Welcome to our online store Portal

Template Information

Sunday, November 24, 2013

MARUFUKU MWEKEZAJI KUFANYA BIASHARA NDOGO NDOGO ZIMBABWE


Wamiliki wa makampuni ya nje yanayoendesha shughuli katika baadhi ya sekta nchini Zimbabwe kuanzia Januari mosi mwaka 2014 hawataruhusiwa na iwapo watakiuka agizo hilo watakamatwa mmoja wa maafisa waandamizi wa serikali ya nchi hiyo amesema.
Katibu wa Uwezeshaji Uchumi George Magosvongwe alitoa onyo katika bunge la nchi hiyo, gazeti moja la serikali limesema.
Kumilikisha uchumi kwa wanyonge ni moja ya kampeni ya Rais Robert Mugabe katika uchaguzi uliofanyika mwezi Machi.
Kilimo, maduka ya kunyoa nywele, biashara za saluni, biashara ya kuuza vitafunio ni miongoni mwa kazi zitakazofanywa na wazawa pekee nchini humo.
"Kuanzia Januari mosi mwezi mmoja unaokuja tutaanza kuchukua hatua na tayari tumeandaa utaratibu na hatua za kuchukuka kwa wal watakaokiuka agizo hilo," Gazeti la serikali ya Herald limemnukuu Bwana Magosvongwe akisema.

Amesema raia wa Zimbabwe wamekwishaandaliwa ili kuchukua nafasi za kuendesha shughuli zilizokuwa zikiendeshwa na wageni ili kuepuka upungufu wa bidhaa.
Kwa mujibu wa gazeti la Herald biashara zilitengwa kwa wazawa ni pamoja na biashara za reja reja na jumla, maduka ya kunyoa, biashara za saluni, biashara za kutengeneza na kuuza vitafunio, kilimo , usafirishaji, biashara za majengo na matangazo.

Amesema migahawa inayomilikiwa na wageni ambayo haitengenezi vyakula vya asili haitaathirika.
Wamiliki wa biashara ambao hawatakidhi vigezo vya biashara za wazawa watakuwa katika hatari ya kupigwa faini au kifungo kama wataendelea kufanya biashara hizo gazeti la Herald limesema.

Related Product :

0 comments:

Post a Comment

Why Shop on Bongo Online?

We make your shopping experience easy and exciting with our multiple payment options, amazing deals and unbeatable prices. You may pay on delivery or online with your Mobile Money. We fulfill your orders within the estimated time frame at your preferred location. We are committed to serving you, and your satisfaction is of utmost importance to us. Rest assured that for a wonderful shopping experience, Bongo Online Shop is the best place to be

About

Swissgear Smart Bag

468x60 Ads

HIDDEN CAMERA

Support : tzamaizing@gmail.com | Tzamaizing Template | +255 653 33 29 24
Copyright © 2015. AZIZI COMPUTER DOCTOR - All Rights Reserved
Template Created by Tzamaizing Published by Tzamaizing
Proudly powered by Bongo Online Shop