali au mtu binafsi ni sharti ufuate na kuendana na
masharti yaliyomo kwenye Katiba hii na kwamba, sheria, mila, desturi
au uamuzi wowote ambao hautawiana au kwenda sambamba na masharti
ya Katiba hii utakuwa batili.
Quantity : Add to Cart

No comments:

Post a Comment

Labels

Blogroll

Labels

About